Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 15, 2012

Baadhi ya wachezaji wa Tanapa ktk viwanja vya jamhuri Dodoma wakiwa wameshikilia makombe baada ya kushinda katika mashindano ya SHIMUTA mwezi wa 11/2012

By On December 15, 2012

Meneja wa timu(Namweni)akiwa ameshikilia moja ya kombe la ushindi katika viwanja vya jamhuri Dodoma.
TANAPA ilinyakuwa makombe 6 katika mahindano ya SHIMUTA  Mwaka huu(2012)huku busketball wanawake ikiwa Mshindi wa kwanza,Mpira wa miguu washindi wa pili,mpira wapete washindi wa pili,dusk mshindi wapili,pooltable mshindi wa pili,riadha mshindi wakwanza na wapili

vyakula vya msingi kwa ubora wanywele zako

By On December 15, 2012

Fahamu vyakula vya msingi kwa ajili ya ubora wa nywele zako
Karibu tena mpenzi msomaji wa makala hii ya Urembo na Mitindo inayokujia kila wiki kupitia safu hii.Katika makala hii nitazungumzia utunzaji wa nywele  kwa wanaume na wanawake .Nitakutajia vyakula ambavyo hufanya nywele kuwa imara  na  zenye mvuto asilia,Watu wengi hulalamika  nywele kukatika,kuwa nyepesi,kuwa kavu na kukosa mvuto.
Watu wengi hupenda kutumia vyakula mbalimbali bila ya kufahamu umuhimu wa vyakula hivyo katika miili yao.Vifuatavyo ni vyakula ambavyo hufanya nywele zako kuwa imara, na vyakula hivi si vigeni katika maisha yetu ya kila siku.
Maharage
Maharage yana protini nyingi kama vile zinc, biotin pamoja na madini ya chuma ambayo hufanya nywele kuwa na virutubisho na muonekano mzuri. Maharage ni mboga inayopendwa na watu wengi, pia ni rahisi kupatikana.  Kadri unavyoitumia ndivyo nywele zako zitakavyozidi kuwa bora na imara zaidi.
Mayai na Maziwa
Watanzania wengi hawana mazoea ya kunywa maziwa huku wengi wakijenga imani potofu kuwa maziwa hufaa kwa watoto wadogo pekee.Maziwa yanaprotini nyingi ambazo husadia kutoa vurutubisho katika nywele na kuzuia kukatika.
Mayai
Mayai pia yanaprotini nyingi ambazo husaidia nywele zako kuwa imara na huzuia  zisikatike hovyo.Hata ukijaribu kuchunguza baadhi ya shampoo ambazo hutumika kusafishia nywele huwa zimetengenezwa kwa mchanganyiko wa kemikali mbalimbali pamoja na mayai.
Samaki
Samaki ni miongoni mwa vyakula muhimu sana katika kustawisha nywele na kuzifanya ziwe imara na zenye muonekano mzuri. Matumizi ya samaki katika mlo husaidia kuzifanya nywele zako kuwa imara toka kwenye ngozi hadi kwenye ncha ya nywele kutokana na uwingi wa protini inayopatikana katika Samaki.
Karoti
Matumizi ya karoti kwa walio wengi hupenda kutumia kama kiugo katika vyakula na hasa mboga.Ni vyema kutumia karoti kwa wingi kwani zina vitamin A na hivyo zitazifanya nywele zako kuwa imara pamoja na kuiacha ngozi yako kuwa yenye kuvutia  na kuondoa ukavu wa ngozi.
Unapotumia karoti inasaidia kuzuia kuungua ngozi wakati unapoweka dawa kichwani, kuepusha michubuko katika ngozi, na pia huzuia kuwepo kwa mba kichwani. Hivyo basi kama unasumbuliwa na mba, ni vyema ukatumia karoti ili kuepukana na tatizo hilo.
Unashauriwa kujua aina yako ya nywele iliuweze kuchagua dawa iliyo sahihi kwa nywele zako hii itakusaidia kuepuka nywele kukatika,kuwa kavu,kuwa nyepesi na kukosa mvuto pia ni muhimu kumtafuta mshauri wa anayejua masawala ya nywele ili uwe na uhakika unapo tumia vupodozi vya nywele.

MWISHO…………

Vitu vya Msingi kwenye mkoba wa mwanamke

By On December 15, 2012
Vitu vya msingi  kwa mwanamke katika  Mkoba(Hand bag )wako.
Naomba leo tukumbushane mambo matano ambayo yanaweza kuwa msaada kwetu.Wanawake tunamambo mengi na wakati mwingine tunaweza kushau mambo ya msingi kutokana na kutokuwa na mpangilio mzuri,
Hivyo basi ilikuondokana na tabia hii ni vema leo katika safu yetu ya Urembo na mitindo tukumbushane mambo hayo matano:
Pochi
Ni muhimu kuwa na pochi ndani ya mkoba wako ambayo itakuwa na pesa,kadi ya benki,vitambulisho na vitu vingine ambavyo unaweza uka weka katika pochi yako.Hii itakusaidia kujua vitu kama hivyo vipo sehemu gani katika pochi yako  kuliko kufungua mkoba mzima na kuanza kutafuta.
Simu
Nafahamu kuwa ni vigumu kutembea bila simu hivyo basi chagua sehemu maalumu ambayo utakuwa unaiweka simu yako  hasa katika mifuko ya ndani ya Mkoba , ilikuhakikisha  kuwa usahau sehemu ulio weka na kuondoa usumbufu wa kukagua begi zima simu itakapoita au wakati ukihitaji kuitumia.
Funguo
Tusisahau funguo maana utakapoteza itakufanya uzunguke siku nzima kutafuta hasa sehemu ulizo pita katika mizunguko yako na  huu msururu wa magari  barabarani utakufanya uchanganyikiwe zaidi.
Kipochi kidogo
Ni  vema ukiwa na kipochi kidogo  kwa ajili ya kuwekea vitu kama rangi za midomo(lipstics),wanja,poda,mafuta,vitana,ilikuzuia mpangilio mbaya wa vitu ndani ya mkoba wako pia kuzuia kuchafua mkoba endapo vikimwagika .
Daftari(Notebook) na kalaamu
Litakusaidia kujua vitu unavyohitaji kununua na pia utaweza kuorodhesha vitu ulivyo nunua,kwa wale wenye tabia ya kusahau vitu  alivyopangilia kuvifanya mahali anapo kwenda  na hukumbuka wakati amekwisha rudi nyumbani nadhani daftari ni la msingi sana kwao.

Kanga
Mwanamke  lazima utembee na kanga au kitenge mda wote kiwe ndani ya mkoba wako ili usihadhirike unapopatwa na tatizo.Hapa inategemea unaelekea wapi? Usije ukabeba kanga au kitenge wakati unakwenda kwenye sherehe.Unapokuwa na safari ndefu ni muhimu kubeba kanga.Kama haitakusaidia wewe itamsaidia mtu mwingine.
Viatu (Flatshoose)
Hasa wanaopenda  kuvaa viatu virefu na hata wengine kwa ajili ya tahadhari pale kiatu kinapokuwa kimekatika kitakusaidia kulinda unadhifu wako na kuepusha aibu.Nimetaja vitu vichache lakini kuna vile vingine ambavyo ni muhimu kwa mwanamke hasa ukishajua nyakati zako,nimekuwa nikishuhudia wanawake wengi wakipatwa na aibu kutokana na hilo tuwe makini.
0756377940.

UVAAJI WA SKAFU

By On December 15, 2012

Jifunze aina mbalimbali za kuvaa Skafu

HABARI za wikiend mpenzi msomaji wa safu hii mpya ya urembo na mitindo ya mavazi inayokujia kila siku ya Jumatatu.
 Katika safu hii utaweza kufahamu na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu urembo na mitindo ya mavazi kwa wanaume na wanawake, na hivyo kukufanya msomaji kwenda na wakati na kuonekana wa kisasa zaidi.
 Katika makala hii ya mwanzo kupitia safu hii nitajikita katika kuzungumzia juu ya uvaaji wa skafu pamoja na kukujuza mavazi yanaoendana na skafu.
Kwa kuanza kabisa napenda utambue kuwa skafu ni kitambaa kinachovaliwa shingoni kama urembo, unaweza kuvalia na aina yoyote ya nguo kwa kuzingatia muktadha na vazi unalovalia.
Kuna aina mbalimbali za skafu kutokana na aina ya kitambaa pia ukubwa na muundo wa skafu, mfano kuna skafu ndefu, fupi na nyingine zamraba.

Katika Miji mbalimbali yenye hali ya baridi, imekuwa kawaida sana kuwaona vijana na watu wengi, wanawake na wanaume wakiwa wamevaa skafu kwani ni moja ya vazi linalomfanya mtu aonekane nadhifu na kupendeza zaidi.

Kuna njia tofauti za kufunga skafu, na hii mara nyingi hutokana na aina ya nguo mtu aliyovaa pamoja na sehemu anayokwenda.

Unaweza funga skafu kwa kulinganisha pembe zilingane na pia unaweza kufunga katika nusu ya urefu, kisha kuiweka kwenye shingo yako ili mwisho moja iwe ndefu nyingine iwe fupi kufanya fundo huru katika pande zote.

Zile skafu ambazo zipo mraba unaweza kuikunja kwanza kama pembetatu kisha kuiweka shingoni huku ukiifungia nyuma ya shingo na ukaonekana nadhifu.
Skafu huvaliwa na wanaume na wanawake, ingawa mara nyingi wanawake ndiyo wenye uwanja mpana sana wa kuvaa skafu. Skafu uweza kuvaliwa na nguo yeyote pia husaidia kuongeza mvuto wa vazi ulilovaa.
Sehemu za baridi mara nyingi utaona watu wakiwa wamevaa skafu ilikujikinga na baridi na kipindi cha baridi ni vyema ukitumia skafu nzito na ufungaji wake lazima uwe ule wa kuzungusha shingoni kama duara.
Licha ya skafu kuvaliwa shingoni, pia inaweza kutumika kama kibanio cha nywele na wengine wanazitumia kama mkanda, na pia unaweza kuifunga skafu yako pembeni ya mkoba wako ikiwa ujapenda kuivaa shingoni lakini hapa ni zile skafu fupi ambazo siyo ndefu ndiyo unaweza kuzifunga pembeni ya mkoba wako.
Unashauriwa ukivaa skafu usivae mkufu kwasababu hauwezi kuonekana na pia, ni vyema kuvaa skafu nzito kipindi cha baridi na wakati wa jioni, mchana unashauriwa kuvaa skafu ambazo ni nyepesi kulingana na hali yahewa itakavyo kuwa.
Ukiwa umevaa vazi la Ofisini pendelea kuvaa skafu fupi kulingana na vazi ulilo vaa.
MWISHO…

Upambaji wa chumba

By On December 15, 2012
Upambaji wa Chumba
Chumba ni sehemu muhimu kuliko mahali popote katika nyumba.Tulio wengi huona sehemu hii kama mahali pa kupumzika pale tunapokuwa tumechoka na wakati wa kulala ndipo huwa tunakumbuka eneo hili.
Fahamu kuwa hamna sehemu iliyo na maana sana katika maisha yetu kama chumbani au sehemu ya kulala.
Sehemu hii inapaswa kuwa tulivu, safi na yenye vitu  vichache, Unapoweka vitu vichache ndani ya chumba chako utakifanya kiwe na  hewa nzuri nzuri zaidi.
Chumbani  ni mahali ambapo unaweza kupumzisha ubongo wako na kufikiria mikakati   ya kimaendeleo na ukaweza kupata wazo jipya lakini yote hayo utayapata endapo chumba chako kitakuwa kisafi, tulivu pamoja hewa nzuri.
Zifuatazo ni dondoo za upambaji wa chumba:
Mwanga
Chumba kinapopata  mwanga wakutosha huvutia zaidi  na kuwa na hewa ya kutosha.
Ninapo zungumzia mwanga nina maanisha mwanga kutoka dirishani, mwanga wa taa za chumbani ambazo uwekaji wake upo tafauti kulingana na uwezo ulio nao, kuna taa ambazo huwekwa chini, ukutani au zile ambazo huwa pembezoni mwa kitanda. Mwanga wa taa ya chumbani hupaswa kuwa hafifu.
Rangi.
Katika uchaguzi wa rangi ni pamoja na rangi ya ukuta wa chumba chako, mapazia, shuka, pamoja na rangi za mito. Hapa inategemea unapendelea rangi gani lakini unashauriwa rangi za chumbani ziwe rangi ambazo ni tulivu.
Sehemu ya joto utatakiwa kuweka mapazia ambayo sio mazito, katika hali ya baridi tumia mapazia mazito pia ni muhimu kuzingatia rangi, usipendelee rangi zitakazofanya chumba chako kuwa giza.
Pendelea mashuka yenye rangi moja au yenye maua machache. unapaswa kutumia rangi ambazo huonyesha usafi mfano rangi nyeupe.
Unaweza kuchanganya na rangi zingine katika mito yako ya kitandani.Ubunifu katika utandikaji wa kitanda chako ni muhimu ili kiweze kukuvutia muda wote.
Sakafu
Kuna watu wanaopenda kutumia Mazulia (carpets) chumbani. Jaribu  kuchagua rangi nzuri aidha inayoendana na ukuta wako wa chumbani, ilikuleta muonekano mzuri pia unashauriwa kapeti lisiingie chini ya kitanda ili kukupa  urahisi wakati wa kufanya usafi.
Ni muhimu kusafisha zulia lako ili kuondoa vumbi na kuepuka kupata mafua. Pia ni vema kuwa na tabia ya kulitoa maramoja moja ili kuweza kusafisha sakafu yako na kuondoa harufu ya unyevunyevu  uliopo chini ya zulia.
Mwisho zingatia kuweka vitu vichache chumbani na kuwa na mpangilio mzuri wa vitu ndani ya chumba chako.

Namna ya kuosha unyayo

By On December 15, 2012
Jinsi ya kusafisha Unyayo

Si kitu cha ajabu katika saluni zetu kuwakuta wanawake wakisafishwa kucha  na kupakwa rangi ili kuvutia miguu yao.Usafishaji na utunzaji wa miili yetu ni jukumu letu kufanya hivyo ili kuendelea kuvutia zaidi.

Leo katika safu hii ya urembo napenda nizungumzie suala hili la usafishaji wa unyayo.Wapo wanawake au wanaume ambao miguu yao huchanika, kuwa na fangasi au kuwa  na funza kutokana  na mazingira tunayoishi na jinsi tunavyotunza nyayo zetu, wengi wetu tunajisahau katika jukumu hili la kusafisha nyayo zetu.

Zifuatazo ni njia za utunzaji wa Unyayo

Jitahidi kila siku kuosha unyayo wako kwa maji ya uvuguvugu na  sabuni, kabla hujaanza kusafisha unyayo wako weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika 5 kisha anza kusafisha kwa sabuni.

Changanya maji yako na asali, ambayo husaidia kulainisha ngozi ya Unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika Unyayo.

Ukimaliza kuosha Unyayo wako, hakikisha unajikausha na kitambaa kikavu kuanzia katika vidole vyako. Usipo kausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu vya kudumbukiza.Watu walio chanika miguu wanashauriwa kutumia viatu vya wazi kwa muda mrefu huku ukizingatia taaratibu za usafishaji wa nyayo, pia unaweza kutumia cream za kulainisha Unyayo wako ambazo hupatikana katika maduka ya vipodozi.

Pendelea kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika Unyayo wako(baby Oil) au paka Grisalini(glyceline) kwenye unyayo kisha vaa soksi wakati wa kulala, Soksi husadia kulainisha Unyayo wako kutokana na hali ya joto  inayokuwepo ndani ya soksi.

Ongeza kiwango cha kunywa maji, kila siku jitahidi kunywa angalau lita moja ya maji  ambayo husadia  ngozi yako kuendelea kuwa  nyororo.

Umuhimu wa tikiti maji kwa wanaume

By On December 15, 2012

Umuhimu wa Tikitimaji(Watermelon) kwa wanaume

Nitumaini langu kuwa tunda hili sio geni masikioni kwa wengi,Hivyo basi
naomba leo niweze kuwa elezea umuhimu wa tunda hili kwa ambao hawafahamu na inawezekana wengine wanalitumia bila kujua faida ya tunda hili kiafya. Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, 'Potassium', 'Magnesium' na virutubisho vinginekibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha
hisia za kimwili na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (ErectileDysfunction).

Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta
mhemuko wa mwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za
kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya
damu na kuufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa rahisi bila athari
yoyote mbaya.

Upungufu wa nguvu za kiume au Ugumba.
Tikitimaji lina kirutubisho aina ya'arginine', ambacho huchochea uzalishaji wa 'nitric oxide' kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa yaViagra.

Utafiti uliofanyika  kwa wanaume 50 waliokuwa na matatizo ya nguvu za kiume,
ulionesha kuwa wanaume hao waliweza kufanya tendo la ndoa baada ya
kupewa vidonge lishe (food supplement) venye kirutubisho aina ya'arginine'.

Misuli
Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya 'Potassium' kama vile
Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo.
Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali,
huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
Husaidia kupunguza uzito wa mwili.
Tikitimaji ni tunda lenye  kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango
kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili
linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo
kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia
na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima na bila kuathirika kiafya.

Huimarisha kinga ya mwili.
Kirutubisho cha 'arginine' kilichomo kwenye Tikitimaji kina kazi nyingi
mwilini, mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea
kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Kama unavyojua, kinga
ya mwili ndiyo msingi wa afya bora, kwani ukiwa na kinga imara huwezi
kusumbuliwa na maradhi hata siku moja.

Huondoa sumu mwilini
'Arginine' vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji madonda na kuondoa
'ammonia' na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu
kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.

Faida zingine
Faida za Tikitimaji kiafya ni nyingi, tunda hili hufaa kuliwa na
wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza
nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo
yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa
ya tumbo.

Kumbuka
Matunda kama haya hupaswa kuliwa mara kwa mara na wakati ungali mzima
ili kuupa kinga mwili wako ilikujikinga na maradhi wenyewe, usisubiri
mpaka upatwe na maradhi hayo na kwa kuambiwa na daktari ndiyo uanze
kula, kumbuka siku zote kinga ni bora kuliko tiba!

Siri ya Mwanamke Mrembo

By On December 15, 2012


 Anne Kansiime. Kansiime Kubiryaba Anne (amezaliwa 13 April 1987) anajulikana kwa jina la umaarufu Anne Kansiime ni msanii wa vichekesho kutoka uganda watu hupenda kumwita malikia wa afrika katika vichekesho.Ni mwanamke ninaye mkubali katika tasnia ya usanii na huwa anapenda kuwa kiafrica rangi ya ngozi yake ni kivutio tosha kama mwanamke wa kiafrika.


Kuna msemo usemao kuwa “mwanamke ni pambo la nyumba”hivyo basi kama mwanamke ni pambo la nyumba ndani hata n’je pia  unastahili kuwa nadhifu.Leo katika safu hii ya urembo na mitindo nitazungumzia vitu vichache ambavyo vitakusaidia wewe mwanamke bila kujali kipato chako cha uchumi.

Kujiamini na kujikubali 

 wanawake wengi hushindwa kuvaa baadhi ya mavazi kutokana na maumbile yao,Huona  kuwa miili  yao haiwezi kupendeza katika  mavazi mengine.Mfano wapo watu ambao hushindwa kuvaa nguo fupi kutokana na kuona kuwa miguu yao ni mibaya.Unapaswa kuujua mwili wako  na  mavazi ambayo yanakupendeza na kukuonyesha nadhifu,kwa watu wanene ni vema kuvaa nguo ambazo nipana nikiwa na maana kuwa zisichore mwili wako na kutengeneza muonekano mbaya.Wale wembamba wao wana uhuru katika mavazi isipokuwa usipo jitambua utaonekana kituko uchaguzi wa vazi utakalo kuwa umevaa.

Tambua rangi ya nguo zinazokupendeza,

chagua rangi inayoendana na ngozi yako ambayo itakuonyesha vema,kuna baadhi ya rangi ukivaa zitakufifisha  na kukufanya uonekane ujapendeza hata kama vazi lako ni zuri na la thamani.

Panga bajeti  

kwaajili ya kununua vitu vyako vya msingi ni kimaanisha mavazi,heleni.bangili,mkufu,Hapa mwanamke unashauriwa kununua gauni jeusi,katika manunuzi yako, gauni jeusi fupi au refu,hili litakusaidia unapokuwa na mtoko au sherehe utaweza kutupia gauni lako na kuchanganya na heleni bangili au mikufu na utaweza kuvaa kwenye  mtukio tofauti na kuoneka mpya huku uikiwa umeficha umasikini.

Fanya mazoezi 

wanawake wengi hatuna kasumba ya kufanya mazoezi siku zote.Maozezi ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha viungo vyetu na kutengeneza muonekano wa mwili(body shape).Hii itakusaidia kuepuka matumizi ya dawa zakuongeza maumbile mfano dawa za kuongeza nyonga(hips) na makalio.

 Tumia Maji na Matunda 

ni muhimu kunywa maji angalau lita moja kwa siku kiafya,itakusaidia kuimnarisha ngozi yako,pia jitahidi kupata matunda katika mlo wako au unaweza kutumia matunda kama kifungua kinywa chako na kuepuka utumiaji wa vitafunwa vyenye mafuta.


Epuka utumiaji wa madawa ya kongeza maumbile,
kubadilisha ngozi nikiwa na maana ya vipodozi vya kuchubua mfano Carolight.Hivyo ni baadhi vitu vichache ambavyo ukizingatia mwanamke utaendelea kuonekana kijana na kuepuka uzee usio wa lazima naomba mchunguze watu wengi wamepata madhara baada ya kutumia dawa hizi.Utazifurahia kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa. 

Jinsi ya kuvaa Stoking

By On December 15, 2012

 (Stoking)

 

Stokingi ni vazi ambalo limeshika kasi sana siku hizi, watu wengine uliita vazi hili soksi chupi au soksi ndefu kutokana na muundo wake ulivyo,Vazi hili huvaliwa na rika zote,wengi hupendelea kuvaa kwasababu huwasaidia kustili miili yao huku wengine wakilitumia kujizuia baridi.Katika safu yetu hii ya urembo na mitindo

nitakupatia dondoo chache za vazi hili na namna linavyostahili kuvaliwa:

Chagua rangi sahihi ya stokingi yako:

Watu wengi hawako Makini  katika  rangi za nguo, unatakiwa kujua  mpangilio wa rangi za nguo utakazo vaa (combination of color) ilikukupa muonekano mzuri.

Siku hizi mtindo huo wa kuchanganya rangi wameupa jina la kachumbari,mambo ya kuoanisha(match) kiatu na nguo,mkanda labda na rangi ya nguo au mkoba,

yamepitwa na wakati kwa sasa lakini ni vema kupangilia vizuri mavazi yako ili uweze kuvutia zaidi.Uvaaji wa  stokingi huongeza kitu kipya katika vazi lako kama ni

gauni au sketi ya jinsi au kitambaa.Kitu cha msingi ni kujua rangi ya stokingi utakayovaa pamoja na hilo gauni au sketi yako.Wakati mwingine ukikosea kuvaa vazi hili

 kwa kufanya chaguo ambalo si sahihi utaonekana kituko mbele za watu.

 

Unapokuwa umevaa stokingi kwa ajili ya kuelekea kwenye sherehe,harusi au kwenye mtoko na mpenzi wako au rafiki lazima utahitaji kuonekana bomba zaidi.

Hivyo basi ni vema ukitambua rangi sahihi za kuvalia siku hiyo.Nikiwa na maana kuwa  stokingi nyekundu,bluu,kijani,au njano na rangi zinginezo,rangi hizo ni vigumu

sana katika kutaka kuoanisha (match) na gauni au sketi na ikiwa utavaa  stokingi za rangi hizo unaweza kuonekana kituko katika ulimwengu huu wa mitindo.Gauni

 nyeusi au nyeupe rangi hizo za stokingi lazima zitaendana na gauni lako,rangi nyeusi na nyeupe ni rahisi kuoana(match) na rangi zingine.Hakikisha umejitazama katika

 kioo kabla ya kutoka n'je kwasababu rangi zingine za stokingi hazipendezi kuvalia magauni yenye rangi.Pendelea stokingi nyeusi zaidi ambazo ni rahisi kuvalia na

gauni au sketi rangi tofauti.

 

Stokingi za wavu(fish net stocking)

Hizi ni stokingi za kipekee,stokingi zenye muundo wa wavu ni vema kuzivaa na gauni nyeusi ambayo kwa asilimia kubwa inaonyesha
miguu yako kutokana na kwamba stokingi nyingi ni nyeusi,pia unaweza kuvaa na gauni nyeusi ,nyeupe,hudhurungi au kahawia hata gauni la njano.Wakati mwingine
stokingi za wavu unaweza kuvaa unapokwenda disko kutokana na jinsi muundo wake ulivyo.Hakikisha huvai aina hii ya stokingi na gauni au sketi fupi sana kulingana na utamaduni wetu kwasababu stokingi hizi huonyesha ngozi yako.

stokingi nzito

Hizi ni zile stokingi ambazo sio nyepesi na si rahisi kuonyesha ngozi ya mtu aliyevaa,Wengi hupendelea kuvaa stokingi hizi ili kuficha miguu yao wengine huvaa kipindi
cha baridi ilikupata joto, pia unaweza kuvaa  na viatu virefu au viatu vya kudumbukiza.Kama huelewei ni rangi gani? ya stokingi ina kufaa basi pendelea kuvaa stokingi zenye rangi ya ngozi yako.
Watu wengine uvaaji wa stokingi ni sehemu ya maisha yao, haiwezi kupita wiki bila kutupia stokingi kwa ndani hivyo basi kama wewe ni mpenzi wa vazi hili
jaribu kuchagua rangi sahihi itakayo endana na vazi lako ili kukupa mwonekano mzuri zaidi katika vazi utakalo kuwa umevalia.Ukivaa stokingi na viatu vya wazi  lazima utaonekana kituko.

abnerytupokigwe@gmail.com





NJIA YA KUONDOA CHUNUSI NA MABAKA USONI

By On December 15, 2012
 Njia ya kuondoa Chunusi na mabaka usoni
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao hujitokeza kama vivimbe/vipele vidogo vidogo hasa sehemu za uso,kifuani na hata mgongoni.Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani Bacteria.
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa . Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe Karibu asilimia 85 ya  vijana kati ya umri wa miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na  zaidi ya  asilimia 20 ya wanawake  wenye umri wa zaidi ya miaka  ishirini hupata chunusi wakati mwingine hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
Vipele vinaweza kuwa vidogo  au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.Ngozi mpya hutengenezwa kirahisi tu  mahali palipokuwa na chunusi hali hii husababisha mlingano usiosahihi wa  ngozi na hutoa kidonda ambacho baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega na mgongoni.
Chanzo cha Chunusi
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
Umri
Kama nilivyosema( hormone)vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia umri wa kubalehe.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa  nta (sebum) katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
Vipodozi
Baadhi ya vipodozi vya usoni(Make-up) za kina dada na Marashi(spray) za nywele zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
Chakula
Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufanya chunusi kuwa nyingi zaidi.Hasa vyakula vyenye mafuta.
Dawa
Chunusi zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,Steroid ni dawa zenye homoni zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia tofauti na makusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
Magonjwa
Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana
Mazingira
Chunusi huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye  mafuta,grisi au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza uwezekano wa kupata chunusi.
Jinsia
Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
Familia
Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia  wa familia kadhaa kuliko nyingine.
Homoni
Mabadiliko ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
Usafi wa mwili
Kutumia sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au vipele  husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho mwilini au kutooga huongeza uwezekano wa kupata chunusi
Mawazo(Stress)
Mtu anapokuwa na mawazo mengi vikemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huweza kuchangia au kusababisha chunusi
Dalili za Chunusi
Vipele au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama baka dogo.
Ikumbukwe kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana Daktari kuzigundua,japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda kumwona daktari  au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya chunusi.Pale vinapotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya  zaidi.Hata hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu, chakula,ngozi,dawa unazotumia na vitu vingine vinavyoweza.kuchangia mtu kupata chunusi
Matibabu
Matibabu ya chunusi yanajumuisha  kupunguza utoaji wa (sebamu ),kuondoa seli za ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.Matibabu huweza kutofautiana kutokana na wingi au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama nilivyokwishakueleza katika makala iliyopita.
Dawa za kupaka
Kuna dawa za kupaka ambazo hupakwa katika eneo la ngozi lililoathirika kwa chunusi.Dawa hizi hupatikana kama cream,losheni,jel .Dawa hizi hutumika kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele vidogo vidogo tu.
Dawa nyingine ni zile zinazolainisha nta  na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku hasa baada ya kusafisha kwa maji safi  na sabuni ya kawaida na kukausha kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
.
Matibabu mbadala
Haya hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu na kuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu wenye chunusi wanashauriwa  kula mlo kamili wenye vyakula vyenye madini ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B. Ni vema kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.
Mambo ya kuzingatia ili usipate Chunusi
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
·      Osha taratibu sehemu unayodhani ina chunusi  kwa maji safi na sabuni angalau mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au kitu chochote kigumu.
·      Tumia  Vipodozi au vilainisha ngozi visivyo na mafuta  ya mgando
·       Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
·      Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
·      Usibinye au kutoboa  vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
·      Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
·      Punguza mawazo

Kumbuka kuwa chunusi haziwezi kutibika kabisa   iwapo matibabu yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona  na unapokuwa unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika ngozi.

Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa kwa nija ya kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kukusaidia.Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni.Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamoja na krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju,lakini nadhani asali na ukwaju kama utaenda sokoni ni rahisi kupata.Pia ni vema ukitumia losheni yenye mchanganyiko wa asali au ukwaju.




Jumpsuit(bwelasuit)na uvaaji wake

By On December 15, 2012


  JUMPSUIT(Bwelasuti) na uvaaji wake


Mpenzi msomaji wa safu hii ya urembo na mitindo ya mavazi leo nataka kuwajuza historia ya vazi hili ambalo kwa sasa limekuwa likivaliwa sana katika mandhari mbalimbali.

Bwela suti au ovaroli(Jumpsuit) mwaka 1960 ni vazi ambalo zamani lilitumika sana na watu wanaoruka na parachuti kwa lengo la kuzuia hali ya baridi na upepo.

Mwaka 1987 vazi hili lilipata umaarufu katika sekta mbalimbali ambapo lilianza kuvaliwa na Marubani,madereva,wanamichezo,Mafundi bomba,mafundi mitambo,Wasanii  pia huvaa jukwaani, huku vyuoni/mashuleni  likivaliwa kama sale katika vyuo vya ufundi.

Wazazi wengi huwavalisha bwelasuti watoto  wanaotambaa kwa lengo la kuzuia baridi pia kuhofia  kuchafuka kwa wale walio katika kipindi cha kutambaa.

Vazi hili limeendelea kushika nafasi kubwa katika swala la mitindo huku wabunifu wengi  wakibuni vazi hili katika mitindo mbalimbali.
Jinsi ya kuvaa bwela suti

1.Tambua kiuno chako
Hakikisha unajua kipimo cha kiuno chako wakati wa kuchagua bwelasuti iliyo sahihi.Lazima rastiki au mkanda  uliopo katika bwela suti ushike vema kiuno chako ili kuepusha muonekano mbaya wa umbile lako .

2.Fanya chaguo sahihi la bwela suti kulingana na umbo lako
Nivema kutambua umbo lako ili kuweza kuonekana nadhifu ndani ya vazi hili.Kwanza kabisa kwa wale wenye miguu mrefu ni vema kuvaa bwela suti ambazo ni pana miguuni,watu wafupi au wenye urefu wa wastani hutakiwa kuangalia aina ya kitambaa na urefu wa vazi hili.

Wenye maziwa madogo,mikono miyembamba lakini wamejariwa nyonga(hips) unatakiwa kuvaa bwela suti yenye muonekano wa blauzi zaidi pia iweze kuonyesha  mikono yako vizuri.hii itazuia muonekano wa nyonga zako zaidi.

3.Vaa bwela suti na koti
Watu wengi huofia kuvaa bwela suti kutoka na mitindo mbalimbali ya vazi hili kuonyesha mabega,mgongo na sehemu kubwa ya mikono.Kama wewe ni mmoja wapo jaribu kuvaa vazi hili na koti,utaonekana nadhifu pia litakuzuia baridi na kuficha mikono yako  ni vema koti liwe fupi ili kuonyesha umbo lako na mtindo wa bwela suti uliyoivaa..

4.Uchaguzi wa rangi za bwela suti
Bwela suti yenye rangi moja huvutia zaidi kuliko bwela suti yenye rangi moja juu na chini rangi nyingine au yenye mchanganyiko wa rangi mbalimbali chini,Katika uchaguzi wa rangi wengi hutofautiana kulingana na chaguo la mvaaji.

5.Uchaguzi wa kiatu cha kuvalia bwela suti
Unaweza kuvaa viatu vya chini(Flat shoes) au viatu virefu na bado ukaonekana  mwanamke nadhifu na mwenye kuvutia zaidi bila kujali umri ulionao wala umbo lako.

Vazi hili  huweza kuvaliwa nyakati zote na katika matukio tofauti, kitu cha msingi mvaaji aangalie mtindo wa bwela suti ,aina ya kitambaa na eneo analokwenda na tukio(sherehe).

Tuesday, January 31, 2012

Mazingira Yetu

By On January 31, 2012
SEHEMU TULIVU


Mwana-adamu kwa kawaida ameumbwa naa mambo mengi lakini kitu ambacho mpka leo hiii hakuna alie na jibu ni kwamba ni nini hasa hutokea akilini pale uonapo au utizamapo mandhari yanayovutia? Ghafla unajikuta akili yako inabadilika na mawazo kupungua uonapo kitu ambacho ni kizuriii na kinakuvutia hasa mazingira.

Maisha na Mazingira

By On January 31, 2012
UTULIVU



Wakati mwingine akili huhitaji sehemu tulivuuu ili ipumzike japo kimawazo kulingana na siku yako ilivyokuwa na mambo uliyokutana nayo toka ulipoamka mpaka jua kuzama. Jipe amani nafsini mwako

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu