Una mpenzi au mchumba mnapendana sana Je umewahi kujiuliza haya maswali Kabla hujaingia kwenye ndoa?
SARA ISSA AKIWA NA MUME WAKE.
Swali #1:Ni kiasi gani cha fedha tunacho na ambacho tunaweza
kutumia kwa mwaka mzima au kila mwezi.
Swali# 2:Nani anahusika na matumizi ya nyumbani pamoja na
gharama za mipango ya nyumba yetu.
Swali# 3:Ni kiasi gani cha fedha tunaingiza
pamoja,kwasasa,ndani ya mwaka mmoja,miaka 10 na nani anahusika kuingiza kiasi
kikubwa zaidi katika malengo yetu.
Swali#4:Malengo yetu ya mwaka mzima katika mapato
tunayoingiza ni yapi? tutatumia jitihada zipi kufanikisha.
Swali #5:Je? gharama za matumizi yetu katika
(Kodi,Bima,mavazi,chakula na usafiri)yapoje na tunatumia shilingi ngapi kwa
mwezi au mwaka mzima.Tumepanga kutumia vipi?
Swali#6:Je?Mda gani ambao kila mmoja wetu atautumia kazini
au tumepanga kuanza kazi mapema sana au kazi zetu ni za jioni tu.
Swali#7:Je kama mmoja wetu hataki au hawezi kufanya kazi
katika mazingira yoyote yale itakuwaje? au tutafanya nini?
Swali#8:Je mwenzangu anapenda nini na je ninafurahia
anachokipenda mwenzangu.
Swali#9:Nipo huru ninapokutana na mwenzangu katika tendo la
ndoa,na je nalifurahia.
Swali#10:Je tunafanana katika makubaliano yetu ya kukutana
kimwili,tunawezaje kumudu haja zetu kama hazifanani,kidogo au sana labda mwenzangu anahitaji usiku
tu,mchana,kwa wiki mara moja au kila siku au kwa mwezi au mwaka..
Swali#11:Je tunakula chakula pamoja na ni nani anahusika na
gharama za chakula,nani anapika na kusafisha baada ya kula.
Swali#12:Je wote tuna tabia zinazofanana,mfano kunywa
pombe,kuvuta sigara kula sana nk
.
Swali#13:Je familia za wenzetu zinaishije,tutakuwa tunafanya
matembezi ya kuwatembelea au kuwa ruhusu kutumbelea na kwa kipindi gani?
Swali#14:Tutakapopata watoto je ni mahusiano gani
tutayaruhusu kati yao na bibi au babu kama wapo,je ni mda gani tutawaruhusu
kukaa nao.
Swali#15:Je? tutapata watoto na tunahitaji watoto wangapi na
umuhimu wao kwetu ni upi?
Swali#16:Je tutakapopata watoto maisha yetu yatabadilika au
tutaacha kazi au kupunguza kazi au tutatafuta mtu kwaajili ya malezi.
Swali#17:Je marafiki tulionao wanatosha au itakiwa tupunguze
au kuongeza na faida yake ni ipi?
Swali#18:Je dini zetu ni sawa kama si sawa je mahusiano yetu
yanaweza kudumu ikiwa dini zetu ni tofauti.
Swali#19:Je kila mtu ana mda wa kufanya ibada peke yake na
je kila mmoja anaelewa hali ya mwenzake.
Mpenzi msomaji hayo ni maswali baadhi ambayo unapaswa
kujiuliza hata kama hukuwahi jiuliza embu jitafakari kwanza huenda kama
ukiyatazama kwa sasa yakawa na faida siku za usoni katika ndoa yako.
No comments:
Post a Comment