Enter your keyword

Culture for Life.

Wednesday, January 30, 2013

Nafasi ya kazi ya Secretary

By On January 30, 2013
SECRETARY ANATAFUTWA
Chuo cha Fountain kilichopo Arusha sakina kinatafuta karani mwenye sifa zifuatazo:

  •  awe amesomea kozi ya Ukarani          
  •  Elimu kidato cha nne na sita au kuendelea.piga simu zilizopo katika tangazo la chuo hapo juu               

Makeke Africa na ingizo jipya(wapo DSM)

By On January 30, 2013
 ingizo jipya kutoka Makeke Africa

Saturday, January 19, 2013

Historia ya lugha ya kiswahili

By On January 19, 2013
 HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI.
Kiswahili ni lugha ambayo inawekwa katika kundi la lugha za Kibantu. Neno “Swahili” linatokana  na neno la Kiarabu “sahel” linalomaanisha “sawahil” na katika Kiswahili ni “mpaka” au “pwani”(linalotumika kama kivumishi kumaanisha “wakazi wa pwani”. Kuongeza kwa herufi mbili za “ki” [‘lugha’] kupata “Kiswahili” kumaanisha “lugha ya pwani”. Wakati mwingine, neno “sahel” linatumika kumaanisha “mpaka wa jangwa la Sahara”. Unganishaji wa herufi ‘i’ mwisho wa neno “Kiswahili” ni kutokana na umbo la  kivumishi katika lugha ya Arabu (‘sawahil’). Jambo la hakika ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo imeazima maneno kutoka Kiarabu, Kiuajemi, Kireno na hivi karibuni Kiingereza. Hali hiyo, imekifanya Kiswahili kufika kiwango cha lugha ya kisasaZamani, Waswahili walitumia utawala wa mfumo wa mamlaka moja. Karibu na karne ya 10, pwani nzima ya Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa mfalme mmoja ambaye aliishi katika mji mkuu wa Safala.

Karibia karne ya 14, jamii ya Waswahili ilibadilishwa kuwa nchi yenye miji ya kisasa. Miji mingi hiyo ilikuwa midogo yenye majengo ya jiwe, misikiti, familia ya Waislamu walio na tabaka la juu na wengine wengi ambao hawakuwa Waislamu. Majiji makubwa kama Mogadishu, Pate, Mombasa, Malindi, Zanzibar na Kilwa yalijengwa na marijani na matumbawe ambayo yalionesha dalili za utajiri kwani yalikuwa  na vifaa vya ujenzi  vya gharama sana. Idadi kubwa ya majiji hayo yalikuwa chini ya utawala wa Sultani ambaye alikuwa Mwislamu. Ilifika kipindi ambacho majiji makubwa hayo yalitawala mengine ambayo hayakuwa na uwezo wa kuchukua mamlaka. Kwa mfano, Sultani wa Kilwa alitawala sehemu kubwa ya pwani ikiwemo Sofala na Zanzibar. karne ya 14 (kipindi cha mwaka 1390) idadi kubwa ya miji iliyotawaliwa na Masultani wa Omani kama Sofala ilianza kupata uhuru. Kuanzia karne ya 8 mpaka 19, Kiswahili kilizumgumzwa na makabila kadhaa kwa umbali wa maili 1000 kwenye pwani ya Afrika Mashariki kati ya Mozambique na kusini kwa Somalia.

Kwa mamia ya miaka,sehemuambazo palikuwa na Waswahili palikuwa vituo vya biashara muhimu kati ya wenyeji na nchi kama Arabia, India na Asia Mashariki na raslimali za Afrika Mashariki. Ushirikiano huu wa kibiashara uliathiri jamii ya wenyeji (Waswahili), utamaduni, dini na lugha  katika Afrika Mashariki. Katika enzi za karne ya 19, Kisiwa cha Zanzibar kilikuwa kituo kikuu na cha umuhimu kwa ajili ya biashara iliyokuwapo kwenye pwani ya Afrika Mashariki; sehemu ambapo safari ya watu na usafirishaji wa bidhaa kwenda katikati ya eneo hilo (Afrika Mashariki). Wakati huo, Kiswahili kilitumika kama lugha ya biashara na ya mawasiliano. Kutokana na hali hii, watu wengi ambao ni Waswahili walihamia kuishi kwingine hasa katikati ya Afrika Mashariki kwa lengo la kufanya biashara.

Naye Profesa Whiteley (1969), amefafanua hali hii akisema,“Wakati upanuzi wa biashara ulipobadili mbinu ya biashara kwa kutumia msafara kutoka pwani, haja ya kuhitaji lugha muafaka wa biashara ulikuwa muhimu sana na hapo ndipo Kiswahili kilipojizindua jukwaani”.(“When the expansion of trade shifted the initiative to caravan from the coast, the need for an effective lingua franca became acute and Swahili came into its own”).Baadaye, yaani katika karne ya 20, wakati wa ukoloni wa Uingereza, lahaja ya Unguja (aina ya Kiswahili iliyotumiwa na Wazanzibari ilienea sana Tanzania na aina nyingine ya Kiswahili ilienea mpaka Kenya, Uganda, Burundi, Congo, Mozambique na ilifika mbali sana hata mpaka Afrika Kusini. Aina hii ya Unguja ilikuwa imeathirika sana na Kiarabu.

Aina nyingine zilizojitenga kutoka Unguja zilipitia mabadiliko tofauti wakati wa usambazaji wa Kiswahili. Kwa sasa, tuna aina nyingi za Kiswahili zinazotofautiana angalau kidogo sana katika lugha hii ya Kiswahili. Ni muhimu kukumbuka kwamba kulikuwa na sababu moja ambayo ilisababisha usambaaji wa Kiswahili. Hii ilikuwa hali ya kuoana miongoni mwa wafanyabiashara (ambao walikuwa Waswahili) na wenyeji ambao wengi walikuwa watumwa. Inakubalika bila shaka kwamba watoto waliozaliwa na familia ya mchanganyiko huo walipata nafasi ya kujua na kuongea Kiswahili.

Bongo flava na historia yake

By On January 19, 2013
Historia fupi ya muziki wa kizazi kipya
  ulianzishwa na Wamerekani weusi huko the Bronx, New York Marekani mnamo mwaka 1970.Wamerekani wenye asili ya Afrika ,ambao babu zao walichukuliwa kwenda Marekani kama watumwa.Elementi hizi za utamaduni wa hiphop zilikuwa zikijitokeza kwa awamu moja  na inapofifia inaibuka nyingine ,ilivyo ni kwamba ilianza grafiti ikafuatwa na udijei,mabreka,halafu rap(yasin,2001;rose1994;toop2000;mitchel2001;southern1983).
Mizizi hasa ya rap Afrika, mbali ya kuanzishwa na wamarekani weusi una sifa mbalimbali za kimuziki na kifasihi simulizi za kiafrika ikiwa ni pamoja na matumizi ya midundo au ridhimu usimulizi,kiitikio na majigambo.Hiphop au muziki wa kizazi kipya ulikuwa kama jukwaa la mshikamano miongoni mwa vijana wa kimarekani  wa mjini na baadaye kuwa kama mtindo  wa maisha na sauti ya vijana .Ni utamaduni ambao uliwakutanisha wale walionyimwa haki ,walionyanyaswa  na kugandamizwa katika historia  na ukawa utambulisho  miongoni mwa Wamerekani weusi na ukawa kipaza sauti chao.

Muziki wa kizazi kipya au rap nikipengele kimoja wapo  cha utamaduni wa hiphop.Ni aina ya ushairi ,usimuliaji,au usemaji unaopangwa vina kwa kufuata mdundo wa ala  za muziki (ambao tayari ulisharekodiwa ).Muziki huu ulianza kama sehemu ya burudani  ya vijana weusi na baadaye  ukakuwa na kuenea  na kuwa maarufu  katika nchi nyingi  duniani .Hapa Tanzania  muziki wa kizazi kipya ulianza mwaka 1980.Vijana walianza  kuimba wakiwa ufukweni na baadaye katika sherehe mbalimbali ulianza kisikika redioni  mwaka 1995.
Kama ilivyokuwa kwa Wamerekani weusi vijana wengi  wa Kitanzania pia hutumia muziki wa kizazi kipya  kuelezea matatizo yao  ya kila siku kama vile ukosefu wa ajira  na athari zake ,Dola na nguvu zake  na umasikini.Hapo mwanzoni  nyimbo hizi ziliimbwa kwa kuwaiga wasanii wa  kimarekani  kama vile Vanillah Ice,Kriss Kross na Naughty by Nature, halikadhalika walitumia  baadhi ya maneno au sentensi kutoka nyimbo hizo .Hivyo kila mwimbaji  alijaribu kuwa mbunifu na kutunga nyimbo zake mwenyewe ilikuwapata mashabiki na kujiongezea umaarufu.Muziki wa kizazi kipya unaojulikana sana kwa jina la Bongo flava ulishika kasi sana mwaka2000.muziki huu umewapatia vijana wengi  fusra baada ya kusikia nyimbo kutoka n’je ya

Tanzania  hususani marekani ambapo vijana waliiga na kutoka na staili yao wakitumia lugha ya Kiswahili na wengine walichanganya nyimbo hizo na lugha kama Kingereza na lugha za asili.
Walichoweza kufanya vijana wengi ni kuiga (ala) za Wamerekani lakini waliamua kutumia lugha ya Kiswahili ili kuweza kufikisha ujumbe  kwa Watanzani na kama inavyojulikana kuwa kazi yoyote ya sanaa ina malengo  ya kufundisha ,kukosoa na kuburudisha.Wakati muziki huu unaanza Tanzania  hakuweza kuzaniwa kama unge fika karne za mbele lakini hivi sasa una waimbaji wengi pamoja na mashabiki wengi wa rika tofauti hasa vijana, watu wazima si wote wanao upenda muziki huu.
Baadhi ya vijana waliokuwa waanzilishi wa muziki huu kwa Tanzania,vijana wa mwanzo kabisa ambao kuanzia mavazi yao na kufokafoka kwao kulikuwa ni burudani tosha kwa watu kuanza kudadisi kuhusu utamaduni wa mavazi hayo ambayo yalionekana  kama uhuni tena wa kupita kiasi kutokana na uvaaji wa mavazi hayo kihip hop.Hawa ni baadhi ya wasanii wachache ambao walivaa kihip hop Samora Avenue,John simple,DJ Rusual,The BIG ONE,Babu manju,Davidi,Nhigula,Abdulhakim Magomelo,Kessy,Ibony Moalim,Tom
 London,Opp(now JayP)  NA DJ Ngomeley.Hao walikuwa chachu katika uvaaji wa kihiphop na katika kughani Muziki huu wa kizazi kipya.
Pia kuna wasanii wa mwanzo kabisa katika kuimba muziki huu wa kizazimkipya akiwepo mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (BBG lianza na MR.11)FreshXE Mtui,Adili Kumbuka,KBC(Mbeya Tech)Saleh Jabir,Samia X,The Big,Rhymson,2Proud,Kwanza Unit,GWM,Hard Blasters na Bantu pound ambao walianza kuimba katika sherehe za mashuleni,kwenye matamasha mtaani kabla hata ya kurekodi nyimbo zao studio. Kulikuwa na wale wenye kuimba kama wanamuziki wengi wa Marekani kwa kupitia matamasha mbali mbali katika Jumba la utamaduni la Urusi,Korea na mengineyo yaliyokuwa yakiandaliwa hasa na wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari jijini kama Forodhani pia matamasha yaliyokuwa yakifanyika kando kando ya ufukwe ambako wengi wenye kutaka kuimba walijitokeza.

Kulikuwa na  kundi kama la Mawingu na mwana dada Pamela,mwanadada Stara Thomas na Judith Wambura ambao uwezo wa kughani na kuimba kama Mc Lyte ulimuinua hasa alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha DJ show ya Radio One,shukrani kwa Ipyana Malecela Mkwavi (RIP) kwa zawadi ya LP yenye mdundo,ala ya single “Keep,Keeping on” ndiyo iliyomtambulisha Jay Dee wa leo Radioni kwa mara ya kwanza japokuwa kabla ya hapo alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani lakini mweye kusita kuingia kwenye muziki wa kidunia.
Pia Kundi la R&B lililojulikana kama Four Krewz Flava pia Herbert Makange ambaye pia alikuwa akiimba. Kwa kufanya haya na mengineyo mengi muziki huu sio tu utakuwa ni wenye kujijengea heshima bali kuweka kumbukumbu kubwa ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania na hadhi yake kuwa ni ile isiyofutika kwa urahisi machoni na akilini mwa kizazi cha sasa na hata kile kijacho kwa muda mrefu.

Pants on the ground/ijue historia ya uvaaji wa milegezo

By On January 19, 2013

Ijue historia ya uvaaji wa milegezo






kinadada tujirekebishe wengi wenu hata mambo yetu yale huwa mnayaonyesha(shanga na cheni za kiunoni)

 

Ninayofuraha kubwa leo katika safu hii ya urembo kuzungumzia suala hili la uvaaji wa milegezo kwa vijana wetu wa kiafrika.Nimeandika mada hii Kutokana na wasomaji  kuomba  sana makala hii,tunaambiwa kuwa uvaaji wa mwanaume au mwanamke hudhiirisha umri wake,Kuna baadhi ya mavazi ambayo ukimuona mtu kavaa bila kuuliza utajua tu huyu ni mtu mzima na ndiyo sababu ukimuona bibi kavaa mitindo ya mabinti wa sasa ataitwa bibi kijana au mzee kijana.Nakubaliana na hili kuwa uvaaji wa suruali wa mwanaume huendana na umri alio nao, wakati vijana wengi hushusha suruali zao chini ya makalio  huku wanaume wanaoanza kuzeeka huzipandisha suruali zao juu ya kiuno.

Binafsi naona kuwa  kuna uhusiano wa uvaaji wa suruali wa mwanaume na umri wake.Jaribu kuchunguza watoto chini ya miaka 12 kawaida huvaa suruali zao kwenye usawa wa kiuno kwakuwa  umri huo hununuliwa nguo na wazazi wao na wakati mwingine kuvalishwa na wazazi wao.Sasa kijana anapo kuwa tayari amekuwa(amebalehe) ndipo muonekano wake wa uvaaji unabadilika na kuanza kuvaa milegezo au kata K kama wanavyoita mtaani.
Leo mpenzi msomaji wa safu hii nataka nikujuze tu ili uweze kujua uvaaji huu umetoka wapi?.Hapa Tanzania mtindo huu hujulikana zaidi kama  kata K au mlegezo na  vijana wengi  wanaopenda kuvaa nguo za ndani maarufu kama  Boska(Boxer) au kaptula hushusha suruali zao chini ya makalio,mimi huwa sielewei kwamba tatizo huwa nini? au wenzetu mnaogopa kubanwa viuno vyenu na mbaya zaidi nguo wanazozionyesha huwa chafu na mda mwingine huwa na maandishi mabaya(cow boy) na zaidi zingine mpaka bei yake huwa mbovu nikimaanisha bei ya chini.

Mtindo wa mlegezo uliigwa kutoka mfumo wa magereza nchini Marekani ambako mikanda ilipigwa marufuku katika magereza ili kuzuia wafungwa kujinyonga. Lakini mtindo huu ulikuja kupewa umaarufu na wasanii wa muziki wa hip-hop katika miaka 1990 na tangu wakati huo umekuwa kama alama ya uhuru na utambuzi wa kitamaduni au alama ya kukataa maadili ya jamii.Jaribu kukumbuka kuanzia bongo flava ilipo anza hapa Tanzania vijana wengi waliokuwa wakiimba bongo flava na wanafunzi  walipendelea kuvaa milegezo kutokana na kuwaiga wasanii wa hip hop wa Marekani na kusahau maadili na utamaduni wetu kama Watanzania ingawa tatizo hili lipo  hadi sasa, kuna vijana ambao hawawezi kuacha kuvaa milegezo.
Naomba ni mnukuu kijana Elias mkazi wa Arusha   anazungumziaje? suala hili la uvaaji wa milegezo" kiujumla mimi wana ni kera na siku moja nilikuwa katika daladala  na konda wa daladala aliinama mbele yangu nguo chafu  huku suruali ikiwa chini ya makalio  nilichokifanya nilimpandisha suruali kisha nika mwambia vaa vizuri bwana unavaavaa vibaya halafu unaniinamia watu kwenye daladala walikaukia kucheka na konda hakushusha tena suruali yake mpaka tumefika "Ninachojaribu kukisema hapa  ni kwamba naomba tubadilike kama mnavyo wazungumzia watoto wa kike na mavazi yao kuwa yanakwenda kinyume na utamaduni wetu hivyo hivyo kwenu nyinyi wanaume haipendezi ukiwa una tembea njiani au umeongozana na mama,bibi,baba hata mchumba wako  na unaona kawaida tu kuvaa hivyo kiukweli hapendezi naomba niifanananishe uvaaji huo na muonekano wa makalio ya nyani kama kijana  badilika ,ukivaa vizuri utaonekana mstaarabu daima hata kama unafanya biashara watu watavutia kutokana na uvaaji wako bila kuwa sahau dada zangu mnao vaa blauzi fupi na mkiinama nguo zenu za ndani zionekana naomba tuhistili miili yetu vema .

Mpenzi msomaji usichoke kuendelea nami katika safu hii kuanzia wiki ijayo nitaendelea kukupa mada mbalimbali za urembo na mitindo,wiki hizi mbili tulikuwa tunawekana wazi katika suala zima la uvaaji kwa upande wa wanaume na wanawake.


abnerytupokigwe@gmail.com

Tuesday, January 15, 2013

FORM FOUR 2013 result ,THE FOUNTAIN JUSTICE COLLEGE ARUSHA

By On January 15, 2013


THE FOUNTAIN JUSTICE TRAINING COLLEGE ARUSHA
  P.O. BOX 13190 ARUSHA.REG.214118

   MAHALI:-SAKINA KIBANDA MAZIWA,ARUSHA
WASILIANA:  0713045707
                  0786-164-966
                  0752-129-462
CHUO KINAWATAFUTIA KAZI WANAFUNZI WANAOFAULU VIZURI:
COURSEDURATIONAMOUNT'TSH
HOTEL MANAGEMENT
1YR
        480,000/=
TOUR GUIDING
1YR
480,000/=
TOUR OPERATION AND TRAVEL MGT
1YR
600,000/=
TEACHING (Earlier Childhood Education)
1YR
600,000/=
MARKETING
1YR
720,000/=
HUMAN RESOURCE     MGT
1YR
600,000/=
SECRETARIAL STUDIES
1YR
600,000/=
BUSINESS STUDIES
1YR
720,000/=
COMMUNITY DEVELOPMENT
1YR
720,000/=
SALES & MARKETING
1YR
720,000/=
PURCHASING & SUPPLY MANAGEMENT
1YR
720,000/=
ENTERPRENEURSHIP
1YR
        600,000/=
COMPUTER APPLICATION
3 MONTHS
150,000/=
PROJECT  PLANNING AND  MANAGEMENT
1YR
720,000/=
HAIR DRESSING, BEAUTY THERAPY
6 MONTHS
480,000/=
HIV/AIDS COUNSELLING
1YR
        600000/=
MALAZI:HOSTEL ZINAPATIKANA KWA TSH25,000 KWA MWEZI  BILA CHAKULA

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu