Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, September 22, 2020

FASIHI ANDISHI-KWA KIDATO CHA TATU NA NNE.

Mwalimu wa Kiswahili

1.Fasihi hubeba yote anayoibusha binadamu katika maisha yake ya kila siku.Jadili kauli hii kwa mifano- Maudhui (Dhamira)

2.Fasihi hubeba yote anayoibusha binadamu katika maisha yake ya kila siku.Jadili kauli hii kwa mifano- Maudhui (Dhamira)

3.Jadili vipengele viwili vya fani na vitatu vya maudhui vilivyojadiliwa katika riwaya uliyosoma.(Fani na maudhui)

4.Ujumbe wa Tamthiliya ya Kilio chetu na Orodha una umuhimu mkubwa katika Tanzania ya leo.Jadili kauli hii kwa kutumia vitabu hivyo vilivyotajwa.Maudhui (Ujumbe)

5.Taswira ni kipengele muhimu sana kwani huipamba lugha ya ushairi na kufikisha ujumbe kwa hadhira .Onesha ukweli wa kauli hii kwa kutumia vitabu viwili ya ushairi ulivyosoma kati ya vilivyosoma kati ya vilivyoorodheshwa hapo juu. Fani ( Taswira ilivyoibua ujumbe)

6.Jadili kufaulu na kutofaulu kifani kwa waandishi wa vitabu viwili vya riwaya ulivyosoma.(Fani kwa ujumla kufaulu na kutofaulu)

7.Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma chagua wahusika watatu kwa kila kitabu na uoneshe jinsi wahusika wanavyopaswa kulaumiwa na jamii.Wahusika (dhamira au ujumbe mbaya/wasifu mbaya)

8.Kwa kutumia diwani mbili ulizosoma, eleza jinsi taswira tatu kutoka katika kila diwani zilivyotumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe kwa jamii.Fani (Taswira zilivyoibua ujumbe)

9“Waandishi wa kazi za fasihi huibua migogoro mbalimbali na kupendekeza suluhisho ili kuelimisha jamii husika”. Thibitisha kauli hiyo kwa kutoa hoja tatu kwa kila kitabu kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.Maudhui(Migogoro ilivyoibua ujumbe)

10.Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, fafanua madhara yanayotokana na kukosekana kwa elimu ya jinsia kwa vijana kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila kitabu.Maudhui (Madhara ya usefu wa elimu ya kijinsia)

11.Jadili namna jina la kitabu la mwandishi wa tamthilia uliyosoma linavyoweza kubeba wazo kuu la mwandishi wa kazi ya fasihi.(Swali linaweza kulenga riwaya,mashairi na tamthiliya) Fani (Fafanua ujumbe uliopo katika jina la kitabu)

12.Jadili matumizi ya jazanda yalivyojitokeza katika tamthiliya uliyosoma.(swali hili linaweza lulenga  riwaya na mashairi/diwani) Fani ( Taswira)

13.Kwa kutumia riwaya uliyosoma, fafanua jinsi mwandishi alivyoweza kuwatumia wahusika wawili katika kuibua maudhui yake.Fani (Wahusika na maudhui( ujumbe,dhamira,migogoro)

14.Tumia Riwaya ulizosoma kisha toa hoja tano (5) zinazo thibitisha kuwa wanaume ni kikwazo cha mafaniko katika jamii. Maudhui( nafasi mbaya ya mwanaume)

15.“Kazi za fasihi hufichua mivutano/mitafaruku  iliyopo katika jamii” kwa kutumia hoja sita (6) kutoka diwani mbili ulizosoma darasani .Fafanua mivutano hiyo hoja tatu kutoka katika kila diwani.Maudhui (migogoro)

16.“Kipenda roho hula nyama mbichi”.Fafanua msemo huu kutoka riwaya ya Takadini na riwaya ya Watoto wa Mama n’tilie. Kwa kutumia hoja sita(6) Maudhui (Mambo hasi yaliyotokea kwa wahusika kutokana na matendo yao)

17.Waandishi wengi wa tamthiliya wanajitahidi kuonesha ufundi wao kwa kutumia tamathali za semi mbalimbali katika kazi zao.Thibitisha ukweli wa kauli hiyo kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma darasani.Hoja (3) kutoka katika kila tamthiliya.Fani (Tamathali za semi)

18.Waandishi wa kazi za fasihi andishi  huandika kazi zao kulingana na jina la Kitabu jinsi lilivyo.Kwa kutumia  hoja tatu kutoka kila tamthiliya onesha namna jina la kitabu linavyoendana/kusadifu mawazo ya mwandishi.Fani (Fafanua ujumbe uliopo katika jina la kitabu)

19. Kwa kutumia riwaya mbili ulizosoma fafanua namna ambavyo waandishi wametumia kipengele cha mtindo kuumba kazi zao.Toa  hoja tatu kwa kila kitabu.Fani (Mtindo)

20.Kazi za fasihi andishi zinafananishwa na kisu kikali katika jamii zetu” Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa vitabu viwili ulivyosoma.Maudhui (Ujumbe)

21.“Mshairi siku zote hukemea uonevu katika jamii”Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila diwani kati ya diwani mbili ulizosoma.Maudhui (dhamira)

22.“Fasihi ni chuo cha kufundisha maisha kwa jamii husika” Jadili ukweli wa kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya mbili ulizosoma.Maudhui (Ujumbe)

23.Kwa kutumia hoja tatu kwa kila tamthiliya mbili ulizosoma,jadili kufaulu kwa waandishi katika kipengele cha utumizi wa tamathali za semi.Fani (Kufaulu kwa matumizi ya tamathali za semi)

24.Msanii ni kinda la jamii husika,hivyo anayoyaandika ni kuhusu jamii hiyo. Jadili kauli hii kwa kutumia hoja tatu(3) kutoka katika kila diwani moja kati ya diwani mbili ulizosoma.Maudhui (Dhamira)

25.Jadili wahusika wawili kama kielelezo halisi cha kukubalika au kutokukubalika kwao katika jamii kati ya Takadini,Mamantilie na Brown Kwacha kutoka katika riwaya mnili ulizosoma. Fani (Wahusika)

26.Dhana ya mapenzi imejadiliwa  kwa mapana .Thibitisha kauli hii kwa kutumia tamthiliya kati ya ulizosoma. Maudhui (Mapenzi ya dhati na yasiyo ya dhati)
Kujikomboa ni kwa namna nyingi katika maisha ya mwanadamu.Thibitisha kauli hii kwa mifano kutoka katika riwaya mbili ulizosoma.Toa hoja tatu kwa kila kitabu.Maudhui (ukombozi)

27.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu