FASIHI ANDISHI-KWA KIDATO CHA TATU NA NNE.
1.Fasihi hubeba yote anayoibusha binadamu katika maisha yake ya kila siku.Jadili kauli hii kwa mifano- Maudhui (Dhamira)
2.Fasihi hubeba yote anayoibusha binadamu katika maisha yake ya kila siku.Jadili kauli hii kwa mifano- Maudhui (Dhamira)
3.Jadili vipengele viwili vya fani na vitatu vya maudhui vilivyojadiliwa katika riwaya uliyosoma.(Fani na maudhui)
4.Ujumbe wa Tamthiliya ya Kilio chetu na Orodha una umuhimu mkubwa katika Tanzania ya leo.Jadili kauli hii kwa kutumia vitabu hivyo vilivyotajwa.Maudhui (Ujumbe)
5.Taswira ni kipengele muhimu sana kwani huipamba lugha ya ushairi na kufikisha ujumbe kwa hadhira .Onesha ukweli wa kauli hii kwa kutumia vitabu viwili ya ushairi ulivyosoma kati ya vilivyosoma kati ya vilivyoorodheshwa hapo juu. Fani ( Taswira ilivyoibua ujumbe)
6.Jadili kufaulu na kutofaulu kifani kwa waandishi wa vitabu viwili vya riwaya ulivyosoma.(Fani kwa ujumla kufaulu na kutofaulu)
7.Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma chagua wahusika watatu kwa kila kitabu na uoneshe jinsi wahusika wanavyopaswa kulaumiwa na jamii.Wahusika (dhamira au ujumbe mbaya/wasifu mbaya)
8.Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.Fani (Taswira zilivyoibua ujumbe)
9“Waandishi wa kazi za fasihi huibua migogoro mbalimbali na kupendekeza suluhisho ili kuelimisha jamii husika”. Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.Maudhui(Migogoro ilivyoibua ujumbe)
10.Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, fafanua madhara yanayotokana na kukosekana kwa elimu ya jinsia kwa vijana kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila kitabu.Maudhui (Madhara ya usefu wa elimu ya kijinsia)
11.Jadili namna jina la kitabu la mwandishi wa tamthilia uliyosoma linavyoweza kubeba wazo kuu la mwandishi wa kazi ya fasihi.(Swali linaweza kulenga riwaya,mashairi na tamthiliya) Fani (Fafanua ujumbe uliopo katika jina la kitabu)
12.Jadili matumizi ya jazanda yalivyojitokeza katika tamthiliya uliyosoma.(swali hili linaweza lulenga riwaya na mashairi/diwani) Fani ( Taswira)
13.Kwa kutumia riwaya uliyosoma, fafanua jinsi mwandishi alivyoweza kuwatumia wahusika wawili katika kuibua maudhui yake.Fani (Wahusika na maudhui( ujumbe,dhamira,migogoro)