Enter your keyword

Sinyati Blog

Culture for Life.

Monday, October 9, 2017

Party dress#2017

By On October 09, 2017
Muonekano  Wa  gauni  la  party  kutoka  kwa  muigizaji  Wa  Kike Iniedo  kutoka  nigeria-Afrika

Wednesday, September 27, 2017

Jinsi kijana unavyoweza kuchangamkia fursa katika sanaa #mimi na sanaa

By On September 27, 2017
Gerald Soka ni kijana  aliyemaliza shahada ya utalii katika chuo kikuu cha Dodoma Tanzania.Mbali na shahada hiyo Gerald anasema alikuwa anapenda sana kuchora na alishawahi kuwa mshindi katika uchoraji kipindi cha UMITASHUNTA mwaka 1999.Anasema baada ya kumaliza chuo alipata nafasi ya kutembelea Uganda na rafiki yake.

Saa ya ukutani

Gerald Anasema alipofika Uganda ndipo aliona fursa ya uchoraji kuwa ni sanaa itakayomlipa.Anasema aliona kuwa vitu ambavyo jamii inaona kama uchafu lakini yeye anatumia kujiingizia kipato hasa anapo tumia katika sanaa yake.


Flame za picha

Gerald anatumia.magunia,majani ya migomba na maboksi au makaratasi na vitenge kutengenezea vitu kama.
Saa ya ukutani zenye picha iliyochorwa,flame za picha,keyholder,tablemats, menu file,tissue boksi,boksi La zawadi,lampholder,flower vessel na tissue box.

Flower vessels

Tissues boksi


Lampholdets


 FAIDA
kijana Gerald Anasema kupitia sanaa hii ya uchoraji anamsomesha mtoto,anapata mshitaji ya familia,na kuweza kulipia gharama za malazi.mbali na hayo Gerald Anasema kwa mwezi huweza kuingiza kiasi cha milioni moja endapo anatapata oda nyingi na laki nne endapo biashara haipo vizuri.Pia nimefanya kazi na kampuni kama,Africafe,Eng'noto,Triple A,nk.

CHANGAMOTO
Kwanza ni uhaba wa masoko,mtaji was kutosha,hali ya hewa hasa kipindi cha mvua migomba huwa hadimu(majani makavu).

USHAURI KWA VIJANA
Waache kubweteka,wasiwe wavivu katika kutafuta kipato wafanye kazi kwa bidii pia wajitunze.
Ukihitaji kazi za Gerald wasiliana naye kwa namba.0757746506
 email:Gerald soka@gmail.com

Sunday, September 24, 2017

How to style kitenge with strip Attire.

By On September 24, 2017
Ukiwa na kitambaa cha mistari(strips) unaweza tafuta kitenge chenye maduara au maua ya karibu na kuyakata mtindo wa duara au umbo utakalo hitaji ,kisha bandika mwenye nguo yako.Hakika utapata muonekano wa tofauti sana na ukiwa kiasili pia.

Tuesday, September 19, 2017

Gauni La kitenge kwa muonekano wa kanisani na sherehe#2017

By On September 19, 2017
 Endapo utashona kwaajili ya kanisani hakikisha inakuwa ndefu kidogo kwani kanisani ni mahali patakatifu na panahitajibkuheahimiwa pia.
 Mishono kama hii utakapoitumia kama kuwa nguo ya kutokea namaanisha Street wear utakuwa hujaitendea haki.
Muonekano wa suti za kike #2017

By On September 19, 2017
 Suti yenye kifungo kimoja,mtindo wa suruali kama unavyouona haijafika mwenye ankle.
 Muonekano huu pia ni mzuri.kwa MTU ambaye hana tumbo kubwa.
 Muonekano huu umekuwa ukiwa vutia wadada wengi .ni vema pia unapoushona hakikisha unamguu wa kuvalia isije onekana suti kama imetundikwa.Sunday, September 17, 2017

Urembo wa asili shingoni.#"mimi na Sanaa kwanza"

By On September 17, 2017
Wanawake kwanza nawapa pongezi kwa jitihada zenu katika karne hii,wanawake wengi wameweza kuwa wabunifu has a kwa kutumia rasilimali zinazotunguka.
Leo nitazungumza namna ya kuwezakuvaa  hizi shanga shingoni,IPO mitindo mbalimbali .

shanga zilizounganishwa na kitenge.

Unaweza kuvaa shanga hii hasa katika vazi lla mtaani,mwenye sherehe (watu wengi hutumia shanga hizi kwenye harusi maranyingi)Tukiendelea hivi utamaduni wetu utaimalika na kuwavutia wengi.

Vikapu vya asili huweza kuwa mbadala wa Mifuko ya Rambo.

By On September 17, 2017
Mifuko ya rambo imekatzwa kutumika nchini kenya.sasa unaweza kutumia vikapu vizuri kama hivi kwa ajili ya manunuzi ya vitu vyako sokoni.

Vikapu hivi hutengenezwa na wanawake nchini Tanzania,Pia huviuza kwa being ndogo ambayo mtanzania yeyote huweza kumiliki kikapu hiki.


Kwa mtu anaye hitaji nitafute kwa namba +255 756377940

Saturday, September 16, 2017

NATARAJIA KUINGIZA SOKONI KITABU CHANGU HIVI KARIBUNI KINACHOKWENDA KWA JINA "MAPENZI KABURINI"

By On September 16, 2017
 

 

Ningependa ujue kipaji hiki kimeanzia wapi?

Huwa napenda  kujibembeleza au kujifariji nikiwa natembea kwa kutengeneza hadithi katika fikra zangu ili kuweza kufika ninakoelekea bila kuchoka au ninapotaka kulala,Vilevile kipindi nikiwa shuleni nilikuwa napenda sana kutengeneza hadithi na kuweza kuziigiza wakati wa mahafali na wanafunzi wenzangu ingawa wakati mwingine wenzangu walinicheka na kuniona ninakihelehele lakini sikukata tamaa.Hata nilipoendelea na elimu yangu ya chuo kikuu kipaji,hakikuishia hapo niliendelea kutunga hadithi na kuzihifadhi.

Siku moja baada ya kushiriki shindano la uandishi wa Riwaya fupi kwa wanafunzi wa shule ya msingi,sekondari na vyuo vikuu Tanzania kwa ajili ya Tuzo ya mama Salma Kikwete iliyoandaliwa na  TASAKI(Tamasha la Sauti ya Kiswahili) niliibuka mshindi wa pili wa riwaya fupi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania mwaka 2010.

Hivyo hiki kitabu ni muendelezo wa Riwaya niliyopatia Tuzo.Soma kitabu hiki uweze kujionea ubunifu wa hali ya juu wa fani pamoja na mshikamano wa maudhui uliyopo ndani ya kitabu hiki.

Mapenzi Kaburini ni kitabu chenye mtazamo yakinifu,ni kitabu ambacho maudhui yake yamezitazama nchi za Afrika  na changamoto zilizopo katika nchi kwa upande wa viongozi pamoja na wananchi.Kimebeba maudhui yanayowalenga wananchi wote bila kujali utabaka.Kwa upande wa fani kimetumia majina ya halisi na kubuni hasa kwa upande wa maeneo ya miji mfano kuna miji kama Kinyonga,kupe,chatu ambayo ni majina yaliyopo katika nchi ya Simba.Nchi hii ya Simba ni nchi inayosimamia nchi zilizopo Afrika Mashariki.

Mbali na hilo pia visa na matukio vimepewa majina ya hifadhi za Taifa zilizopo katika nchi ya Tanzania.Mfano hifadhi ya Ruaha,Sanane,Manyara na kitulo kama ukisoma kitabu hiki utagundua kuwa sifa ya hifadhi inaendana na visa na matukio yaliyopo katika sehemu hiyo iliyoandikwa kwa jina la hifadhi.Mfano hifadhi ya Kitulo inasifika kwa kuwa  na maua,kama tujuavyo maua huashiria sifa nyingi moja wapo hapo ni upendo,watu wengi hutumia maua katika kuwapa wapenzi wao,mfano kuomba msamaha,kumfariji mtu,hata kuonesha upendo kwa mtu unayempenda.

Utakaposoma kitabu  hiki  utaburudika na kufundishwa baadhi ya mambo kama Kukuza imani yako kwa Mungu,uaminifu katika ndoa,uzalendo katika nchi yako na Madhara ya kujihusisha katika mahusiano  na mtu usiye mjua.

Nitakupatia kionjo kidogo katika sura ya kwanza ili kuweza kuona mwanzo tu wa hadithi hii ambayo hutapenda kuacha kuifuatilia:

 

Sura ya kwanza 

 Hifadhi ya Sanane  

Ilikuwa siku ya Jumatatu katika ghorofa la tajiri mmoja, mmiliki wa hoteli maarufu katika nchi ya Simba. Tajiri huyo alifahamika  sana kwa kuwa alikuwa akijitolea sana kwa wananchi wasiojiweza, katika miji mbalimbali ya nchi hiyo.Watu husemamfadhili  punda kuliko mwanadamu vilevile  tenda wema kisha nenda zako baraka utazipata kwa Mungu,usisubiri hisani  za wanadamu.

 Pamoja na misaada aliyoitoa kwa watu mbalimbali lakini wananchi wa Simba hawakujali misaada yake, walimteta kila kona kuwa anatumia nguvu za giza na amekwisha toa kafara ndugu, jamaa na hata watoto wake ili kujipatia utajiri mkubwa alionao. Siku hiyo ya Jumatatu katika pagala  la tajiri huyo aliyefamika kwa jina la Pesa nyingi.

 katika moja ya chumba cha ghorofa hilo kulikuwa na mwanamke mrembo na mzuri sana wa sura, mrefu mithili ya twiga, mwenye umbo zuri la kiafrika, chini alikuwa amevaa suruali ya chupa huku akiwa amevaa blauzi tatu juu zenye rangi tofauti na nywele timutimu zikiwa zime nakishiwa na vitu vya jaani kama vichana,visude, rasta chakavu na kufungwa kitambaa cha kitenge aina ya makenzi ,uso wake ulikuwa kama paka mwenye madoa kutokana  na kujipamba kwa majivu na masizi ya mkaa wa jaani. Pembeni ya ua hilo alikuwepo mnyama mwenye maringo

mbugani kuliko wote, sio mwingine bali ni kijana mtanashati aliyekwenda hewaani, rangi ya ngozi yake   nyeusi ya kung’aa. Tabasamu la mwanaume huyo lililokuwa likimfariji mtoto mzuri, lili mvutia sana Savannah. Ghafla ilisikika sauti ya mwanamke huyo ikiita kwa sauti ya chini iliyojaaa simanzi na mateso ya muda mrefu,ilisema “John naumia mume wangu, hali yangu kila kukicha afadhali ya jana”. 

John alijibu  “usijali Savannah nipo hapa mke wangu kwa ajili yako utapona tu tutakwenda hospitali,subiri  nikuandalie chakula ule, kisha nikupeleke hospitali  malikia wangu”. Basi baada ya John kumfariji Savannah aliamka na kuelekea jikoni pembeni ya sehemu aliyokuwa amelala mpenzi wake. Watu hawa walipendana sana ni vile tu hali yao haikuwa nzuri kifedha waliishi kwa kuhangaika, kuomba msaada na wakati mwingine walifukuzwa na walimwengu pale walipokuwa wakiomba msaada, watu waliwapita kama mbwa waliokosa matunzo. 

Wapenzi hao Walizoea maisha ya kuokota vyakula jalalani na kukimbilia magari ya taka sambamba na kusubiria mabaki ya chakula katika migahawa mbalimbali. Wakati huo John alikuwa akitimiza ahadi aliyo mhahidi malikia wake alimuandalia chakula walicho kiokota katika soko kuu la mji huo wa Chatu. John alimuinua Savannah pale alipokuwa amelala kwenye kanga chakavu akiwa amejifunika magunia yalionekana ni ya mpunga. John alimlisha Savannah chakula kile ambacho hawakujua kilipikwa lini na kutupwa na nani na lini. Savannah alisikika akisema “asante mume wangu hata

mwanangu anafurahi sasa naona napata nafuu, nahisi ni njaa ilikuwa inaniuma”. Mwanangu nisamehe mama kakushindisha njaa, nakupenda sana najua wewe utakuwa mrembo zaidi yangu mwanangu hata baba yako anakupenda”. John alikuwa anapenda sana utani alicheka na kusema “atakuwa mrembo kama wewe kweli mke wangu lakini rangi ya ngozi yake itakuwa kama yangu, yako iko kama ya nguruwe hahahaaaa!” Savannah alikuwa mweupe kama Nguruwe, ingawa alivyokuwa anaonekana ni kama mtu mwenye  ngozi  ya rangi ya maji ya kunde kutokana na ugumu wa maisha. 

Wawili hao walifurahi pamoja na kusahau shida walizokuwa nazo.Walipomaliza kula wapenzi hao waliamua kutoka  nje baada ya kukaa ndani ya paghala hilo kwa muda wa wiki moja, Dikidiki hao walikuwa na kaida ya kufanya hivyo wanapotafuta riziki na kujilimbikizia ndani ya paghala lao kisha wana kaa kwa muda huo bila kutoka. Usilolijua ni  kama usiku wa kiza, basi Savannah na John walipotoka  wakiwa n’je ya mgahawa mmoja uliokuwa unapendwa sana na wananchi wa mji huo wa Chatu zilisikika sauti za wanawake wakisema: 

“haya  jamani sasa ni ule wakati wa Pesa nyingi kuingiza hela sasa wenzi wametoka fungate”. Waliamini kuwa Pesa nyingi alikuwa anawatumia Dikidiki hao  kama misukule inayotoka na kurudi ndani na wanapotoka basi  mzee Pesa nyingi huingiza hela nyingi sana. Kwakuwa wenzi hao walikuwa hawaelewi kinachoongelewa waliendelea kuomba msaada kwa wateja waliokuwepo hapo mgahawani. Wanapokosa waliamua kucheza baadhi ya nyimbo zilizokuwa

zikipigwa katika mgahawa huo, wakicheza hupewa chakula na fedha ambazo hutoka katika mifuko ya wateja. John alikuwa anapenda sana kucheza,wakiwa wamekaa chini walisikia wimbo wa mwanamuziki maarufu Tanzania Diamond unaosema Je, Utanipendaga? John alimuinua Savannah aliyeonekana kachoka na mimba yake. Savannah aliamka na kucheza na mpenzi wake ,walicheza kwa  miondoko ya kihindi, machozi yalisafisha uso wa Savannah huku yakiosha kifua cha John kilichokuwa kimejaa kama mlima na mikono iliyokuwa na miinuko ya kupanda na kushuka ilizunguka juu ya  kifua cha Savannah na kumfanya ahisi kazungukwa na jeshi kubwa la malaika wa ulinzi.

 Baada ya kumaliza kucheza savannah alikuwa amechoka sana, kitendo cha kucheza kilimsababishia kuchokoza maumivu na kupelekea kupata uchungu katika kizazi chake. Baada ya kuona hivyo John aliinama na kuchukua zawadi walizozipata kutoka kwa hadhira iliyokuwa ikiwatazama huku baadhi ya hadhira wakibubujikwa na machozi walimpelekea hela na chakula John katika kapu lake la kukusanyia riziki. Watu waliokuwa wakiwatazama Savannah na John hawakujali maumivu ya mwanamke yule na kuona kawaida. 

Wapo waliosikika wakisema hawa vichaa wana akili, wengine walisema hawa si vichaa, vichaa gani wana akili ya kutafuta hela hivi, wamekusanya umati mkubwa hivi na kuwafanya watu kutoa kile walichonacho. Mama mmoja mwenye busara anayeuza katika mgahawa huo aliyefahamika kwa jina la mama ndaga akasema“Jamani mimi nawafahamu hawa vichaa kwanza hawakuwa wakitembea hivi pamoja kama Dikidiki, huyo kaka unayemuona alikuwa..........pata mwendelezo kwa kujipatia kitabu hiki.

Nicheki kwa mawasiliano haya:+255756377940

                                    intagram:sinyatiblog

                                     facebook:Tupokigwe Abnery

 

Wednesday, September 6, 2017

Ubunifu wa kitenge 2017

By On September 06, 2017

Msanii Elizabeth Michael katika muonekano wa kitenge 2017

Muonekano huu wa kuongezea nakshi katika kitenge umekuwa kivutio hasa unapoweza kuchanganya urembo wa hiyo nashi katika kitenge chako,unaweza kuweka chini ya magoti,shingoni,katika kifua,hata mikononi.Vazi la kitenge ni vazi ambalo ubora wake kila siku unaongezeka,kinachotakiwa ni kuongeza ubunifu vazi hili ili kulipa uthamani wake,Huu ni mtindo mpya wa kitenge ambao umeonekana kuwavutia watu wengi hasa nakshi hii inapowekwa.

Tuesday, May 23, 2017

Beyonce Baby Shower #ASili ya Baby shower na namna ya kuifanya.

By On May 23, 2017
" Baby shower"Asili yake ni kwamba hufanya mwanamke mjamzito,mimba yake inatakiwa iwe na miezi sita(6) au nane(8) na kwautamaduni wa wenzetu kama Egpty ufanya hasa kwa mwanamke ambaye anatarajia kupata mtoto wa kwanza katika familia yake.Pia kipindi hiki mwanamke anatakiwa kula milo mizuri kwa ajili ya kujenga afya ya mtoto.

Ambapo mwanamke huyo huwaalika rafiki zake wa kike ambao humletea zawadi za mtoto,Hii pia humsaidia mwanamke kujiandaa kuwa mama mwema na kujua mavazi ya kumvisha mtoto pamoja na kumlea,Vilevile unaweza kufanya baby shower kwa mtoto ambaye anajinsia tofauti na yule wa kwanza.

Pia baba wa mtoto anaweza kufanya baby shower ambapo anaweza kuwaalika wanaume wenzake na wakampa zawadi za mtoto,anaweza kufanyia sherehe hizo pub au sehemu nyingine ambapo wanaweza kunywa,kuangalia mpira na kufanya mambo mengine ambayo wanaume wanaweza fanya wanapokuwa pamoja.

 Vilevile mwanamke huweza kuweka mchezo wakati wa kufungua zawadi ,hii pia husherehesha sherehe.
 Katika party aliyooita  "Carter Push Party’ and Twinning" pia wanawake maarufu walioweza kuhudhuria siku hiyo kama... star Serena Williams,La La Anthony,Kelly Rowland and Michelle Williams,
Sherehe zingine ambazo zinaweza kufanya ni pamoja na Diaper Shower,Grandma's Shower,Sprinkles shower.

Monday, May 22, 2017

Muoekano mzuri wa kwenda beach kiutamaduni zaidi

By On May 22, 2017
Kujivunia vitu vya asili ni muhimu kwa kila mwananchi bila kujali utaifa wako.Leo nitaongelea ubebaji wa mikoba ya asili wakati unapokwenda kupumzika ufukweni na familia yako,marafiki au mpenzi wako.Basi vitu vyako unaweza weka katika mikoba hii,pia hakikisha unavaa viatu flat kama ambavyo vinaonekana hapo.Sunday, May 14, 2017

Pleated skirt # Skirt za malinda zimerudi tena katika mitindo ya mavazi.

By On May 14, 2017
Malinda katika vazi la mwanamke yalionekana sana katika mavazi ya wanafunzi hasa mashuleni lakini miaka 1994 mavazi yenye mtindo huu wa malinda yalivaliwa sana na wamama(wakina mama wenye makamo)vilevile mavazi yenye malinda yalivaliwa sana na watoto wa kike,hasa katika magauni au skirt zao .


Sasa hivi hili vazi linavaliwa na kinadada zaidi,lakini hata msanii wa kike Emilia Clarke katika filamu ya Game of Throne ameonekana pia kavaa vazi hili la malinda .vazi linaonekana vema pale alipokwenda kuwafunga Dragoni wake baada ya kuua mtoto mmoja baada ya Emelia kuletewa mashitaka, aliamua kuwafunga hao Dragoni kwa minyororo .Basi katika onesho hilo utaona vema vazi hili la malinda katika gauni la mwanadada huyu mwenye umri wa miaka 31 sasa.


Emelia Clarke katika gauni lenye malinda,Amezaliwa 23/10/1986

Mitindo ya skirt za wanawake kwajili ya kanisani.

By On May 14, 2017
Wanawake tumeumbwa kuwa walezi katika ulimwengu huu,Hivyo hata vazi la mwanamke linapaswa kuwa la mfano katika nyumba ya ibada,Mwanamke unapokwenda kanisani hakikisha unavaa vazi ambalo halioneshi mwili wako.Mwanamke katika kanisa ni muombolezaji katika kuombea kanisa.


3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu