Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, May 8, 2015

MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI.



Diamond msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, amekuwa ni daraja kubwa kwa taifa na n'je ya nchi yake hasa katika kuitangaza lugha yake kwa nyimbo zake ambazo zinapendwa. kutangaza Lugha ya Kiswahili



HAKIMILIKI

Mimi Tupokigwe Abnery ,ninatamka kwamba tasnifu  hii ni kazi yangu asilia ,na kwamba haijawahi kuandikwa na wala kuwasilishwa katka chuo kuu chochote kwa ajili ya kutunukiwa digrii inayofanana na hii au nyingine yoyote.
Sahihi :T.Abnery
simu:+255756377940.
Anuani ya barua pepe:abnerytupokigwe@gmail.com
Mwalimu wa somo la Kiswahili.
Shule ya Sekondari Precious Blood-Arusha-Tanazania.

SHUKURANI
Tasnifu hii ni zao la wengi waliyojitoa kwa hali na mali kuikamilisha.Hakika ni singeweza kukamilisha kazi hii peke yangu na kuifanya kama ilivyo .Katika ukurasa huu nitawataja wachache na kuwaomba msamaha wale ambao sijawataja ila kwa dhamiri ya upendo toka moyoni nawathamini na kuwaenzi kwa umoja na ushirikiano wenu wa hali na mali.
Kwanza ,namshukuru mungu kwa kunipa uzima na afya njema katika kipindi chote cha mchakato wa maandalizi ya Tasnifu hii .Pili nawashukuru wasimamizi wangu Bw.Athumani Ponera na Bw. Jacob wa chuo kikuu cha Dodoma  kwa kujitoa katika kazi nzima kwa ushauri na kutupa muongozo jinsi ya kuifanya kazi hii.Kiwango cha upendo na muongozo walichokionyesha hakiwezi kupimika wala kulipwa .Hakika mchango wao hautasaulika kamwe.
Tatu,naushukuru uongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma kwa kunidahili kwa ajili ya masomo ya shahada ya kwanza katika  Isimu ya Kiswahili.Hata hivyo napenda kutoa shukrani zangu za pekee ziwafikie wazazi wangu kwa kunisaidia kwa hali na mali katika kufanikisha gralama za uandishi wa tasnifu hii.Pia napenda kuwa shukuru  wasanii  wa muziki wa kizazi kipya Danny   Msimamo,James christoper a.k.a Jc na  Abulazizi Aboubakar Chende a.k.a Dogo janja na wanafunzi  wa mwaka wa pili na watatu wa shahada ya isimu ya Kiswahili kwa mchango wao mkubwa waliouonyesha katika kufanikisha utafiti huu.
Nne,shukrani zangu za dhati zimfikie mkuu wa idara ya kiswahili wangu  Bw. A.Ponera  kwa kunipa hamasa ya kusoma kozi hii ya utafiti,Tano shukrani zangu za dhati ziwafikie watafiti wenzangu wa taaluma ya Isimu ya Kiswahili pamoja na jamii ya watu wa Dodoma waliochangia mawazo  yao na kuifanya kazi hii ikamilike ,hawa si wengine  bali ni Nibwene paighty,Mapunda suma,kihombo Vicky ,Kweka Shamimu na bakirane Vallelian.

  IKISIRI.

Tasnifu hii inayoitwa “NAFASI YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI”ina malengo mahususi manne,ambayo ni Kubainisha hadhi ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya,kubainisha sababiu zinazo pelekea muziki huu kusikilizwa na vijana,kuelezea mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa jumla.Taarifa zilikusanywa kwa njia ya mahojiano,majadiliano katika vikundi,mapitio ya maandiko na sampuli niliigawa katika makundi yafuatayo:Wasomi wanao sikiliza muziki wa kizazi kipya na wanafunzi wanaosoma Isimu ya Kiswahili.Sampuli ilipatikana kwa nbinu ya sampuli lengwa.Uchambuzi ulifanyika kwa mbinu ya ufafanuzi(uhalisia)

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya ni muziki ambao unabadilika kadri miaka inavyozidi kwenda na hivyo kutokana na hili inaonyesha kuwa endapo jitihada za taasisi ya utamduni na lugha isipo angalia swala la utumizi wa lugha katika muziki wa kizazi kipya hapo baadaye muziki huu utapelekea vijana kuwa na lugha yao na hivyo kusababisha utabaka katika jamii kwasababu utafiti unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya ni muziki wa vijana na lugha inayotumka wanailewa wenyewe kwa asilimia kubwa hivyo basi  kutokana na mwingiliano wa wasanii katika shoo,nyimbo zinazosikilizwa na jamii kuna uwezekano wa kuibuka kwa lugha ya kisheng inayotumiwa na vijana wengi  nchini Kenya na sasa inasikika katika muziki huu wa kizazi kipya na kuididimiza  lugha ya Kiswahili.Kwasababu lugha  ya kisheng  ni mchanganyiko wa lugha ya  Kiswahili ,kingereza na lugha za kibantu na utafiti unaonyesha kuwa wasanii wa muziki huu wana mtindo wa kuchanganya lugha tofauti katika mashairi yao.



YALIYOMO.
HAKIMILIKI
SHUKRANI
IKISIRI
YALIYOMO
SURA YA KWANZA…………… ………..…………………1-11
1.1Ufafanuzi wa dhana  maalumu zilizotumika katika Tasnifu hii
1.2Usuli wa Tatizo. 
1.3 Tamko la Tatizo la utafiti.
1.4 Malengo ya utafiti.
1.5 Malengo la jumla.
1.6 Malengo mahususi.
1.7.Maswali ya utafiti.
1.8 Manufaa ya utafiti.
SURA YA PILI. ………………………………………………12-13
2.0.Mapitio ya maandiko.
2.1 Maandiko yanayohusu  muziki wa kizazi kipya kwa ujumla.
2.2 Pengo linalo paswa kuzibwa.
SURA YA TATU………………………………………………14-16
3.0 Mbinu ya utafiti.
3.1 Mpango wa utafiti.
3.2 Eneo la  utafiti.
3.3 Mbinu za kupata Data.
3.4 Mbinu za kukusanya data
3.4.1Mahojiano.
3.4.2 Majadiliano katika vikundi.
3.4.3 Mapitio ya maandiko.
3.4.4 Vifaa vya utafiti.
3.4.5 Mbinu za uchanganuzi data.
3.4.6 Mawanda ya Utafiti.
3.4.7 Mpango wa Tasnifu.

SURA YA NNE………………………………………….17-36
4.0 Mjadala wa utafiti.
4.1Utangulizi.
4.2Hadhi ya muziki wa kizazi kipya katika lugha ya Kiswahili.
4.3Sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana.
4.4Mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni  wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
SURA YA TANO…………………………………………37-41
5.0 Hitimisho la utafiti.
5.1 Muhtasari wa utafiti huu.
5.2Mchango mpya wa utafiti huu
5.3 Maoni ya ujumla kuhusu utafiti.
5.4 Mapendekezo kuhusu tafiti zijazo.

MAREJELEO……………………………………………….42-46
Nyongeza mbalimbali.
A,Picha za wasanii wa  muziki wa kizazi kipya wakiwa katika matamasha pamoja na picha za vijana wakifuatilia tamasha.
B.Maswali ya dodoso
SURA YA KWANZA.
1.1 Ufafanuzi wa istilahi maalumu zilizotumika  katika Tasnifu hii:
1.1.1 LUGHA.
kwa mujibu wa Kiswahili sanifu TUKI(2005,Lugha (1)ni mpangilio wa sauti  na maneno unaoleta  maana  ambayo hutumiwa na watu wa taifa au kundi Fulani kwa ajili ya kuwasiliana.(2) ni maneno na mtumizi yake(3) ni mtindo anao utumia mtu kujieleza.

Kwa mujibu J.Habwe na P.Karanja,misingi ya sarufi ya Kiswahili(2004),lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wajamii wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.

 Hivyo basi lugha ni mfumo wa sauti nasibu na ishara za kisarufi ambazo kwazo watu wa jamii  Fulani ya lugha huwasiliana na kupokezana  utamaduni wao.Hii ina maana kwamba  lugha ni chombo muhimu cha utamaduni ,lugha ni sehemu ya utamaduni na ni chombo kinachosheheni sifa za utamaduni wa jamii husika katika misamiati,miundo na matumizi ya lugha zinazo husika.Lugha utumika  kukuza utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

1.1.2 MUZIKI.
Kwa mujibu kamusi ya English-Kiswahili toleo la 3(2005),muziki ni sanaa iliyokusudiwa na kuweza kukubaliwa na jamii, msanii hana budi kubuni mitindo ya lugha mbalimbali katika utungaji wake.
 Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu  Toleo la 3(2006),Muziki ni kitendo cha kutunga  na kutia sauti.
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu  toleo la pili (2004),Muziki ni mpangilio wa sauti za ala,uumbaji au vyote viwili.
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981), Muziki ni mpangilio  wa  sauti za ala na uimbaji unaoleta athari  fulani  kwa kiumbe.


1.2 Suala la muziki wa kizazi kipya.
Sehemu hii ina lengo la kuchunguza suala hili kihistoria,kwa kufanya hivyo tunaweza kupata  au kujua nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya  katika kukuza lugha ya Kiswahili ,katika kushughulikia suala hili ,nilichunguza hali halisi ya kuwepo kwa muziki wa kizazi kipya nchini baada ya vijana kuanza kuimba nyimbo hizi zenye mahadhi  ya kihiphop kutoka Marekani  na kutaka kujua  muziki huu una mchango gani katika lugha yetu  ya Kiswahili  kutoka mwaka 1970 ulipoanza kusikilizwa na jamii.Hii ni kwasababu jamii ndiyo  inayosikiliza ujumbe uliopo katika nyimbo hizo .Ambapo muziki huu hapo mwanzo ulikuwa ukionekana ni wakihuni  na ni wavijana pekee yao na sio wazee ,hii imekwenda sambamba na matumizi ya msamiati wa lugha ya Kiswahili inayotumika katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya .
Hivyo nimeona kuwa uchunguzi wangu uzingatie jamii inayosikiliza muziki huu wa kizazi kipya ,katika sehemu hii nimegawa makundi maalumu ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya ambao naamini kuwa suala la nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya linaweza kudhirirka kwa uwazi zaidi.Pamoja na kudhihirika huko  katika makundi haya nyimbo nyingi za muziki wa kizazi kipya(bongo flava) zilikuwa zikisikilizwa tangu mwaka 1970 hadi sasa.
1.3Historia fupi ya muziki wa kizazi kipya
  ulianzishwa na Wamerekani weusi huko the Bronx, New York Marekani mnamo mwaka 1970.Wamerekani wenye asili ya Afrika ,ambao babu zao walichukuliwa kwenda Marekani kama watumwa.Elementi hizi za utamaduni wa hiphop zilikuwa zikijitokeza kwa awamu moja  na inapofifia inaibuka nyingine ,ilivyo ni kwamba ilianza grafiti ikafuatwa na udijei,mabreka,halafu rap(yasin,2001;rose1994;toop2000;mitchel2001;southern1983).
Mizizi hasa ya rap Afrika, mbali ya kuanzishwa na wamarekani weusi una sifa mbalimbali za kimuziki na kifasihi simulizi za kiafrika ikiwa ni pamoja na matumizi ya midundo au ridhimu usimulizi,kiitikio na majigambo.Hiphop au muziki wa kizazi kipya ulikuwa kama jukwaa la mshikamano miongoni mwa vijana wa kimarekani  wa mjini na baadaye kuwa kama mtindo  wa maisha na sauti ya vijana .Ni utamaduni ambao uliwakutanisha wale walionyimwa haki ,walionyanyaswa  na kugandamizwa katika historia  na ukawa utambulisho  miongoni mwa Wamerekani weusi na ukawa kipaza sauti chao.

Muziki wa kizazi kipya au rap nikipengele kimoja wapo  cha utamaduni wa hiphop.Ni aina ya ushairi ,usimuliaji,au usemaji unaopangwa vina kwa kufuata mdundo wa ala  za muziki (ambao tayari ulisharekodiwa ).Muziki huu ulianza kama sehemu ya burudani  ya vijana weusi na baadaye  ukakuwa na kuenea  na kuwa maarufu  katika nchi nyingi  duniani .Hapa Tanzania  muziki wa kizazi kipya ulianza mwaka 1980.Vijana walianza  kuimba wakiwa ufukweni na baadaye katika sherehe mbalimbali ulianza kisikika redioni  mwaka 1995.
Kama ilivyokuwa kwa Wamerekani weusi vijana wengi  wa Kitanzania pia hutumia muziki wa kizazi kipya  kuelezea matatizo yao  ya kila siku kama vile ukosefu wa ajira  na athari zake ,Dola na nguvu zake  na umasikini.Hapo mwanzoni  nyimbo hizi ziliimbwa kwa kuwaiga wasanii wa  kimarekani  kama vile Vanillah Ice,Kriss Kross na Naughty by Nature, halikadhalika walitumia  baadhi ya maneno au sentensi kutoka nyimbo hizo .Hivyo kila mwimbaji  alijaribu kuwa mbunifu na kutunga nyimbo zake mwenyewe ilikuwapata mashabiki na kujiongezea umaarufu.Muziki wa kizazi kipya unaojulikana sana kwa jina la Bongo flava ulishika kasi sana mwaka2000.muziki huu umewapatia vijana wengi  fusra baada ya kusikia nyimbo kutoka n’je ya nchi.

Tanzania  hususani marekani ambapo vijana waliiga na kutoka na staili yao wakitumia lugha ya Kiswahili na wengine walichanganya nyimbo hizo na lugha kama Kingereza na lugha za asili.
Walichoweza kufanya vijana wengi ni kuiga (ala) za Wamerekani lakini waliamua kutumia lugha ya Kiswahili ili kuweza kufikisha ujumbe  kwa Watanzani na kama inavyojulikana kuwa kazi yoyote ya sanaa ina malengo  ya kufundisha ,kukosoa na kuburudisha.Wakati muziki huu unaanza Tanzania  hakuweza kuzaniwa kama unge fika karne za mbele lakini hivi sasa una waimbaji wengi pamoja na mashabiki wengi wa rika tofauti hasa vijana, watu wazima si wote wanao upenda muziki huu.
Baadhi ya vijana waliokuwa waanzilishi wa muziki huu kwa Tanzania,vijana wa mwanzo kabisa ambao kuanzia mavazi yao na kufokafoka kwao kulikuwa ni burudani tosha kwa watu kuanza kudadisi kuhusu utamaduni wa mavazi hayo ambayo yalionekana  kama uhuni tena wa kupita kiasi kutokana na uvaaji wa mavazi hayo kihip hop.Hawa ni baadhi ya wasanii wachache ambao walivaa kihip hop Samora Avenue,John simple,DJ Rusual,The BIG ONE,Babu manju,Davidi,Nhigula,Abdulhakim Magomelo,Kessy,Ibony Moalim,Tom
 London,Opp(now JayP)  NA DJ Ngomeley.Hao walikuwa chachu katika uvaaji wa kihiphop na katika kughani Muziki huu wa kizazi kipya.
Pia kuna wasanii wa mwanzo kabisa katika kuimba muziki huu wa kizazimkipya akiwepo mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (BBG lianza na MR.11)FreshXE Mtui,Adili Kumbuka,KBC(Mbeya Tech)Saleh Jabir,Samia X,The Big,Rhymson,2Proud,Kwanza Unit,GWM,Hard Blasters na Bantu pound ambao walianza kuimba katika sherehe za mashuleni,kwenye matamasha mtaani kabla hata ya kurekodi nyimbo zao studio. Kulikuwa na wale wenye kuimba kama wanamuziki wengi wa Marekani kwa kupitia matamasha mbali mbali katika Jumba la utamaduni la Urusi,Korea na mengineyo yaliyokuwa yakiandaliwa hasa na wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari jijini kama Forodhani pia matamasha yaliyokuwa yakifanyika kando kando ya ufukwe ambako wengi wenye kutaka kuimba walijitokeza.

Kulikuwa na  kundi kama la Mawingu na mwana dada Pamela,mwanadada Stara Thomas na Judith Wambura ambao uwezo wa kughani na kuimba kama Mc Lyte ulimuinua hasa alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha DJ show ya Radio One,shukrani kwa Ipyana Malecela Mkwavi (RIP) kwa zawadi ya LP yenye mdundo,ala ya single “Keep,Keeping on” ndiyo iliyomtambulisha Jay Dee wa leo Radioni kwa mara ya kwanza japokuwa kabla ya hapo alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani lakini mweye kusita kuingia kwenye muziki wa kidunia.
Pia Kundi la R&B lililojulikana kama Four Krewz Flava pia Herbert Makange ambaye pia alikuwa akiimba. Kwa kufanya haya na mengineyo mengi muziki huu sio tu utakuwa ni wenye kujijengea heshima bali kuweka kumbukumbu kubwa ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania na hadhi yake kuwa ni ile isiyofutika kwa urahisi machoni na akilini mwa kizazi cha sasa na hata kile kijacho kwa muda mrefu.

1.3.1 HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI.

Kiswahili ni lugha ambayo inawekwa katika kundi la lugha za Kibantu. Neno “Swahili” linatokana  na neno la Kiarabu “sahel” linalomaanisha “sawahil” na katika Kiswahili ni “mpaka” au “pwani”(linalotumika kama kivumishi kumaanisha “wakazi wa pwani”. Kuongeza kwa herufi mbili za “ki” [‘lugha’] kupata “Kiswahili” kumaanisha “lugha ya pwani”. Wakati mwingine, neno “sahel” linatumika kumaanisha “mpaka wa jangwa la Sahara”. Unganishaji wa herufi ‘i’ mwisho wa neno “Kiswahili” ni kutokana na umbo la  kivumishi katika lugha ya Arabu (‘sawahil’). Jambo la hakika ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo imeazima maneno kutoka Kiarabu, Kiuajemi, Kireno na hivi karibuni Kiingereza. Hali hiyo, imekifanya Kiswahili kufika kiwango cha lugha ya kisasaZamani, Waswahili walitumia utawala wa mfumo wa mamlaka moja. Karibu na karne ya 10, pwani nzima ya Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa mfalme mmoja ambaye aliishi katika mji mkuu wa Safala.

Karibia karne ya 14, jamii ya Waswahili ilibadilishwa kuwa nchi yenye miji ya kisasa. Miji mingi hiyo ilikuwa midogo yenye majengo ya jiwe, misikiti, familia ya Waislamu walio na tabaka la juu na wengine wengi ambao hawakuwa Waislamu. Majiji makubwa kama Mogadishu, Pate, Mombasa, Malindi, Zanzibar na Kilwa yalijengwa na marijani na matumbawe ambayo yalionesha dalili za utajiri kwani yalikuwa  na vifaa vya ujenzi  vya gharama sana. Idadi kubwa ya majiji hayo yalikuwa chini ya utawala wa Sultani ambaye alikuwa Mwislamu. Ilifika kipindi ambacho majiji makubwa hayo yalitawala mengine ambayo hayakuwa na uwezo wa kuchukua mamlaka. Kwa mfano, Sultani wa Kilwa alitawala sehemu kubwa ya pwani ikiwemo Sofala na Zanzibar. karne ya 14 (kipindi cha mwaka 1390) idadi kubwa ya miji iliyotawaliwa na Masultani wa Omani kama Sofala ilianza kupata uhuru. Kuanzia karne ya 8 mpaka 19, Kiswahili kilizumgumzwa na makabila kadhaa kwa umbali wa maili 1000 kwenye pwani ya Afrika Mashariki kati ya Mozambique na kusini kwa Somalia.

Kwa mamia ya miaka,sehemuambazo palikuwa na Waswahili palikuwa vituo vya biashara muhimu kati ya wenyeji na nchi kama Arabia, India na Asia Mashariki na raslimali za Afrika Mashariki. Ushirikiano huu wa kibiashara uliathiri jamii ya wenyeji (Waswahili), utamaduni, dini na lugha  katika Afrika Mashariki. Katika enzi za karne ya 19, Kisiwa cha Zanzibar kilikuwa kituo kikuu na cha umuhimu kwa ajili ya biashara iliyokuwapo kwenye pwani ya Afrika Mashariki; sehemu ambapo safari ya watu na usafirishaji wa bidhaa kwenda katikati ya eneo hilo (Afrika Mashariki). Wakati huo, Kiswahili kilitumika kama lugha ya biashara na ya mawasiliano. Kutokana na hali hii, watu wengi ambao ni Waswahili walihamia kuishi kwingine hasa katikati ya Afrika Mashariki kwa lengo la kufanya biashara.

Naye Profesa Whiteley (1969), amefafanua hali hii akisema,“Wakati upanuzi wa biashara ulipobadili mbinu ya biashara kwa kutumia msafara kutoka pwani, haja ya kuhitaji lugha muafaka wa biashara ulikuwa muhimu sana na hapo ndipo Kiswahili kilipojizindua jukwaani”.(“When the expansion of trade shifted the initiative to caravan from the coast, the need for an effective lingua franca became acute and Swahili came into its own”).Baadaye, yaani katika karne ya 20, wakati wa ukoloni wa Uingereza, lahaja ya Unguja (aina ya Kiswahili iliyotumiwa na Wazanzibari ilienea sana Tanzania na aina nyingine ya Kiswahili ilienea mpaka Kenya, Uganda, Burundi, Congo, Mozambique na ilifika mbali sana hata mpaka Afrika Kusini. Aina hii ya Unguja ilikuwa imeathirika sana na Kiarabu.

Aina nyingine zilizojitenga kutoka Unguja zilipitia mabadiliko tofauti wakati wa usambazaji wa Kiswahili. Kwa sasa, tuna aina nyingi za Kiswahili zinazotofautiana angalau kidogo sana katika lugha hii ya Kiswahili. Ni muhimu kukumbuka kwamba kulikuwa na sababu moja ambayo ilisababisha usambaaji wa Kiswahili. Hii ilikuwa hali ya kuoana miongoni mwa wafanyabiashara (ambao walikuwa Waswahili) na wenyeji ambao wengi walikuwa watumwa. Inakubalika bila shaka kwamba watoto waliozaliwa na familia ya mchanganyiko huo walipata nafasi ya kujua na kuongea Kiswahili.

1.4USULI WA TATIZO LA UTAFITI
Wahakiki na watunzi wa nyimbo hizi wamejikita kwa kiasi  kikubwa kuangalia fani vilevile na maudhui, Lakini tahakiki zao zimejikita katika fani.katika maudhi watafiti na wahakiki wengi wamegusia baadhi ya vipengere na kukisahau kipengere cha utabaka kutokana na matumizi ya lugha ya kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya ambapo hutenganisha jamii kwasababu nyimbo zao huonekana ni za vijana tu.Chachage(2002)amezungumzia muziki wa kizazi kipya kuwa lugha inayotumika katika nyimbo hizi zina matumizi makubwa ya maneno  yanayoibuka kila siku ambayoyanaonekana kuwa lenga vijana  na ndiyo wanaoelewa maneno hayo.Jarida la TUKI(2006)wameelezea vipengere mbalimbali vya Fani hasa lugha katika muziki wa kizazi kipya kama uchanganyaji wa lugha,lugha isotafsida,matumizi ya lafudhi za lugha za asili,matumizi ya taswira na matumizi ya tashititi. na maudhui ya muziki huu kama umasikini,unyanyasaji,ukosefua wa ajira na uchumi.

Hii inadhihirisha kwamba suala la nafasi ya lugha ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi  kipya kama kipengere cha fani na  pia katika maudhi hawajaangalia kwa undani jinsi matumizi ya misamiati ya lugha ya kiswahili yanavyotumika katika nyimbo hizo inaleta utabaka kwa jamii kwasababu misamiati hiyo inaeleweka na vijana pekee yao.kukwepwa kwa vipengere hivyo kwa wasikilizaji wa nyimbo za muziki wa kizazi kipya na watumiaji wa lugha ya Kiswahili kuna leta utabaka katika jamii.Hii ni kwasababu usikilizaji wa nyimbo hizi unahitaji misamiati inayoeleweka na inayozingatia utamaduni wa lugha husika kwa jamii ili iwe mali ya jamii nzima.Hivyo,utafiti huu unatarajia kuziba pengo lililobainishwa hapo juu kwa kuchunguza hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya,kuangalia sababu zinazopelekea muziki wakizazi kipya kusikilizwa na vijana zaidi na mchango wa muziki wa kizazi kipya katika lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
1.5 TAMKO LA UTAFITI .
Katika kipengele hiki nilishughulikia  mada ya utafiti ambayo ni  nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.Watafiti wengi waliotangulia  walichunguza lugha ya kiswahili ilinavyotumika katika muziki wa kizazi kipya ambapo waliegemea zaidi kwenye kipengele cha fani. Hivyo utafiti huu ulichunguza nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya kwa kuzingatia kipele cha maudhui .
1.6MALENGO YA UTAFITI  .
Malengo ya utafiti huu yamegawanywa katika sehemu kuu mbili,sehemu ya kwanza ni malengo ya jumla na sehemu ya pili ni malengo mahsusi.
1.6.1 Malengo ya jumla.
Utafiti huu unalenga kuchunguza nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.

1 .6.2 Malengo mahsusi.
Malengo mahususi ya utafiti huu ni kama yafuatayo:
         i.            Kuchunguza hadhi ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya.
       ii.            Kuchunguza sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana zaidi.
      iii.            Kuchunguza mchango wa muziki wakizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujmla.
1.7Maswali ya utafiti.
Maswali yatakayo tuongoza katika kufikia malengo hayo ni:
         i.            Lugha ya Kiswahili ina hadhi gani katika  muziki wa kizazi kipya.
Swali hili liliandaliwa ili liniongoze katika ukusanyaji na uwasilishaji wa data za utafiti wangu.Hili ni swali kuu la msingi katika tasnifu hii kwa kulijibu swali hili nilitaraji kubaini hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,kwa kuwa wasanii wengi wa nyimbo hizi utumia lugha ya  Kiswahili katika kufikisha maudhui ya nyimbo zao.
       ii.            Kwanini muziki wa kizazi kipya unasikilizwa na vijana tu?.
Swali hili liliandaliwa ilikukamilisha jambo mahususi lililoulizwa na swali kuu.Kwa kutumia swali hili mambo yaliyopelekea muziki huu kuwa mali ya vijana kwa asilimia kubwa na sio wazee.Swali hili lililenga zaidi katika kuibuka  na taarifa  kuhusu mada ya utafiti na kuweza kujua nini kianacho pelekea muziki huu kusikilizwa na vijana zaidi.
      iii.            Kuna machango gani wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.Swali hili liliandaliwa ilikujua mchango unaopatikana katika muziki wa kizazi kipya kwa jamii yetu,hii imetokana na sababu za mwanzo ambazo zilionyesha muziki huu ni wakihuni.hivyo swali hili litasaidia kufafanua mchango wa muziki huu katika utamaduni wa lugha yetu ya Kiswahili.
1.6 Manufaa ya Utafiti.
Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuleta manufaa yafuatayo:
         i.            Kwanza kabisa, utafiti huu utapendekeza maoni mbalimbali ambayo yanaweza kutumika kuharakisha utekelezaji wa wasanii kutunga nyimbo zao kwa kutumia misamiati iliyo sanifu ambayo itasikilizwa na jamii nzima.
       ii.            Vilevile, matokeo ya utafiti huu yatawasaidia viongozi  na Taasisi mbalimbali zinazohusika katika  kukuza lugha ya Kiswahili na sanaa, kuhakikisha wasanii wanaitumia vema lugha ya Kiswahili na kuuzingatia utamaduni wake wanapotunga nyimbo zao.
      iii.            Kuonyesha umuhimu wa muziki wa kizazi kipya kwa jamii nzima na kuisaidia jamii kuelewa mchango wa muziki wa kizazi kipya kwa vijana.
     iv.            Kuonyesha nafasi  ya lugha ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya.
1.9 Nadharia ya uchambuzi.
Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya uhalisia  hivyo,ukusanyaji wa data,uchambuzi na uwasilishaji wake utafanywa kwa kuzingatia nadharia hii.
NADHARI YA UHALISIA.
Uhalisia ni hali ya ukweli kuhusu kitu au jambo na utayari wa kuupokea ukweli huo au kutendea kwa njia inayowezekana ,sifa ya kufanana kabisa na mtu,kitu,au mahali ambapo pamewakilishwa kwa njia ya michoro,muziki,mchezo wa kuigiza ,kitabu na filamu.Mtindo wa sanaa na fasihi ambao hujaribu kuwasilisha jambo ambalo linafahamika au liko wazi katika maisha halisi. Uhalisia kama nadharia  ya kiuhakiki ni mkondo unaosisitiza usanii wa matukio       katika  fasihi ufanye matukio hayo yajitokeze kama maisha ya kila siku.
Neno uhalisia lilitumiwa kwa mara ya kwanza huko Ufaransa katika miaka ya 1850’s kwa lengo la kuelezea  kazi za sanaa zilizojaribu kusawiri ulimwengu kama ulivyo na si unavyodhaniwa   au kufikiriwa. Kama nadharia ya uhakiki,uhalisia huzingatia  namna ya ukweli unavyosawiriwa katika nyakati mbalimbali.Jinsi  ya kuusawiri au kuuelewa uhalisia hutofautiana  kutoka jamii hadi jamii na kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine,
            -Zamani za akina Galileo Galilei dunia ilidhaniwa kuwa kama meza,kumbe ni ya mviringo.
 -Zamani sayari  zilidhaniwa ni maumbo yasiyofikika,kiumbe kikitua huko,zitatunguka,kumbe ni mada zenye kudhibitiwa na mivutano  kama dunia.
            -Zamani kulidhaniwa kuwako ulimwenguni mmoja tu wenye mifumo ya jua ,kumbe yasemekana kuna ulimwengu zingine.
            -Zamani hakukuwa na vifaa anuwai  vya kisasa vya kizazi  na burudani ambavyo vimerahisisha sana maisha. Yote  hayo  na mengineyo mengi,kadiri ambavyo yamekuwa  yakitokea,ndivyo  ambavyo yamebadili fikra za watu.
Kwa hiyo kila kizazi kina uhalisia  wake ambao huweza kusawiriwa na fasihi,lakini fasihi inaweza  kusawiri uhalisia wa wakati ujao kwa kutumia huu uliopo.Hali kadhalika,fasihi inaweza kusawiri  uhasilia kwa kutumia ubunifu unaongozwa  na msingi  ya kisayansi  na misingi ya kihistoria .
Nadharia ya uhalisia iliwekewa misingi na mwana-falsafa na Hegel katika kitabu chake cha Aesthetik(UJUMI),Hegel alipendekeza matumizi ya dhana ya uhalisia ielezee kazi ya fasihi  inayowasilisha ulimwengu  wa maisha ya  kijamii  yenye wahusika wanaotenda mambo yanayodhibitiwa na hali ambayo wahusika hao wamo.Nadharia ya uhalisia husisitiza usawiri wa uhalisi katika ukamilifu wake,kwa maana kwamba yanayoshughulikiwa hayana budi kudhibitika.Hivyo mchango mkubwa wa nadharia hii ni kuchora maisha kama  yalivyo.
Mtaalam Larkin(1972),anasema  kuwa madhumuni ya mwandishi kwa anaowaandikia ni kuwaakisia ulimwengu wao wa kawaida,Kwa hiyo ulimwenguni huo sharti uwe halisi au wa ukweli.
Lukacs(1972),anasema  kuwa  nadharia  ya  uhalisia  ilianza  kuhusishwa  katika  fasihi kwa sababu  waasisi wa nadharia  hii waliona kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kazi za kisanaa na mtazamo wa msanii kuhusu  mazingira  aliyomo.
Hivyo,ninapotumia nadharia hii katika  fasihi tunataka kuona ni kwa kiasi gani mwandishi anatuleta karibu na maisha ya kawaida  ya kila siku.
Mhimili wa uhalisia ni  msanii kujitahidi kuchora maisha jinsi yalivyo  bila kuathiriwa;na hufanya hivyo kupitia vipengele muhimu vya maisha  kama  vile siasa,uchumi,utamaduni,jamii.lugha huwa ya kawaida inayoeleweka katika jamii  husika,mandhari na matukio yawe yanaonekana,kujulikana na yaendane  na jamii husika.,Msanii huangalia matatizo ya jamii na kuchunguza chanzo chake na kuzingatia mabadiliko ya  kihistoria ambayo husababisha hali mbalimbali ya maisha  ikiwa pamoja na kuathiri mfumo wa kifikra.
Hata hivyo  mchango wa  muziki wa kizazi kipya hususani katika kutumia lugha ya kiswahili   nitachunguza kwa kuangalia  vipengele vya  historia ya jamii lengwa,masuluhisho ya muziki  katika  katika kutumia lugha ya Kiswahili kwa jamii na matatizo ya muziki hii katika  kulenga jamii.


SURA YA PILI :
2.0 MAPITIO YA MAANDIKO.
Sura hii inabainisha machapisho mbalimbali yanayohusiana  na mada hii,machapisho hayo yatahusu maandiko mbalimbali ya muziki wa kizazi kipya na lugha .Baadhi ya waandishi wameelezea muziki wa kizazi kipya kwa kuelezea maudhui na fani.Kwa ujumla kupitia kazi hizo muziki wa kizazi kipya umeonekana kuwa lenga zaidi vijana kutokana na lugha inayotumika katika nyimbo hizo.Muziki wa kizazi kipya umeonwa kama chombo kinacho wasaidia vijana kuelezea matatizo yao kwa kutumia lugha wanayoielewa wenyewe.

2.1 MAANDIKO KUHUSU MUZIKI WA KIZAZI KIPYA.
Waandishi mbalimbali pamoja na wasanii wameuelezea muziki wa kizazi kipya jinsi ulivyoanza na  mtazamo wao kuhusu uelekeo wa muziki huu hapo baadaye. Machapisho kuhusu wataalamu wanasema nini juu ya muziki wa kizazi kipya.
Hapa tutawaangalia(Chachage,2002;Mgembe,1998;Fenn&Perulla,2000;Senkoro2003;)

Majembe(1998),anasema
uchanganyaji wa lugha ndiyo sifa kubwa inayojitokeza katika nyimbo hizi
 kwasababu wasanii wengi huchanganya lugha tofauti ilikuonyesha ubunifu
 tofauti na wasanii wengine na kupelekea watu wazima kuona nyimbo hizo ni
uhuni”.

Senkoro(2003),katika maandishi yake ya sanaa anasema :
wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatumia lugha kama bidhaa
ambayo wameizalisha baada ya kujiajiri wenyewe.Ingawa nyimbo
hizi zina mchanganyiko wa kiingereza, Kiswahili na lugha za kienyeji
nyimbo hizi zinatumia sana misimu sababu ndiyo inayoeleweka kwa vijana”.

Chachage(2002) anasema :
Watanzania wengi wanadhani muziki wa kizazi kipya unapotosha
utamaduni wa mtanzania hawa ni wapotofu wa mawazo.kwani utamaduni
katika jamii ni mwingiliano wa mambo mengi toka ndani na n’je ya nchi
Chachage yupo sahihi lakini hata kama tunaiga utamaduni kutoka n’je haipaswi tuvuke mipaka ya utamaduni wa nchi yetu na lugha yetu..

Fenn na perulla(2000)
“matumizi haya ya uchanganyaji lugha yanatokana na itikadi ambayo
 imejengeka miongoni mwa wasanii hao na pia kwa lengo la kupata
 mashabiki wengi.Wanatumia kingereza sababu ni lugha ya kimataifa,
wanatumia Kiswahili kwasababu ni inayoeleweka kwa watumiaji wengi.”

 Senkoro,Majembe na fenn Perulla wameangalia nyimbo za muziki wa kizazi kipya kwa kigezo cha lugha hasa lugha ya kingereza.

2.2Pengo linalopaswa kuzibwa.
Ukiyatalii  maandiko  hayo utaona kuwa hakuna aliyezungumzia  suala la nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,wachache wamejaribu kuelezea kidogo suala hili kwa kuchunguza vipengele vya fani vinavyopatikana katika nyimbo hizo hata hivyo waliotupia jicho suala  hili halikuwa lengo lao bali limejitokeza katika mchakato wa kutiririsha  mawazo yao.kwa kufanya hivyo tunakosa muwala mawazo.Aidha imebainika kuwa kipengele hiki kina epwa na wahakiki na watafiti wengi wa kazi za fasihi,watafiti wa lugha ya Kiswahili ambao uamua kufanya utafiti wa jumla  wa fani na maudhui kutokana na upungufu huo niamua kufanya utafiti ili kubaini mambo yanayojitokeza katika katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya, katika lugha ya Kiswahili kwa kuangalia nafasi yake katika muziki wa kizazi kipya.Hatimaye kutathimini kufaa na kutofaa  kwa muziki wa kizazi kipya kwa wakati uliopita/uliopo na ujao.

SURA YA TATU:
3.0 MBINU YA UTAFITI.
Sura hii itaelezea  mpango  mzima wa utafiti kama vile,eneo la utafiti,jamii ya watafiti, zana na mbinu za kukusanya data pamoja na uchambuzi wa data.
3.1Mpango wa utafiti.
Utafiti huu ulikuwa wa uwandani na maktabani .Data zilikusanywa  kutoka kwenye  nyimbo za muziki wa kizazi kipya.Mbinu ya ufafanuzi ndiyo iliyochukua nafasi katika utoaji wa matokeo  ya utafiti huu.Data zote  zimekusanywa zimehakikiwa,kuchambuliwa na hatimaye kutolewa maelezo ya kina ili ziwafikie wasomaji .Nililikwenda uwandani kuwahoji wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya ,watumiaji wa lugha Kiswahili  ili kujua  ni kwa namna gani? Muziki wa kizazi kipyamuziki wa kizazi kipya una mchango gani  katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili pamoja na jamii.

3.2. Walengwa wa utafiti.
Walengwa wa utafiti huu ni  jamii ya watafitiwa kwa ujumla wake.
3.2.1 Jamii ya watafitiwa.
Jamii iliyo lengwa kutoa taarifa za utafiti huu ilijumuisha makundi yafuatayo:
         i.            Nyimbo mbalimbali za muziki wa kizazi kipya zimesaidia kuonyesha jinsi lugha Kiswahili ilivyo na nafasi katika muziki huo.

       ii.            Wapenzi ,wasanii na wasikilizaji wa nyimbo za muziki wa kizazi kipya au bongo fleva.

3.2.3Eneo la utafiti.
Utafiti ulifanyika Dodoma Tanzania.Eneo hili lilitosha katika ukusanyaji wa data.Dodoma ni eneo ambalo mtafiti anasoma ilikuwa rahisi kupata maoni kutoka kwa watu ambao ni wapenzi wa muziki na watumiaji wa lugha ya Kiswahili.

3.3 ukusanyaji wa data .
Sehemu hii inafafanua  njia na zana tofautitofauti zilizo tumika katika ukusanyaji data.


3.3.1Zana na  njia za ukusanyaji data.
Zana zilizo tumika ni uhojaji ,daftari na kalamu , mahijiano,na majadiliano ya vikundi pia nilisoma vitabu mbalimbali ambavyo ni vyanzo vya upatikanaji  wa data.Nilitumia zana hizi kutokana na elimu ya walengwa wangu  wa eneo lenyewe la utafiti.
3.3.2Uhojaji.
Nili uulizaji maswali ana kwa ana au kwa njia ya simu na njia ya mtandao(facebook na  barua pepe) ambayo niliwauliza watafitiwa kwa ajili ya kupata na kukusanya data .Nilitumia zana hii katika kukusanya data kutoka kwa watu  wazima na vijana,wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wapenzi wa muziki huu. Uhojaji ulirahisisha upatikanaji wa data mbalimbali zinazohusu muziki huu wa kizazi kipya.

3.3.3 Daftari na kalamu.
Zana hizi zilitumika katika mahojiano na kupitia maandiko mbalimbali,nilitumia zana hizi wakati wa kunukuu data zilizo patikana kutokana na maandiko mbalimbali na mahojiano nilyo fanya kwa ajili ya kutumika  wakati wa uchambuzi na uunganishaji.

3.3.4Mchakato wa ukusanyaji data.
Data za maktabani zilikusanywa kwa kutumia mwongozo wa usomaji ulioandaliwa.Mwongozo huo uliniongoza wakati wa kusoma tasnifu,vitabu,majarida na vielelezo mbalimbali ili kupata data  za utafiti huu.Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia uhojaji.

3.3.5Uchambuzi na uunganishaji wa data.
Uchambuzi wa data za utafiti huu ulitumia mbinu ya ufafanuzi wa maudhui yaliyojitokeza kwenye ukusanyaji wa data za utafiti huu.Mbinu ya ufafanuzi ilitumika zaidi katika utafiti huu kwasababu ilikuwa ya maelezo zaidi na sio takwimu. 
3.3.6Vikwazo vya utafiti.
Mambo yafuatayo yalikuwa kikwazo katika kuyafikia malengo.
         i.            Uhaba wa fedha za kugharamia shughuli mbalimbali kama vile nauli kwenda kwenye maeneo ya kutafuta data ,ukusanyaji wa data pamoja na uunganishaji na uandishi wa ripoti.
       ii.            Muda katika kutafuta data kwasababu ilikuwa ni kipindi cha masomo na sio likizo.kwahiyo ilikuwa vigumu kupata muda wa kutosha katika kukusanya data kwa kina zaidi kutokana na kutumia muda mwingi kwenye masomo  ya darasani.


 www.jikonifashen.com 
SURA YA NNE.
4.0 MJADALA WA UTAFITI.
4.1Utangulizi
Sehemu hii ni ya muhimu sana kwasababu inaelezea namna utafiti ulivyofanywa uwandani .Hii ni sehemu yenye uchambuzi wa data pamoja na matokeo ya utafiti huu .hivyo katika sehemu hii  mjadala wa utafiti umegawanyika katika sehemu kuu nne zinazo akisi maswali yaliyoongoza utafiti huu .Sehemu ya kwanza inaelezea hadhi ya  lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
        Sehemu ya pili inaelezea sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana kwa asilimia kubwa.Sehemu ya  mwisho itaelezea  mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni  wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
4.2 Hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu (2005)inasema kwamba “hadhi ni cheo daraja, uluwa,taadhima,utukufu,2.Heshima,staha,turuhani.Hivyo katika sehemu hii tutaangalia hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.Kutokana na utafiti ambao umefanyika na mtafiti anathibitisha hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya  kwa kuangalia hadhi ya juu na hadhi ya chini.
4.2.1Hadhi ya juu ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
Katika kuitazama hoja hii mtafiti anathibitisha hoja hiyo kwasababu zifuatazo: kutokana na utafiti na utafiti uliofanyika imeonyesha kuwa lugha ya kiswahili lugha ina hadhi ya juu katika muziki wa kizazi kipya kuliko lugha zingine wanazo zitumia wasanii wengi  wa Afrika Mashariki kwa ujumla kwa mfano wasaniii wa Tanzania ambao wengi wanatumia lugha ya Kiswahili katika kutunga mashairi ya nyimbo zao nyingi.Lugha ya Kiswahili  inapewa kipao mbele katika nyimbo/mashairi yao kutokana sababu zifuatazo:


Lugha ya  Kiswahili ni lugha ya Taifa kwa nchi za Afrika mashariki.Lugha ya Kiswahili ni lugha ya taifa ambayo imepitishwa na sera ya lugha na mpango wa lugha ,ni lugha ambayo inaeleweka zaidi kwa jamii inayosikiliza mashairi ya wasanii  wa muziki  huu, wasanii wengi hutumia lugha ya Kiswahili kwasababu ndiyo lugha wanayo ifahamu vema na hii ndiyo sababu ya  wasanii wengi kujiingiza katika muziki  pasipo kuwa na elimu ya kutosha hivyo wengi wao uimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwasababu ndiyo lugha wanayoifahamu vema  ingawa lugha hii pia ni lugha  ya mawasiliano kwa nchi  za afrika mashariki.
Urahisi wa lugha ya Kiswahili.Lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo ni rahisi na inaeleweka vema kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya hivyo inakuwa rahisi kwao kuzungumza kutunga mashairi yao kwa kutumia Kiswahili na si lugha zingine ambazo hawazifahamu vizuri.
Katika utafiti uliofanyika  nilimhoji kijana mmoja anayesomea shahada ya isimu ya Kiswahili, mwaka wapili katika chuo kikuu cha Dodoma kuhusiana na hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya, anayefahamika kwa jina la Rehema mhapa na kusema hivi:
       “Lugha ya Kiswahili kwa mimi binafsi ni lugha ambayo naipenda sana kwasababu
        Ni lugha yangu ya taifa pia ni lugha ninayoielewa na nina uwezo wa kuizungumza
        Kwa urahisi bila kusitasita kama lugha zingine za kigeni mfano kingereza.Mimi ni
        Mpenzi mzuri wa muziki wa kizazi kipya kwasababu mashairi yao wanatunga kwa
        Kutumia lugha ya kingereza,hivyo hata ninapo sikiliza na furahia vionjo
        vilivyopo kwasababu lugha inayotumika nina ielewa vema na kilichopo ndani ya
        nyimbo yaani ujumbe naelewa zaidi kuliko nikimsikiliza 50cent.”
Kwa kuzingatia maelezo ya muhojiwa hapo juu tunapata dhana kuwa  wasanii pamoja na wasikilizaji wanaipa hadhi ya juu lugha ya Kiswahili kwa sababu ndiyo lugha yao ya taifa na wanaielewa vema kutokana na lugha hiyo kuitumia katika mawasiliano yao ya kila siku.
Kijana mwingine ambaye naye ni mwanafunzi anayechukua shahada ya kwanza ya isimu ya Kiswahili  pia ni msanii wa muziki wa kizazi  kipya ambaye alijifahamisha kwa  jina la James Christopher a.k.a JC aliseama hivi:
     
“Mimi katika utungaji wa nyimbo zangu napenda kutumia lugha ya Kiswahili
Kwasababu Ndiyo lugha ambayo ninamisamiati ya kutosha hata katika
utungaji wa  mashairi yanguSiwezi kukwama kama ambvyo nikitumia lugha ya Kiswahili kwahiyo hapo na kuwa naSwaga za kutosha katika kuimba na utungaji wa nyimbo zangu,na isitoshe ndiyo lughayangu ninayo itumia katika mishemishe zangu za kitaa”
Wasanii wengi wanaifahamu lugha ya Kiswahili zaidi.Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya elimu yao ipo chini kwasababu wasanii wengi wameishia darasa la saba wengine elimu ya sekondari  waliojitahidi sana  kidato cha sita ingawa asilimia kubwa wengi wameishia kidato cha nne,hivyo kutokana na utafiti uliofanyika inaonyesha kuwa wasanii hawa hawatumii lugha ngeni zaidi kutokana  na kigezo cha kutokuwa na elimu ya kutosha na wengi wao wanajiendeleza kwa kujifunza lugha ya Kingereza na lugha zingine  wanapokuwa wamefanikiwa katika soko la muziki, ili waweze kuwa na mawasiliano mazuri wanapo pata fursa ya kwenda kufanya shoo za  nyimbo zao n’je ya nchi.Hili tatizo ni kubwa na utafiti unaonyesha kuwa vizazi vya sasa wengi wao wana kimbilia kuimba wanapo shindwa kufaulu vema katika masomo yao pia wanapokuwa wamefanikiwa katika ajira hii ya muziki wanaikwepa elimu na kuendelea na muziki.Hali hii ndiyo inayopelekea lugha ya Kiswahili kupewa fursa ya kwanza katika utunzi wa nyimbo nyingi za wasanii wa  muziki huu wa kizazi kipya.

4.2.2 Hadhi ya chini ya  lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kpya.
Katika kuitazama hoja hii mtafiti anathibitisha hili baada ya kuchunguza  na kupata majibu tofauti kutoka kwa watafitiwa  namna ambavyo lugha hii inavyochukuliwa na jamii wanaposikiliza muziki  huu wa kizazi kipya.Yafuatayo ni maelezo ya baadhi ya watafitiwa  kuhusiana na lugha ya Kiswahili kuonekana ina  hadhi ya chini kutokana na namna inavyotumika katika nyimbo hizi za kizazi kipya.Yafuatayo ni maelezo ya watafitiwa kuhusiana na hoja hii ya Kiswahili kuonekana ina hadhi ya chini  katika muziki wa kizazi kipya.Mkazi mmoja wa Dodoma aliyejitambulisha kwa jina la mary john ambaye ana umri wa miaka 23,ni mfanyakazi wa saluni alisema hivi:
“Wasanii wetu wanatumia lugha ya Kiswahili vibaya,misamiati wanayoitumia katikaNyimbo zao inashusha hadhi ya lugha ya Kiswahili kwasababu wao wanatumia  lugha isiyotafsida katika nyimbo zao katika baadhi ya nyimbo zao na kuharibu utamaduni wa Misemo wanayoitumia ni ya mtaani sana kiasi kwamba baadhi ya maneno hatuyaelewi Vema na ujumbe haufiki ulivyokusudiwa  kwa jamii,zaidi wanao faidi muziki wa kizazi Kipya huwa ni vijana tu.”

Hivyo basi lugha ya Kiswahili inashushwa hadhi kutokana na matumizi mabovu  ya lugha wanayoitumia na kupelekea muziki huo kuonekana ni wa kihuni miongoni  mwa wapenzi wa muziki huu na wasikilizaji wa muziki wa kizazi kipya,kwa asilimia kubwa muziki wa kizazi kipya hapo mwanzo ulionekana ni wa kihuni  na unawahusu vijana kutokana na muziki huu mwanzoni uliimbwa na vijana kwa lengo la kufikisha matatizo ya vijana kwa njia ya nyimbo mfano katika swala la ajira kwa vijana,manyanyaso,umasikni na elimu vyote hivi viliimbwa na wasanii hawa lakini hivi sasa nyimbo hizi zimekuwa na changamoto kubwa katika mapenzi zaidi na kusahau mambo mengine ya kijamii ambayo wakiyaimba yataigusa jamii kwa undani zaidi.mfano misamiati aliyo itumia masanii huyuAboubakar Chende  mwenye umri wa miaka 16 anayejulikana kwa jina la Dogo janja yupo kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Makongo katika wimbo wake wa najua kuna misamiati aliyoitumia ambayo kwa mtu mzee hawezi kuelewa nini anachomaanisha mfano katika ubeti huu:
            “Nakimbiza kinyama mapaka maboya wanahema,hakuna kuhanya,tunawameza
            Tunawatema,mtakipatapata fresh ya mwaka paka wanatetemeka kuona wabena
            Meka tuko full mzukaaaaa,Wagoro tulianza tu Ngarenaro Masoro wameishiwa
            Idea wanatubero yelooooooooooo!”
Misamiati kama “kinyama” akimaanisha yeye ni zaidi katika kuimba,”kuhanya” ni neon la kibantu likiwa na maana ya kuhangaika au kuwa na hofu,”full mzuka” likiwa na maana ya kuwa kamili yaani kujikamilisha  hivyo basi mtu mzee hawezi kuelewa nini anacho maanisha msanii huyu.Hali hii ndiyo inayopelekea hata jamii nyingine kuona lugha ya Kiswahili ni lugha ya kihuni hivyo hali hii inashusha hadhi ya lugha ya Kiswahili kutokana na utumizi mbovu wa maneno  yasiyo sanifu.
Uchanganyaji wa msimbo.Kitendo cha kutumia lugha mbili katika sentensi moja au msamiati mmoja mfano katika wimbo huu wa msanii Nick aliomshirikisha Joe Makini katika mojawapo ya mistari iliyopo katika wimbo wake huo kachanganya lugha ya Kiswahili na kingereza  kama ifuatavyo:
           
“Yaani four plus four mtaani sio eight na bado utajiri aupo
            Nyuma skirt,hey babies squeeze everybody tuwanasomebody
            High,high me take you higher,nakupeleka higher higher
            Nakuhitaji kwa higher higher”
Msanii kaingiza maneno ya kingereza katika mistari ya nyimbo zake na hivyo kufanya lugha ya Kiswahili kuonekana kuwa haijitoshelezi kimsamiati,hali hii ipo katika nyimbo nyimgi za wasanii wa muziki wa kizazi kipya.Utafiti umeonyesha kuwa wasanii wengi huchanganya lugha  lugha kwa lengo la kupata soko la kazi zao kwa jamii,wasanii  wanapo tumia lugha mbili mfano kingereza na Kiswahili,Kiswahili na lugha za asili au kuchanganya na lugha zingine aidha kwa kuwashirikisha wasanii wa n’je katika kuimba nyimbo zao mfano wimbo leo wa msanii Ay aliomshirikisha msanii mwanadada Avril:
“Excuse me baby boy yasikie yanayotoka moyoni mwangu
            Inabidi ungoje boy nishalizwa, nishaumizwa sana
            Sina imani sina imani tena nishalizwa nishalizwa sana
            No no no aaaah aaaah I like the way your  lakini
Sidhani utanifaa kunipa raha  hahahaha! My heart is ready
And let it be.”
Nilipata uthibitisho huu baada ya kupata maelezo kutoka kwa msanii wa muziki  wa kizazi  kipya ambaye niliweza kuzungumza naye  kwa njia ya simu wakati akiwa katika tamasha la burudani nyumbani mjini Mbeya katika uwanja wa Nzomwe  ambalo huwakusanya vijana pamoja na wasanii tofauti kwa lengo la  kutoa burudani ya kutosha kwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya.Msanii Danny msimamu yeye alisema kuwa:
           

“Mimi kwa upande wangu naweza kusema kuwa tunatumia lugha ya kingereza
            Ilikuweka swaga tofauti katika nyimbo pia mpango mzima ni kupata mashabiki
Wakutosha  na kupata soko kutoka n’je na ndani ya nchi,kitu kingine  ni kuongeza vionjo na kuonekana tofauti na wasanii wengine ndiyo sababu wengine wanapenda kutumia lugha zao za asili,pia hata waandaaji(producer)wakati mwingine wao ndiyo wanapenda  kutumia lugha ya kingereza,mfano mimi katika wimbo wangu I just wanna peace mwanzoni producer(muandaaji)alipenda nianze kwa kuimba kingereza”
hii ni baadhi ya mistari ya mwanzo ambayo msanii huyu aliimba kwa kunipa vionjo vya mwanzo vya wimbo huu ambao lengo kuu ni kuwaasa wezi wa kazi za wasanii kuacha na kuwaonea huruma wasanii hawa:
            “It is the shame some nigger gonna slow the rolemen,slow down
            Your roll player,you know what I mean cause some nigger
            Have been acting right you know when you act like this is like
You don’t know what time is,so listen up here goes you nigger  talking shit.Nimechoka nyimbo zangu kupigwa redioni halafu silipwi hata kumi
Huu ni uhuni ,redio zinaingiza kwa matangazo ya biashara,inamaana
Wimbo wangu unaopigwa ni hasara kwanini haulipwi  huu ni uchawi
Sheria haizingatiwi au nazo wameziloga,nazielezea hisia zangu bila uwoga
Hivyo hali hii ndiyo inayoonyesha hali kubwa iliyopo sasa kwa wasanii wengi  ambao wameimba kwa kuchanganya lugha tofauti katika lugha zao  huku lengo lao kubwa likiwa ni kufikisha ujumbe kwa jamii,kwa watu wengine ambao wanafahamu lugha ya Kiswahili na wasio fahamu lugha ya Kiswahili.Huku wasanii wengine wakitumia lugha zao za asili katika kuimba ili kuitangaza lugha zao  na utamaduni wao mfano Mr.Ebbo katika wimbo wake wa mimi mmasai bwana.
  
“mimi mmasai bwana nasema mimi mmasai nadumisha mila ile nyingine ishashindwa Mi mmasai bwana nasema mi mmasai”
4.3 Sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana kwa asilimia kubwa. Swali hili ni mojawapo ya maswali katika maswali ya utafiti huu,linajadili mambo ambayo yanachangia vijana wengi kusikiliza muziki wa kizazi kipya kuliko kundi lingine katika jamii.Utafiti huu umepata data ambazo zinapelekea vijana wengi kusikiliza muziki wa kizazi kipya zaidi kuliko nyimbo zingine kama nyimbo zingine ,mfano dansi,r&b na ragge,sababu zilizopatikana kutokana na utafiti  huu ni lugha inayotumika kwenye nyimbo hizo ni ya mtaaani,nyimbo nyingi zinalenga maisha ya vijana,ni sehemu ya ajira ya vijana ambayo wanaitegemea,vijana wengi wanapenda utamaduni wa nje kuliko utamaduni wao pia muziki wa kizazi kipya ndiyo muziki ambao kwa sasa una wafaa vijana kutokana na kipindi kilichopo.
Lugha inayotumika katika muziki wa kizazi kipya ni ya mtaaani.Kutokana na utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa kwa asilimia kubwa misamiati wanayo itumia  katika mashairi yao  sio sanifu utumizi wa maisamiati ya mtaani ndiyo chanzo cha vijana kusikiliza muziki wa kizazi kipya kwa sababu kinachoongelewa katika nyimbo hizo huwa wanaelewa vema ,tofauti na mzee ambaye akika kaa na kusikiliza nyimbo hizo hawezi kuelewa kabisa nini kinachozungumzwa katika nyimbo hizo.mtafiti alipata uthibitisho wa data hii baada ya kufanikiwa kumuhoji mzee  Abdallah Yusufu mwenye umri wa miaka 55 mfanyabiashara wa Dodoma katika soko la Sabasaba wakati akijibu swali hili kuwa kwanini muziki wa kizazi kipya uansikilizwa na vijana kwa asilimia kubwa:
                “Mwanangu mimi mzee  na mda wote nipo hapa sokoni,kwanza wanachokiiamba
            Vijana hawa wa siku hizi mimi naona uhuni maana huwa hata sipendi kusikiliza
            Nyimbo zao,mwananagu  hata nikisikia sitelewa maneno wanayoyatumia”
  Kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi wa sekondari ya Jamhuri mjini hapa Dodoma yeye alisema
            “Sisi vijana tunapendelea  muziki wa  kizazi kipya kwasababu ndiyo muziki wa vijana
            Hatuwezi mkusikiliza dansi wala zilipendwa kwa kuwa hizo nyimbo zilikuwa  za wazee
            Wetu,pili ukizingatia muziki huu wa unatugusa vilivyo yaani zile swaga zake mimi
mwenyewe     nazikubali sana  hasa msanii Chidi benz,Mr.temba kiujumla kundi
            zima la wanaume family kwamba wanacho kiimba kinatugusa vilivyo”
Hivyo basi kutokana na data hii tunaona kuwa muziki wa kizazi kipya ni wa vijana  wakileo mfano katika wimbo wa msanii Chidi benzi  katika wimbo wa Dar es salaam stand up tunaona maudhui yanayo imbwa na misamiati iliyopo ndani ya wimbo huu zinavyo akisi vijana zaidi na kufanya wazee kushindwa kuelewa baadhi ya maneno yana maanisha nii katika nyimbo zao.
“ Sijali  bado chenga nawakomba  ,mi beat na talwaza kama mumii na komba
Kama shilingi na konda,kicheche na ng’onda mlio wa vuumu na Honda
Spiriti na kidonda ,sipigani nikang’ata basi bora nikimbie ,si ng’ang’ani kung’ata
Bali uwezo ndiye , napanda siku baada ya siku  sipandi mchana nishuke usiku
Naamini kitu kuliko kukosa kitu ,love kwa wasanii,love kwa wana jamii
Love mpaka kwa kina na niii hihiiiiiiiii hiii msitenge mwenzenu jamani chonde
Nawawakilisha mtatoka msikonde,hey my African people tukaze tusonge mbele
Nawa wakilisha tusisahau hii miiko tusonge mbele tugange basi hayo tusonge mbele
Tuachekupiga miayo tufikiri kwa urefu”


Hivyo basi katika wimbo huu ambao msanii anawataka watu kuwa amka katika swala la maendeleo na  na pia wale wenye nia ya kuimba wasichoke bali wakaze mwendo ndiyo maana anasema sing’ang’ati kung’ata bora akimbie bali uwezo wake ndiye.hivyo basi kama mtu mwenye lengo na nia kweli inakubidi kupambana.

pia wasanii wa Tanzania wameanza kuimba nyimbo zao kwa kuingiza lugha ya kisheng katika nyimbo zao ambapo kishengi ni  lugha ya mseto inayojumuisha Kiswahili na Kiingereza na hata msamiati kutoka lugha zingine za Kenya Sheng ni kifupisho cha “Swahili-English ,Sheng ni namna ya msimbo au kilahaja cha kundi fulani miongoni mwa vijana. Mfumo huu wa  mawasiliano umesanifiwa na vijana hasa wale wanaoishi katika sehemu za mjini .Mfumo huu  wenyewe hufuata muundo wa kisarufi wa Kiswahili na lugha nyinginezo za Kibantu ila hutumia maneno mengi mapya ya kubuniwa na ya mkopo kutokana na lugha mbalimbali kikiwemo kiingereza na lugha nyinginezo za Kiafrika kama vile Kikamba,Kiluo, Kikuyu, Kiluyia na Ekegusii. Maelezo haya ya kijumla kuhusu maana ya Sheng yametolewa na wasomi kadha kama vile:

 Mkangi (1984: 17), ambaye ameueleza msimbo huu kama lugha mseto au lugha “kiunzi” ya kizazi kipya cha vijana wa mijini. Pia Ogechi (2002: 3) and Shitemi (2001) wanakubaliana na maoni hayo kwamba Sheng ni msimbo wa kijamii unaotumiwa hasa na vijana wa mjini na
 mashambani nchini Kenya. Maelezo haya yanatoa baadhi ya sifa za kimsingi zinazoutambulisha msimbo huu. Kwa mfano, hutumiwa sana na vijana ilikuji tambulisha kama kama kundi la kijamii. Maoni haya pia yameungwa mkono na shitemi.Wachunguzi wengi wanakubaliana kuwa Sheng ilizuka katika miaka ya katikati ya sitini na sabini katika sehemu za makazi za Mashariki mwa jiji la Nairobi kama vile mitaa ya: Kaloleni, Mbotela, Kimathi, Pumwani, Majengo,Bahati, Buruburu, Barma, Umoja, Dandora, Huruma, Mathare, Eastleigh na viunga vyake(Mbaabu na Nzunga, 2003). Kufikia miaka ya awali ya 1970,Sheng ilikuwa imepamba moto sio tu Nairobi bali pia katika miji mingine kotenchini Kenya. Kufikia sasa, Sheng imekuwa kitambulisho cha takriban vijana wote nchini, mijini na mashambani wawe wa shule au la.


Kwa mujibu wa Mukhebi (1986: 11), Sheng ni tukio la kitamaduni ambalo linafungamana sana na mawazo au fikira, hisia na matakwa ya watumiaji wake.Anaeleza kuwa wazungumzaji asilia wa Sheng waligundua kuwa kutokana na hali na mazingira yao ya kifukara katika mitaa ya jamii yenye mapato ya chini,wasingeweza kupata elimu yao na kuwasiliana kupitia Kiingereza bali
walihitaji mfumo wao wenyewe. Anaongezea kuwa kutokana na ufahamu wao duni wa kingereza Kiingereza, iliwawia vigumu vijana hao kuweza kujifunza masomo mseto kwa kingereza kama vile Historia, Jiografia, Fasihi na maisha ya kijamii ya waingereza,masomo yaliyokuwa ya kimsingi katika mitala ya shule za msingi wakati huo.

Kuna nadhariambalimbali zinazojaribu kueleza asili na chimbuko la Sheng. Hata hivyo,
nadharia kuu ni mbili; nadharia ya uhuni na nadharia ya msimbo wa vijana. Kwa mujibu wa nadharia ya uhuni, msimbo wa Sheng ulibuniwa na kuibuka kutokanana wahuni au wakora jijini Nairobi (Kobia, 2006). Waliunda baadhi ya manenokutoka nyuma kuelekea mbele badala ya muundo wa kawaida wa neno. Kwa mfano, neno kama ‘nyama’ lilibuniwa na kuwa ‘manya’. Nadharia inahusishakubuniwa kwa Sheng na haja ya wahuni kuwasiliana kwa ‘lugha’ ambayo watu wengine hawangeweza kuifahamu.
.
Kufuatia kupatikana kwa uhuru hapo mwaka wa 1963, idadi ya wakazi wa jiji la Nairobi ilipanda kwa haraka sana kutokana nakumiminika kwa watu kutoka mashambani wakitafuta nafasi za kazi katika mitaa ya viwanda humo jijini. Wananchi hao maskini waliishia kuishi katika
mitaa ya makazi duni ya viwandani mashariki mwa Nairobi ambapo ndio kitovu cha maendeleo ya viwanda. Ijapokuwa wafanyikazi hawa pamoja na jamii zao walilazimika kutumia Kiswahili kwa mawasiliano baina yao, wengi walikichukia Kiswahili kwa vile kilikuwa kimedunishwa sana na sera ya ukolonikama lugha ya mashambani, lugha ya vibarua au “maboi” wa kuwatumikiaWazungu.Hata hivyo, watoto wa wafanyakazi hao hawakupendelea kuendelea
kukitumia Kiswahili kama wazazi wao kwa sababu kadha. Kwanza kabisa,

kinyume na wazazi wao, watoto wale walilazimika kuishi katika hali ya jamii yautatu-lugha: lugha za kinyumbani, Kiswahili na Kiingereza. Pia, walitambua kuwa ingawa walibidika kutumia lugha nyingi, ni Kiingereza pekee ambachokilipewa hadhi ya juu kama lugha ya utawala, mamlaka, heshima na uwezo wa kiuchumi.Ili kuepuka matatizo ya kimawasiliano na kama njia ya kusuluhisha utata wa hali hiyo iliyowakabili, vijana hao waligundua msimbo wa mawasiliano kati yao ambao, ingawa ulifuata sarufi ya Kiswahili, uliazima msamiati kutokana na
lugha za kiasili na kuunda baadhi ya maneno yake. Msimbo huo ndio uliotokea
kuwa Sheng hapo baadaye.
Lugha hii ya kishengi imeanza kujitokeza katika nyimbo za wasanii Tanzani na hii inatokana kitendo cha kuingiliana kwa jamii,pia wasanii kushilikishana katika nyimbo zao na kupelekea baaadhi ya misamiati ambao ipo katika lugha hii ya kishengi ambayo ni lugha ya vijana kupelekea kusambaa kwa jamii yetu ya Tanzania ingawa lugha hii bado haitumiki sana na vijana wa kitanzania ambapo baadhi yao wamekuwa wa kiiga na baadhi ya wasanii wa Tanzania wanatumia lugha hii katika nyimbo zao.Data za utafiti huu zinaonyesha kuwa wasanii wengi wa nchini Kenya ndiyo wanatumia sana lugha hii ya kishengi mfano Jua kali,Nonini,Nameless na wasanii wengine mfano wa baadhi ya maneno ya kishengi yanayo tumika na vijana na jinsi yalivyo katika lugha ambazo wana kopa maneno hayo au kutohoa kama yalivyo na kubadili mtindo wa msamiati hiyo mfano:Mifano ya matumizi kama hayo ya Kiingereza yametolewa na Nnamonu(1995), ambaye amedai kuwa mengi ya matumizi kama hayo huwa ni makosa yasiyokusudiwa na yanayotokana na athari za lugha za kiasili za Kiafrika. Bila shaka, Sheng imekuwa ikilaumiwa na waalimu kuwa ndicho chanzo kikuu cha kuzorota kwa Kiingereza na Kiswahili sanifu nchini Kenya. Katika mifano hii,watumiaji hutamka dhana za Kiingereza kwa wingi ambazo kwa hakika hazina wingi: Mifano
Kiingereza                                                                                                       Kiswahili
accommodation(s)                                                                                           malazi
ammunition(s)                                                                                                  risasi
behaviour(s)                                                                                                    tabia / desturi
cutler(y|ies)                                                                                                     vyombo vya kulia
equipment(s)                                                                                                   vifaa
elite(s)                                                                                                             wasomi

Sheng                                                                                                  Kiswahili san ifu              
hitaji                                                                                                    mahitaji
oni                                                                                                       maoni
sumbuko                                                                                              masumbuko
jaribu                                                                                                  majaribu
lezi                                                                                                       malezi
Uundaji wa Nomino
Kama anavyosisitiza Ogechi (2005), uundaji wa maneno katika Sheng ni utaratibu changamano unaohusisha mbinu tofauti na kufuata hatua kadha.Akitumia mifano ya uundaji wa majina au nomino, vitenzi na vivumishi, Ogechianaonyesha kuwa leksia za Sheng hutokana na vianzo maalum katika Kiswahili,Kiingereza na lugha zingine za Kenya.Uundaji wa maneno katika msimbo wa Sheng hutumia njia mbalimbali.
Kuna matumizi ya ukopaji wa maneno kutoka lugha ya Kiswahili, Kiingereza nalugha nyingine za Kiafrika. Kuna pia kubuni kinasibu kwa maneno ya Sheng.Zifuatazo ni baadhi ya nomino zinazopatikana katika msimbo wa Sheng:
gichagi                                                                                    sehemu za mashambani
moti                                                                                                     gari
chapaa                                                                                                            pesa
manyakee                                                                                            wasichana
budaa,                                                                                                 mbuyu baba
kingoso                                                                                                Kiingereza
dem                                                                                                     msichana
Uundaji wa Vitenzi
Baadhi ya vitenzi huundwa kwa kuunganisha mwanzo kiambishi ku- na mzizi kwa kitenzi mkopo kutokana na lugha nyingine za Kenya au vitenzi vipya vyakubuniwa vilivyopewa kiambishi cha mwisho cha Kiswahili. Mifano:
ku-bonga                                                         kuzungumza
ku-ush                                                             kuondoka
ku-no                                                               kukasirika
(Kiingereza: “knock
Ufupishaji wa maneno
Katika msimbo wa Sheng, baadhi ya maneno ya Kiingereza yanayokopwa hufupishwa ili kuunda maneno mafupi. Maneno haya hujitokeza kama dokezo laneno kamili. Baadhi ya mifano ni kama vile:
tao                                                                                         mji (Kiingereza: “town”)
mat                                                                                         matatu
hao nyumba                                                                           (Kiingereza: “house”)
Swa                                                                                         Kiswahili, Swahili
Cole                                                                                         chuo (Kiingereza: “college”)
pero                                                                                          mzazi (Kiingereza: “parent”)
hasii                                                                                          bwana wa (Kiingereza: “husband”)
Matumizi ya Jazanda na Tasifida
Msimbo wa Sheng huunda baadhi ya maneno yake kwa kuzingatia mbinu ya
jazanda na tasifida. Kwa mfano:
boli                                                                                          mjammzito
mahewa                                                                                   muziki
kuro                                                                                         kahaba
pupuu                                                                                      kwenda haja kubwa
susuu                                                                                       kwenda haja
Hivyo kutokana na hii hali ya wasanii kutumia lugha hii katika muziki wa kizazi kipya unaonyesha kuwa vijana wengi wanatumia lugha hii katika utungaji wa mashairi yao ambayo ni lugha inayotumika na vijana wengi Kenya na hapa Tanzania miongoni mwa vijana  wengi.Utafiti unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya  una soko kubwa sana na ni ajira kwa vijana wengi wa Afrika mashariki na hii inaonyesha kuwa baadaye lugha hii itazagaa kwa vijana wengi kwasababu  kazi za wasanii wa Kenya pia zina sikilizwa na vijana wengi na wengi wao wanapenda ladha ya nyimbo za wasanii wa Kenya kutoka na misamiati wanayo itumia katika nyimbo zao,mfano katika nyimbo hizi mbili za wasanii wa Kenya,masanii Marya aliyemshilikisha mwanadada  mwenzie Avrill katika wimbo wa Tumekuja chokoza.
           
“Ai wewe mbona machali wanabehave hivi? tumeenda club lakini kunawanaume
Jamaa ajui kama napenda machali au mademu mimi nikiingia club nataka mabeste
Tujuane kwanza ,mimi na beste yangu tumekuja club kazi yetu sisi kuchokoza chali
Unipati after hii party ,tumekuja chokoza haaahaaa,usidhani kama utapata nafasi
Hahaaaaaa”
Wimbo mwingine ni wa msanii Bugz katika wimbo wake wa kamoja tu.
            Nina ubaya na mademu eeh,ah wamechili endelea kuchili ahopu
            Na hizo nywele  utatoa ukienda home kudai anang’owa ati
            Mambo ati mambo ni baada ya ndoa mimi mdogo sana siwezi oa
            Kausha weka mkono kwa koponi siunajua kutoa ni ngoi nikikuumiza basi sori
            Shiiiiii acha mastori mbona ucheki  mimi sisleki inaiva ila lakini haichomeki
            Njaasho kutoka kwa lips,chicks kwa hips”
Misamiati iliyotumika katika nyimbo hizi mbili zinaonyesha namna lugha hii ya vijana inavyotumika katika nyimbo zao na kuzidi kushika kasi katika matumizi ya lugha ya vijana nakupelekea wazee kushindwa kuelewa ujumbe unaotolewa na vijana na hivyo muziki huu kubaki kuwa mali ya vijana peke yao mfano msamiati mademu likiwa na maana ya wasichana,machali likimaanisha vijana,beste likiwa na maana ya rafiki,beshi pia likiwa na maana ya rafiki.
Hali inatokana na kitendo cha uigaji wa utamaduni miongoni mwa vijana wengi ambapo suala la kuiga utamaduni wa jamii nyingine ni pamoja na uwigo wa lugha,mavazi kwani hata mavazi ya vijana wengi kwa asilimia huwaiga wasanii jinsi wanavyo vaa mfano mashati yanayoitwa bushoke jina hilo lili tokana na sababu ya msanii huyo kuvaa shati hilo katika mojawapo ya video ya wimbo wake mmoja hivyo basi kuanzia hapo wakaanza kuyaita mashati hayo Bushoke,nj’e ya vijana kuiga mavazi pia hata matendo yanayoimbwa katika nyimbo hizo vijana hutilia mkazo kwa kuyatenda yale yanayoimbwa na wasanii hao.Mtafiti alimhoji kijana mmoja kwa jina alijitambulisha kwa jina la  Derick yeye alisema:
            “muziki wa kizazi kipya ni muziki ambao umeshika vijana wengi katika
            Kuusikiliza na hata ukienda club(kumbi za starehe/sehemu ya muziki)kwa
            Asilimia  kubwa utakutana na vijana wengi.misamiati wanayo itumia naielewa
             Vema kwa upande  wangu”
Kutokana na nyimbo hizi kugusa maisha ya vijana ndiyo sababu kubwa inayopelekea vijana wengi kuupenda muziki wa kizazi kipya .Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa muziki huu unaoimbwa na vijana wengi unagusa maisha yao waliyonayo mtaani.Nyimbo za muziki wa kizazi kipya zinagusa maisha ya vijana katika swala la maendeleo ya kijamii,siasa na uchumi.
Maendeleo ya kiuchumi,muziki wa kizazi kipya unawagusa vijana wengi katika upande wa uchumi,utafiti uliofanyika umegundua kuwa vijana wengi hawana ajira na ajira kubwa wanayo itegemea ni hiyo ajira binasfi ambayo kwa upande mkumbwa ndiyo vijana wengi wanaipenda ,kwa asilimia kubwa utafiti unaonyesha kuwa vijana wengi hata waliopo mashuleni wanajishughulisha na utungaji wa mashairi ya muziki huu wa kizazi kipya na kuimba katika matamasha mbalimbali na mashuleni wakijulikana kama wasanii wachanga(Underground)kwa wale ambao bado hawajavuma/hawajajulikana  katika soko la muziki huu wa kizazi kipya.
Nyimbo za muziki wa kizazi kipya zingine zinawataka vijana kupamba na maisha na si kuwa nyuma katika kupambana na maendeleo katika maisha yao mfano katika wimbo wa  fungeni mikanda ulioimbwa na wasanii wa Tanzania Chege na Temba wanasema:
            “Vujana fungeni mikanda,fungeni mikanda tukokilimani twapanda
fungeni mikanda”
katika wimbo huu wasanii hawa wanawataka vijana kuwa wastahimilifu na kujikaza ilikupambana na maisha yanayo wakabiri katika misuko suko iliyopo,kwa upande mwingine wasanii wanawahasa vijana na jamii kumshilikisha mungu katika swala la kutafuta maisha  kuwa ni muhimu kumshilikisha mungu ilikuweza kupambana na maisha yanayo wakabiri vijana wengi.
Kwa upande wa siasa ,vijana wengi sasa hivi wamejingiza na siasa,pia utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa vijana wengi wa sasa huwa wanapenda kuimba nyimbo za siasa ilikuweza kupata soko kipindi cha uchaguzi kwasababu wanasiasa wengi kipindi cha uchaguzi huwa wanachukua vijana kwa ajili ya kuwaimbia wanapo kuwa wanajinadi kwa wananchi ilikuweza kuchaguliwa na kwa asilimia kubwa vijana wengi hujitokeza katika viwanja vya mikutano na kushawishika kumsikiliza mgombeaji  na baadaye kuweza kuwa na moyo wa kupiga kula mfano mzuri ni pale Rais wetu wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipomtumia msanii Marow katika kutumbuiza kwenye kampeni yake na kupelekea vijana pamoja wananchi kwa ujumla kujitokeza kumpa heshima ya kumsikiliza na baadaye kumchagua,pia Mgombe mwingine aliyekuwa anagombea kwa Uraisi kwa tiketi ya Chadema  dakt.Wilbroad Silaa aliwatumia wasanii kama Danny msimamo,Mkoloni,G, Mapacha wa tatu.
Katika maendeleo ya jamii,muziki wa kizazi kipya unawagusa vijana,utafiti unaonyesha kwa sasa jamii imeanza kuona muziki huu sio wa kihuni kama hapo mwanzo ulivyokuwa unachukuliwa ,wazazi wa vijana wengi wanaona kuwa endapo  kijana ana uwezo wa kuimba basi haruhusiwe kuimba kwasababu ni mojawapo ya ajira ambayo kijana anaweza kujikwamua na kuondokana na makundi mabaya ya mtaani hivyo basi wazazi wengi sasa hivi hawa uchukuliii mziki huu kuwa ni wakihuni kama zamani,mzazi mmoja ambaye nilimuhoji kuhusiana na hilikuwa muziki wa kizazi kipya unagusaje? maisha ya kijana alijibu kama ifuatavyo:
            “Mimi kwa upande wangu kama mwanangu anaweza kuimba  sitoweza kumkataza
Zaidi nitajitahidi kumsaidia kimawazo na kumskiliza anchohitaji maana sasa hivi ukiangalia vijana wengi waliofanikiwa kutokana na vipaji vyao ni wengi na wana maisha
Mazuri wao na familia zao ,kwahiyo mimi nitafurahi sana kama mwanangu akiwa na kipaji cha kuimba,mimi naona sio uhuni kwakweli”
Maelezo ya mama huyu ambaye ni mfanyabiashara akijulikana kama mama vipodozi,yanadhihirisha  kuwa muziki wa kizazi kipya unawagusa vijana kwa kiwango kikubwa zaidi na walio wengi wamefanikiwa wakiwa na umri mdogo mfano msanii Alikiba,Marow,Dogo Janja na wengieneo.Sababu hizi zilizopatikana katika utafiti ndizo zionyeshazo kwanii vijana wanapenda muziki wa kizazi kipya zaidi kuliko nyimbo zingine.
4.4Mchango wa muziki wa kizazi kipya katika  utamaduni wa  lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.Data za utafiti huu zinaonyesha kuwa kuna mchango chanya na hasi wa muziki wa kizazi kipya  katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
Mchango chanya wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni  wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla,utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya unasaidia kutangaza utamaduni wetu kwa kupitia shoo wanazo zifanya nj’e ya nchi,wasanii hawa wanapo kwenda kufanya shoo n’je huko wanakutana na watanzania wenzao  na watu wa jamii ya nchi hiyo ambayo wanafanya shoo.Hivyo basi kupitia muziki wa kizazi kipya lugha ya Kiswahili inatangazwa na kupelekea kukua na kufahamika,Kutokana na utafiti uliofanyika kwa njia ya kuwahoji baadhi ya vijana katika mtandao wa kwa njia ya facebook walijibu hili swali baada ya kuwaulizwa swali kuwa muziki wa kizazi kipya unamchango gani katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla kama ifuatavyo:Msichana Subilaga Chalres alisema:
“Kwanza unaongeza maneno au misamiati,2 unafanya lugha ya kiswahili
itambulike kwa urahisi hata katika nchi nyingine thus pia mi naona kwamba mziki
 wa kisasa una batilisha utamaduni huo maana hata lugha wanaiichanganya, Pili
una saidia kwa kuendeleza lugha ya kiswahili kwa misamiati mipya na kutangaza utamaduni huo kwa nchi kadha maana mziki huo unasikizwa hadi uropa.pia pale wanapoenda kushiliki mashindano ya nje wanakuza lugha yetu inaweza kuwa
 point moja.

Pia kijana mwingine anayeitwa Daniel simon alisema kuwa:
“ muziki unamchango katika kueneza maneno na misemo mipya ya kiswahili.
..mfano neno sharobaro!cjui ndo mnaiita misimu me naona una faida hapo
 kwa sababu wasanii wa kizazi kipya wana tumia misamiati ambayo inatubidi
kutafuta maana yake”
kijana mwingine anayeitwa Asulikwe Mjaba yeye anasema kuwa:
“me naic unakuza utamadun we2,zen unaelmisha,unaburudsha”
Hivyo basi kutokana na utafiti huu muziki wa kizazi kipya unamchango mkubwa katika lugha ya Kiswahili kutokana na misamiati wanayo itumia  pia  kutokana  na misimu inayotumika kwa vijana sana na hata baadhi ya wazee mfano neno sharobaro kwa sasa ni neno lililosambaa sana miongoni mwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili,maana ya neno sharobaro linavyoeleweka na vijana wengi ni mtu msafi  na anaye jipenda.
Muziki wa kizazi kipya unachangia kukua kwa lugha ya Kiswahili na kuifanya lugha hii itambulike,kupitia muziki wa kizazi kipya na kujiongezea msamiati kwasababu kwa asilimia kubwa misamiati inayotumiwa na wasanii hawa katika nyimbo zao inatumiwa na jamii na maneno hayo yanapokuwa yamezoeleka katika jamii yanasanifishwa kisha kutumiwa  kama misamiati iliyosanifu.viilevile muziki wa kizazi kipya unadumisha mahusiano au kujenga ushirikiano kwa vijana  muziki huu unawakutanisha vijana pamoja pia kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuwasiliana kunasaidia kukuza utamaduni wa lugha ya Kiswahili.Utafiti unaonyesha kuwa wasanii wanao kuja kufanya shoo wakati mwingine huondoka na maneno ya Kiswahili na kuyaingiza katika nyimbo zao mfano  msanii  micheal Jackson ambaye ni marehemu alishawahi kuingiza maneno ya Kiswahili  katika wimbo wake ambazo:
                         “nakupenda pia nakutaka pia mpenzi wee”

Mtafiti alipata maelezo haya kutoka kwa kijana  Hassan Juma ambaye alisema:
                     muziki wa kizazi kipya unadumisha mahusiano kwa vijana kwa
                      Kupitia matamasha yanayofanywa na vijana katika shoo zao
                     Kupitia hapo tunakutana vijana tofauti tofauti na kufamiana zaidi”
Mchango hasi wa muziki wa kizazi kipya katika lugha ya Kiswahili kutokana na utafiti ulio fanyika niliweza kupata majibu ya fuatayo baada ya kuwahoji vijana kwa njia ya  mtandao wa facebook, na haya ni baadhi ya majibu waliyotoa :
       hauna mchango wowote kwa upande wangu, 7bu zimejaa swangilish kuliko
        kiswahili fasahaawell me nadhani una mchango kiburudani na sio kimaadili
      wala katika fasihi ya kiswahili,maana lugha wanazotumia saizingine hazina maadili
       yoyote katika jamii”hauna mchango wowote kwa upande wangu, sababu zimejaa   
      swangilish  kuliko kiswahili fasaha”
kutokana na utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa vijana wengi wanabadilika au kuwa kinyume na utamaduni wetu kimavazi,lugha wanayotumia,chakula na maadili kwa ujumla, kwamba wasanii wengi maudhui ya nyimbo zao kwa sasa umeegamia katika mapenzi zaidi hivyo kutokana na hili vijana wengi hujihusisha na mapenzi wakiwanaumri mdogo kutoka na nyimbo wanzo zisikiliza na kuona picha za nyimbo hizo ambazo nyingi ni za mapenzi na kwa upande wa  mavazi kwamba wasanii wengi wa kike mavazi yao hayasadifu kabisa utamaduni wetu kwani wengi wao huvaa nguo za ovyo ambazo zina valiwa na wasanii wa nj’e na kupelekea wao kuiga mavazi yao.
Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa vijana wengi huona ufahari kuvaa mavazi ambayo wasanii wana ya vaa bila na kusahau  kuwa huo si utamdauni wetu kwani mavazi wanayo vaa wasanii wengi  nj’e na utamduni wetu hafadhari wanaume wanapokuwa jukwaani wanavaa nguo za heshima ingawa wengine kuvaa ovyo mfano kuregeza suruali wanapokuwa wanafanya shoo zao.

Pia utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya unarudisha nyuma lugha ya Kiswahili kutokana na matumizi mabovu ya lugha inayotumika katika nyimbo hizo na kuu fanya lugha ya Kiswahili kuonekana ni ya wahuni kutokana na matumizi mabovu ya misamiati inayo  tumiwa na wasanii hawa katika nyimbo zao kama kuchanganya lugha  na utumiaji wa  lugha ya matusi.mfano katika wimbo ufuatao:
SURA YA TANO
5.0HITIMISHO NA MAPENDEKEZO.
Sura hii ndiyo ya mwisho katika utafiti huu ,kipengele hiki kinaelezea hitimisho la utafiti huu na mapendekezo kwa tafiti zijazo sura hii inabainisha mhutasari wa tasinifu hii .Sehemu ya pili sehemu ya inazungumzia mambo yaliuibuliwa na utafiti wangu na sehemu ya tatu  inapendekeza maoni kuhusiana na mambo mbalimbali niliyoyabaini kutokana na utafti wangu na sehemu ya mwisho inatoa mapendekezo kwa ajili ya tafiti zijazo kutokana na maeneo mbalimbali yaliyoguswa na utafiti huu.
5.1Muhtasari wa tasnifu.
Utafiti huu uliadhimia kuchunguza  nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.Nilifanikiwa kuhojiana na wasanii,wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma  pamoja na wakazi wa manisipaa ya Dodoma  mjini.Kwenye utafiti huu niliongozwa na malengo matatu ambayo ni Hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,sababu zinazo pelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana zaidi pamoja na kuonyesha mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
Tasinifu hii imekamilishwa na sura tano,Sura ya kwanza inaelezea tatizo la utafiti likiwa ni  Kuangalia nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya                         Imejumuisha usuli wa tatizo ,tamko la tatizo la utafiti,manufaa ya utafiti,nadhari ya utafiti na malengo ya utafiti,manufaa ya utafiti  na maswali ya utafiti.katika sura ya pili imefafanua maandiko mbalimbali  yanayozungumzia muziki wa kizazi kipya .Mapengo yaliyotumika katika mada  yamebainishwa na maandiko hayo.
Sura ya tatu imebainisha mbinu na vifaa vilivyotumika katika mchakato mzima wa utafiti wangu,vitu hivyo ni mpango wa utafiti,walengwa wa utafiti,jamii ya watafitiwa,eneo la utafiti,uchambuzi na uunganishaji wa data,zana na njia za kukusanya data pamoja na vikwazo mbalimbali nilivyokumbana navyo wakati wa mchakato wa ukusanyaji na uchambuzi wa data.
Sura ya nne imetoa matokeo ya utafiti uliofanyika .Mjadala  huu  umegawanyika katika sehemu tatu kulingana na maswali yaliyoongoza utafiti huu. Sehemu ya kwanza  hadhi  ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya inajadili.Katika sehemu ya pili nimeelezea sababu zinazopelekea vijana wengi kupenda kusikiliza muziki wa kizazi kipya zaidi.Sehemu ya tatu nimejadili mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya kiswahili.Mwisho nimetoa muhtasari kwa  kuelezea yote yaliyojadiliwa katika sura hii.
 Katika sura ya tano nimehitimisha kwa kutoa muhtasari wa utafiti kwa ujumla yakiwemo matokeo ya utafiti huu. Pia nimetoa mapendekezo kwa tafiti zijazo kuhusu mambo yanayofaa kuzingatiwa katika muziki wa kizazi kipya wanapotumia lugha ya kiswahili.

5.2 Mchango Mpya wa Utafiti Huu.
Ni matumaini yangu kuwa  kutokana  na utafiti uliyo fanyika utafiti huu utakuwa na mchango  mkubwa kwa jamii na kwa wizara ya  sanaa utamaduni na michezo pia kwa baraza la sanaa na wasanii wenyewe ambao ni chipukizi na waliofanikiwa katika muziki huu wa kizazi kipya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.Pia utaleta changamoto katika kuibua tafiti zingine.Kitokana na utafiti huu pia nimefanikiwa kuibua mambo ambayo ni chachu ya maendeleo ya muziki wa kizazi kipya kwa wapenzi wa muziki huu na hata wale wasio penda kusikikliza:
Katika utafiti huu nimefanikiwa kufafanua  kwa kina baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa vinawatatiza wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jinsi lugha ya kiswahili inavyotumika katika muziki wakizazi kipya .Nimafafanua kwa kina mambo yafuatayo:
Nimejadili hadhi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya kwa kuonyesha kuwa wasanii pamoja na taasisi za kiswahili zina changamoto kubwa  katika kuikuza lugha hii ya kiswahili  hivyo basi  wana muziki wanapaswa kuitumia lugha hii vizuri na kuipa hadhi au heshima yake katika kuitumia hili linaambatana na taasisi za lugha ya kiswahili kuweza kufanikisha soko la  muziki huu ambalo ndilo lengo la wasanii kuweza kupata soko la kazi zao kwasababu wasanii wengi wanapenda kuimba kwa kuchanganya lugha,lugha za matusi wanazo tumia na kuifanya lugha ya kiswahili kuwa na hadhi ya chini na hivyo kinyume na utamduni wetu kwamba lugha inaonekana ina  matusi, pia mchango wa utafiti huu ni kuitaka serikali kwa kushilikiana na taasisi za kiswahili kutilia mkazo utumizi wa lugha iliyo sanifu katika nyimbo zao ili kuikuza vema lugha hii ya kiswahili.
Katika kufafanua sababu za vijana kupenda kusikiliza muziki wakizazi kipya kuliko kundi lingine katika jamii inayotuzunguka,nimeweza kufafanua sababu hizo ambapo wasanii wanaweza kujirekebisha  ili sanaa yao iwe ya watu wote nasi vijana endapo wata badilisha lugha wanazo zitumia na kutumia lugha inayoeleweka na jamii nzima,kuacha kutumia lugha ya matusi pia lugha ya kisheng ambayo wasanii wa Tanzania wanaaza kuitumia ktika nyimbo zao na kupelekea muziki huu kuwa amali  vijana peke yao.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiitumia lugha ya kiswahili vema kutokana  na utafiti nilioufanya itasaidia kuondoa utabaka uliopo baina ya wasikilizaji wa  muziki huu wa kizazi kipya kwasababu utatoa fursa kwa rika zote kuupata ujumbe uliokusudiwa na wasanii hawa wa muziki huu.
Vilevile kitendo cha wasanii kuchanganya lugha,kutumia misamiati wanayoiibuwa wenyewe inasaidia katika kuongeza maneno au misamiati katika lugha ya kiswahili kutokana na  wasanii hawa kutohoa maneno toka katika lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya kiingereza  na lugha za asili.
Mwisho utafiti huu utoa ufafanuzi kwa wasanii kutumia lugha inayoeleweka ilikulinda utamaduni wa lugha yetu ya kiswahili na jamii kwa ujumla kutokana na hili utafiti huu unawataka wasanii kuilenga jamii nzima ili ujumbe ufike kama ulivyo kusudiwa kufika na si kwa kundi moja ambalo ni vijana kwamba kuna wazee pia wanao penda kusikiliza muziki huu wa kizazi kipya lakini wanapopata fursa ya kusikiliza wanapata tabu kuelewa misamiati inayotumiwa na wasanii hao.Utafiti huu unatoa mchango kwa kuwakumbusha wasanii wa muziki huu kuwa sanaa yao ni mali kwa jamii nzima .
Wale wasanii wanao chipukia sanaa hii ili waweze kufanya vema zaidi ya waliotangulia na wanapo pata mwanya wa kuenda kufanya  shoo zao nj’e ili waweze kuutangaza utamaduni wa lugha hii vizuri na kuendelea kuitangaza lugha hii ya kiswahili ndani na n’je ya nchi yetu.Pia wasanii wanapaswa kutambua kuwa muziki wao unatazamwa na kusikilizwa na  jamiii kwa ujumla hivyo basi kulinda utamaduni wa lugha yetu ni muhimu zaidi kwasababu  wanamuziki wengi huiga wasanii wa n’je kimiondoko,mavazi na hata mambo wanayo imba katika nyimbo zao pia yanasadifu hadhi ya nj’e na vijana wengi mambo yao mengi wanayo ya fanya huwa  wameyasikia katika nyimbo hizi za muziki wa kizazi kipya hivyo basi wasanii hawana budi kufuata sheria na taaratibu za utamaduni wetu.
Hivyo ufafanuzi huu wa kina utakuwa chachu kwa jamii ambayo ni wapenzi wa muziki wa kizazi kipya na wanaoipenda lugha hii ya kiswahili nj’e na ndani ya nchi.  Hii ni pamoja na jamiii iliyo kuwa ikiuchukulia kuwa muziki wa kizazi kipya ni wakihuni ili waweze kubadilisha mtazamo wao wa mawazo na kuweza kuusikiliza muziki huu wa kizazi kipya hasa wazee ambao huona muziki huu ni wakihuni.
5.3 Maoni Kuhusu Utafiti Huu.
Muziki wa kizazi kipya ni aina ya muziki ambao umekuwa ukibadilika siku hadi siku sio kama hapo mwanzo ambapo muziki huu ulikuwa chombo cha vijana kuelezea matatizo yao,.kwa sasa  jamii inaona muziki huu ni wakihuni kutokana na muziki huu unavyo wasilishwa kwa jamii na kuonekana ni wa vijana zaidi.Utafiti huu utauwa fikra na mitazamo ya wazee wengi ambao hawapendi kuusikiliza muziki huu wa kizazi kipya kwa kuwa wanauona ni muziki wa kihuni na una walenga vijana zaidi.
Maoni yangu kutokana na utafti nilioufanya kuhusu nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ninaona vema taasisi za lugha ya kiswahili zikishilikiana na baraza la sanaa na lugha kuweza kukaa na wasanii na kuongea nao kuhusiana na sanaa pamoja na lugha wanazo zitumia katika utungaji wa nyimbo zao  ikiwa ni pamoja na kuangalia swala la utumizi mzuri wa lugha ya kiswahili katika nyimbo zao.
Pia maoni yangu mengine ni kwa jamii inayo sikiliza muziki wa kizazi kipya hasa wazazi wanao waachia vijana wao ambao wana umri mdogo kusikiliza nyimbo hizi ambazo zingine zinachochea mapenzi na kuwaafanya vijana kuanza mapenzi wakiwa katika umri mdogo pia kuvaa mavazi ya ajabu kutokana na kuwaangalia picha za wasanii ambao huuvaa mavazi ya ajabu katika shoo zao.vilevile kwa wasanii ambao wana vaa nguo za ajabu mtaani ambazo ni kwa ajili  ya kufanyia shoo na wakati mavazi mengine yanakuwa hayasadifu utamaduni wetu na hivyo wasanii hawa kujidharirisha na kuwafanya vijana wengine kuiga mavazi yao.Pia wasanii wanapaswa kutumia lugha inayoeleweka na jamii yote na hii itawasaidia katika soko la kazi zao ikienda sambamba na ujumbe wanao utoa kwa jamii kwamba wasiegemee kwenye mapenzi zaidi kwasababu wasanii wengi nyimbo zao zimejaa dhamira ya mapenzi sana na hii ndiyo inayopelekea vijana wengi kujiangiza katika swala la ngono wakiwa katika umri mdogo.Endapo watazingatia hayo muziki wa kizazi kipya utakuwa ni mali ya jamii nzima na itakuza na kueneza lugha ya kiswahili vema nj’e na dani ya nchi.
5.4 Mapendekezo Kuhusu Tafiti Zijazo.
Napenda kupendekeza mambo yafuatayo kwa tafiti zijazo ambayo yatachangia maendeleo ya lugha ya kiswahili na muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
Kwa watafiti watakao jikita katika swala hili la lugha ya kiswahili pamoja muziki wa kizazi kipya ni vema wakaangalia  chanzo cha misamiati inayotumiwa na wasanii hawa katika muziki wa kizazi kipya kwasababu misamiati mingine inatoholewa katika lugha za asili na misamiati mingine ni maneno ya vijana ambayo yanafaahamika miongoni mwao tu na kupeleke muziki huu kuwa ni mali ya vijana peke yao.Hivyo itakuwa vema endapo watafiti wa kazi zijazo kutazama vema chanzo cha misamiati wanayoitumia katika nyimbo zao.
Pia natoa pendekezo kwa vyombo vinavyojihushisha na lugha ya kiswahili pamoja na sanaa kwa ujumla kutoa kipaombele kwa kazi za wasanii hawa kwasababu sanaa kwa upande mkubwa inatangaza taifa kuliko nyanja nyingine yeyote kwa njia ya shoo wanazo kwenda katika mataifa mengine.Hivyo basi watafiti watakao fanya utafiti wa kazi hii itawapasa kushirikiana na taasisi za lugha pamoja na wasanii kwa kushirikiana na serikali.
Pia naendelea kusisitiza kuwa msanii anapaswa kujitambua kuwa yeye ni kioo cha jamii na ni mtu muhimu sana kwa jamii.Hivyo basi wasanii hawana budi kuheshimu kazi zao,kujiheshimu wao wenyewe hii ina ambatana na mavazi ya wasanii wanyewe kuva katika shoo zao ,lugha inayotumiwa na wasanii katika nyimbo zao,mienendo ya wasanii katika maisha yao ya kila siku na mwisho kabisa msanii anapaswa kuzingatia ujumbe na kuwa mfano kwa jamii na vjina.
MAREJEO.                                                           
 Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981),TUKI,Dar-es-salam.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu  Toleo la pili(2005),TUKI,Dar-es-salam.
Mbaabu I. N. K( 2003).English-Kiswahili Dictionary of Sheng: Deciphering East Africa’sUnder-World Language. TUKI,Dar es Salaam:

Mkangi, K.( 1984).Sheng and the Kenyan Culture. The Standard, Nairobi, August 30
(17–18).
Mukhebi, L. (1986)..Is Language and Culture Inseparable? Kenya Times, Nairobi, May 28

Masamba D.P.B(2006),Jarida la Taasisi ya Uchunguzi  wa Kiswahili,Dar-es-salam.
Taji. L(2008),Chimbuko la Muziki wa kizazi kipya,Bongo celebrity,Dar-es-salam.
Wamitila K.W(2003),Kichocheo cha Fasihi simulizi na andishi,English press;Dar-es-salam.
Chachage ,C.S.L.(2002),Ndani ya Bongo utandawazi na migogoro ya utamaduni”Makala yaliwasilishwa katika mkutano wa kumi wa hali ya siasa Tanzania.Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Senkoro.F.E.M.K.(2003)Rethinking popular Arts and culture in the 21st century East Africa”Makala yaliyowasilishwa katika maadhimisho ya 30 ya codesria.
Majembe.A.K.(1998) “language use in Tanzania Hip Hop scene”,Un- published research paper, University of Dar es salaam.
Fenn,J na Perullo,A.(2000),language  choice and Hip Hop inTanzania katika popular music and society.University of Bowling Green City.
Fema,(2006),Bongo flava utambulisho au umaarufu,vol.16
www.google.com. Halhamisi,28/4,2010.
www.freemedia.co.tz/habar php? Halhamisi28/4/2010.
Nyongeza mbalimbali.
A.Picha za wasanii pamoja na picha za baadhi ya tamasha la muziki wa kizazi kipya.
Msanii Abdulazizi Aboubakari Chende a.k.a Dogo janja .


Msanii Danny Msimamo akiwa na Msanii mwenzie Adili katika tamasha la Burudani nyumbani lililoandaliwa na  Joseph Mbilinyi Mbunge wa jiji la Mbeya  katika viwanja vya nzomwe tarehe 9/7/2011.
 Wasanii wakiwa wanaimba katika juu kwa na huo ni umati wa vijana wakifuatilia tamsha hiloo
B.Maswali ya dodoso 
1.Je? Kuna utumizi mzuri  wa  maneno ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
a)Ndiyo.
b)Hapana.
2.Kama ni ndiyo taja maneno baadhi unayoyafahamu  yalitumika katika muziki wa kizazi kipya na yanafahamika vema na watu wa rika zote.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
3.Pia kama jibu ni hapana  tao sababu zinazo sababisha matumizi mabaya ya maneno ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
4.Je? Muziki wa kizazi kipya unamchango wowote katika lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa,na mawasiliano nchini Tanzania
5.kama ndiyo taja michango unayoifahamu na kama hapana toa sababu……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
6.Je? Muziki wa kizazi kipya(bongo flava)una mchango katika utamaduni  wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla( ndiyo   )
7. kama ni ndiyo toa sababu. ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
 8.Unafikiria nini chanzo cha muziki wa kizazi(bongo flava) kipya nchini Tanzania.
………………………………………………………………………………………………………......................................................................................................................................
9.Unafikiria ni rika gani hupendelea kusikiliza muziki  wa kizazi kipya?vijana(  ),wazee,au wote( ).unadhani ni kwanini rika hilo hupenda kusikiliza muziki wa kizazi kipya.


























2 comments:

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu