Enter your keyword

Culture for Life.

Wednesday, April 26, 2017

2017#Miaka 53 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Vazi la taifa ni lipi mpaka sasa?

By On April 26, 2017

Miaka 53 ya muungano Kauli mbiu ni  tuulinde na kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na kuwajibika na kufanya kazi kwa bidii.

Stara Thomas, mwimbaji wa zouk akiwa amevalia vazi murua kabisa!
Picha: hisani ya haki-hakingowi blog.

Katika kuadhimisha miaka 53 ya uhuru ni vema pia tukikumbuka kutafuta vazi ambalo linatutambulisha kama watanzania kama mataifa mengine yanavyojitambulisha kupitia maleba hata wanayovaa katika kazi zao za sanaa.Nimejaribu kuonesha baadhi ya picha ambazo watu wanajaribu kuonesha asili yao kwa kuvaa nguo zenye rangi ya bendera ya Taifa ili kuonesha uzalendo.

Msanii wa mashairi ya kughani akionesha uzalendo kwa kuvaa cheni ya kichwani yenye rangi za bendera ya Taifa.


Msanii Diamond akiwa na wasanii wengine ambao waliungana kutengeneza wimbo wa muungano,Lakini nia yangu  katika picha hii nikuonesha ambavyo wasanii hawa wanashauku ya kuwa na vazi la taifa na wanapokosa basi wanatumia vitambaa kuonesha uzalendo lakini bado haitoshi,nadhani serikali inatakiwa kuangalia pia suala la vazi la taifa kwani mpaka sasa ni suala Mtambuka.


 

 
Maoni yangu ni kwamba suala la kila mwananchi kujiamulia vazi la kuvaa sisahihi hata kama tunatofautiana kimazingira,basi vazi hilo liangaliewe katika hali ya rangi au kitambaa ambacho kila mwananchi anaweza shina nguo na kuvaa pahala popote.

 Historia ya Muungano

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (inayojumuisha Visiwa vya Pemba na Unguja). Tanganyika ilikuwa ni mwendelezo wakoloni la Ujerumani, utawala wa Waingereza kwa Mamlaka ya Umoja wa Mataifa, Himaya ya Umoja wa Mataifa chini ya utawala wa Uingereza na mwisho Taifa huru kuanzia mwaka 1961 ndani ya nchi za Jumuiya ya Madola.

Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ziliingia mkataba wa Muungano mnamo mwaka 1964 na kuanzishwa Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mkataba huu wa Muungano ulitiwa saini na aliyekuwa Rais wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume tarehe 22 Aprili 1964 huko Zanzibar. Mkataba huo ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi hapo tarehe 26 Aprili, 1964 na mnamo tarehe 27 Aprili, 1964, viongozi wa nchi zote mbili walikutana katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar esSalaam na kubadilishana Hati za Muungano. Sheria za Muungano zilitoa tamko la Jamhuri ya Muungano katika Ibara ya 4 kwamba:

“Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zitalazimika, baada ya kuungana na siku zote baada ya kuungana, kuunganishwa kuwa Dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar’ (Ibara ya 4 Sheria za Muungano)”
Jina hili la “Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar” lilibadilishwa baadae mnamo tarehe 28 Oktoba, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Sheria ya Jamhuri ya Muungano, Sheria namba 61 ya mwaka 1964.

Tuesday, April 25, 2017

Sunday, April 23, 2017

Mavazi unayopaswa kuvaa mwanaume kwaajili ya Interview

By On April 23, 2017

Epuka kuvaa suti nyeusi,

ukweli ni kwamba suti nyeusi haipitwi na wakati lakini ni vema wakati wa usahili ukivaa suti ya kijivu(solid navy) au gray,ikiwa unafanya interview ya utangazaji unaweza vaa suti nyeusi.Hakikisha uvai  vizuri zaidi kuliko mfanya usahili,ni nivema muonekano wako ujieleze zaidi kuliko mavazi
 yako.


Epuka kuvaa suti zenye vifungo viwili mbele

Kwa usahili wa kwanza ukivaa shati nyeupe si mbaya.Usivae shati la bluu hilo linafaa kwa kipindi cha kufanya biashara si interview,Epuka shati lenye kora zenye urembo au zenye umbo la duara,vaa shati lenye kora ya kawaida.


mwanaume hupaswi kukosa tai katika kabati lako hii ni muhimu na tai hukupa muonekano mzuri zaidi.

 

Wednesday, April 19, 2017

Vitu 8 vinavyopelekea kuchukia ukuta wa nyumba yako.

By On April 19, 2017

1.Kuogopa rangi ziletazo giza

 wakati mwingine katika kuchagua rangi ya nyumba mtu anachagua rangi zinazong'aa  ilikuifanya nyumba iwe na rangi yenye kung'aa wakati kuna rangi zingine nzuri ambazo hukufanya kuwa katika hali ya utulivu.Unaweza ing'arisha kwa mapa

2.Uwekaji wa picha ukutani.

Ndiyo picha huleta mvuto katika nyumba haijalishi zipo katika muonekano gani lakini unapoziweka pamoja bila kuzingatia rangi zake,rangi za frame au ukubwa wa frame na kuziweka sehemu moja lazima zitakuboa,Weka kwa kuzingatia rangi zinazofanana kama unaziweka pamoja au angalia ukubwa wa frame zako na shauri utumie picha za kiutamaduni au za kisanaa zaidi kwa picha pia humsaidia mtu kupumzisha akili yake hasa anapoziangalia

3.Kwa ajili ya kuwa na nyumba yenye nafasi

 Hali hii hupelekea nyumba yako kuoneka katika muonekano mbaya mfano hata uwekaji wa picha kuweka kwa wima ili kukwepa kubana nafasi wakati ukiweka picha hiyo kwa wima ingeonekana vema,Unapofanya hivyo nyumba lazima ikuboe.

Kupitia hayo mambo matatu niliyoyatajanaamini utajifunza kitu kidogo na kurekebisha muonekano wa nyumba yako.

 

 

 


Tuesday, April 18, 2017

Emelia Brobbey reveals her new look, and you will love it!!!

By On April 18, 2017
Emelia Brobbey has said goodbye to big weaves and long hair, at least for a moment and she is looking stunning!



 She took photos revealing her low cut hair and already, fans are loving it!
The actress  is currently preparing to premiere her self-produced movie ‘Adanfo Bone’ in three cities – Kumasi, Accra and Sunyani. The movie features Nana Ama McBrown, Liwin, Bill Asamoah, Akrobeto, Bishop Bernard Nyarko and many others



source:Ameyawdebrah.com

Keke Palmer amewashangaza watu aliponekana na begi la mfuko wa shangazi kaja mtaani

By On April 18, 2017
Keke Palmer  Mwigizaji,mwimbaji,mwandishi wa nyimbo na mtangazaji  kutoka nchini marekani  amekuwa gumzo katika mitandao na ulimwengu kwa ujumla baada ya kuonekana na begi la shangazi kaja ambalo linafahamika zaidi kama Ghana bag.pata muonekano wake:Angalizo tu,sidhani kama hii style wabongo mnaweza iga?

African print headwrap

By On April 18, 2017
Pata muonekano wangu wa kichwani kwa kutumia kipande kidogo cha kitenge ambacho kilibaki katika nguo yangu niliyoshona,Wakati mwingine huwa tunashona nguo lakini vile vipande vinavyobaki tuna tupa nakuahikikishia hivyo hayo mabaki ya vitambaa unavyotupa unaweza kutengenezea vitu vingi kama pillow,nguo ya mtoto wako,tablemate,zuria la mlangoni,hereni,cheni,au mkufu wa kitenge lakini wengi tumekuwa tuki dharau na kutupa.

Hiki ni kipande cha kitambaa kilichobaki kwenye kitenge changu nikaona vema nikijitupia katika casual wear yangu na huu ndiyo muonekano wangu:

PIC CREDIT:Me production wapo Arusha  jengo la nmvua plaza karibu na stand kubwa.


Nikijiangalia najipenda zaidi,nimejifunza kwamba siku zote jikubali na jipende zaidi haijalishi unaishi vipi lakini katika suala la kujipenda lipo juu yako,usisubiri mtu aje akupende zaidi ili kukupa muonekano mzuri.

ZIJUE Njia 18 ZA KUFUNGA TAI .

By On April 18, 2017



18 ways to tie a necktie for men
Huenda ulikuwa unapata tabu katika ufungaji wa tai,tumia hiyo picha kuweza kufunga tai na kila siku uwe na muonekano mpya.

Viatu vya kiofisi ambavyo mwanaume unatakiwa kuwa navyo.

By On April 18, 2017
Kila mwanaume huitaji viatu haijalishi anavivaa wapi lakini nimuhimu mwanaume kuwa na viatu ambavyo vitakupa muonekano mzuri unapovaa na nguo zako.Leo nitaonesha baadhi ya viatu ambavyo unapaswa mwanume kuwa navyo kwaajili kazini au mazingira ya kistaraabu mikutanoni,kwenye semina,kwenye sherehe za heshima.Leo nitakuonyesha baadhi ya viatu ambavyo wewe kama mwanaume ni muhimu kuwa navyo:


1. Patent Leather Shoes  ni viatu vyenye muonekano mzuri wa kung'aa,wakati mwingine waweza vaa na jeans lakini hakikisha suruali yako inakipa kiatu uhuru wa kuonekana.


 2.Chukka Boots  ni viatu ambavyo asili yake nikutoka jeshini vilikuwa vikivaliwa sana jeshini kwasababu ya muonekano wake kama buti.Vipo vingine vyenye muundo wa leza na viatu viatu ambavyo unaweza vaa na nguo ya kiofisi na ukapendeza

 

3.The Double Strap Monks  viatu hivi ni kwa mwanaume yeyote aliyenadhifu na msafi.

 


4.Full Strap Loafers,Kaitu hiki ni kwa wanaume wote wanaojijali kama huna fanya kununua

 

5.Wholecut ni vaitu vinavyofahamika na wanaume wengi na huvaliwa sana na mavazi ya  kiofisi.

 

6.Plain Toe Blucher  Viatu hivi unaweza kuvalia suti,koti,au wakati mwingine kwa ajili ya casual wear au mtoko wa kawaida unaweza vaa na suruali ya khaki.

 

 

 

 

Monday, April 17, 2017

Badili muonekano wa nywele zako

By On April 17, 2017
Angalia walivyopendeza na mitindo ya nywele ambayo inafaa maeneo mbalimbali ofisini hata katika matembezi mbalimbali.
 


Kwa wanaopenda mitindo ya nywele fupi

Ni vizuri kwenda na wakati japo usiwe mtumwa wa mitindo au fashion mpya zinazokukja kila uchao.


Nywele ni moja ya mambo yanayomfanya mwanamke kuonekana wa kisasa na wa kuvutia.


 


Unapochagua mtindo wa nywele uwe makini, kuna mambo ya kuzingatia  kwa uchache tu kuna la kuzingatia kazi uifanyayo, umri, wadhifa katika jamii, sura na umbile lako, rangi ya ngozi, maeneo unayokwenda.

Sunday, April 16, 2017

vitu 10 vya kufanya katika mahusiano yako.

By On April 16, 2017

Ni kweli kuwa kuna wakati kama mwanadamu tunachoka hata katika shughuli za kawaida huwa zinamchosha mtu hata chakula ukila kila siku chenye ladha moja unachoka vivyo hivyo katika mahusiano kama hamna ubunifu baina ya wenza hawa lazima ufikia hatua ya kuchokana na kupelekea wenza kuaachana,Leo mpenzi msomaji wa safu hii  nitakupa dondoo chache ambazo zitakusaidia kujenga mahusiano yako.

1.Hakikisha mnatazama au kusikiliza mziki kwa pamoja.

 

 

Mnaweza kutumia Tv kuangalia vipindi mnavyopenda wote au kusikiliza mziki mkiwa pamoja hii itaongeza chachu ya mapenzi vilevile kwa wale wapenzi wa filamu mnapotazama kwa pamoja hasa love story mtajifunza vitu vingi nakuona udhaifu wa kila mmoja na kujirekebisha.

 2.Pangeni mambo yenu pamoja,

Mnaweza kupanga vitu kwajili ya maisha yenu ikiambatana na maendeleo yenu,au kutoka out,trip,dinner na vitu kibao ambavyo mnaweza kuplani pamoja.Hii italeta chachu ya mapenzi zaidi kati yenu.

 3.Pangeni kupumzika katika hoteli iliyo n'je na mji wenu.

Msanii wa muziki Diamond na mke wake Zari.

 4.kufanya mazoezi pamoja.

 5.Hakikisha mambo uliyokuwa ukimfanyia kipindi cha uchumba huachi kuyafanya kwani ndiyo yalimvutia zaidi,unapoyaacha yanapunguza mapenzi.

 

6.Kuwa mbunifu kila siku mfanyie jambo jipya mwenzi wako.

 

7.Mambo yalimvutia mpenzi wako ulipo yafanya usiache kufanya penda kuyarudia zaidi ili kumfurahisha zaidi.

 

8.Mnunulie zawadi mwenzi wako.

9.Katika suala la mapenzi ondoa aibu na mpe kile mwenzi wako anapenda ila zingatia afya yako

.

10.Ogopa kuwashirikisha watu wa n'je madhaifu ya mwenzi wako zaidi zungumza na mwenzio,tafuta njia nzuri ya kuweza kuongea naye.

 

Friday, April 14, 2017

Pregnancy Fashion Tips To Look Stylish Wherever You Go!

By On April 14, 2017

1.Vaa koti ambalo utalifunguo vifungo

2.Chagua nguo ambayo haionyeshi ukubwa wa tumbo lako sana na ikupe muonekano mzuri. 

Blogger Shamimu Mwasha kushoto pic ya kwanza alipokuwa  mjamzito na mwanamitindo Kiki katika vazi ambalo hata mjamzito anaweza kulishona na akapendeza.

3.Tafuta cheni au hereni,bangili ambazo zitakupa muonekano mzuri kulingana na vazi lako.Hii husaidia kumfanya mtu kushangaa urembo uliotupia zaidi .

 4.Vaa kama mtoko ya kawaida(casual wear)

 

 


 5.Waweza vaa shati na suruali isiyo bana tumbo lako kama kuna baridi vaa na skafu


6.Vaa nguo zenye mistari mikubwa ili kuficha muonekano wa tumbo.

7.Bwela suti(jumpsuit)Unaweza ivaa wakati wowote itakufanya uonekano katika mtindo murua na wakupendeza.


Masai wedding dress the best Tanzanian style ever.

By On April 14, 2017

Bibi harusi kulia akiwa na msimamizi wake katika mazingira ya umasain,Hili ndilo kabila linalodumisha utamaduni wake Tanzania ,kabila hili lina utajiri wa vitu vya asili ambavyo binafsi huwa vinanivutia sana kwani vinapobuniwa vema basi huwa na thamani kuwa hata katika kununua.

PIC CREDIT: ME PRODUCTION-ARUSHA

PIC CREDIT: ME PRODUCTION-ARUSHA

 Bibi harusi wa kabila la kimasai vazi lake lazima lijae nakshi za shanga kwa wingi pamoja na cheni ya kimasai hiyo ndefu pamoja na hizo zinazo onekana shingoni kwake ni muhimu sana kwa binti wa kimasai,ambazo huita enkarewa.

 Vazi la bibi harusi wa kimasai si chini ya T.SH 500,000/=Napenda watanzania wote tungekuwa na mwamko wa kuvaa mavazi yetu ya asili hata kama huna basi waweza vazi la kitamaduni lilipo katika kabila lako.

 

PIC CREDIT: ME PRODUCTION-ARUSHA

ME PRODUCTION-ARUSHA 

Wapo  Jijini Arusha karibu na jengo la Namvua Plaza Ghorofa ya Kwanza karibu na Stand kubwa ya mabasi ya mikoani.

Wanapiga picha katika location tofauti pia katika sherehe mbalimbali kama harusi,birthday,sendoff,cocktail part...na matukio yoyote pamoja na video shooting wana bei poa fanya nao kazi ufurahie kumbukumbu ya tukio lako.

Watafute kwa mawasiliano haya:

meproduction22gmail.com

Mobile no.+255 752026643

                  +255 763782044

 


3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu