Ni
wazi kuwa wengi tunalitambua vazi hili
na miongoni mwetu tunapendelea kulivaa vazi hili. Suti huvaliwa na jinsia zote
mbili yaani wanawake na mwanaume, isipokuwa mwanaume hawezi kuvaa suti ya sketi
kama ilivyo kwa wanawake,ambao wana
uwanja mpana katika uchaguzi wa Suti. Vazi hili huvaliwa sana maofisini katika
Taasisi binafsi na za serikali,kwenye harusi,sherehe,mikutano, na mazingira
tofauti ambayo ni rasmi.Leo mpenzi msomaji wa safu hii Naomba tukumbushane baadhi
ya kanuni za vazi hili la suti ambazo zitakupa hadhi ndani ya vazi la suti kama
ifuatavyo:
1.
Epuka kuchomekea koti
2.
Epuka kutembea peku
3.
Usipende kuongea kwa sauti au kupiga
kelele wakati unazungumza
4.
Acha kula magengeni.
5.
Usipende kupanda Daladala,kuendesha
pikipiki au baskeli ukiwa umevaa suti
6.
Usivae kandambili au kubeba mfuko wa
plastiki(Lambo)
7.
Usivae soksi zilizo chanika na suti
8.
Usijisaidie uchochoroni (kuchimba dawa)
uwapo safarini.
9.
Epuka kupenga kamasi barabarani au
kutema mate hovyo
10. Acha
kuchekacheka hovyo
11. Epuka
kutafuna hovyo barabarani
12. Usitembee na pesa za sarafu mfukoni
13. Marufuku
kupiga mruzi
14. Marufuku
kutokwa na jasho hovyo,tembea na leso
15. Usipende
kukimbia ukiwa ndani ya vazi la suti
16. Marufuku
kuwa mbishi au kusababisha mjadala usio na maana
17. Usinywe pombe za kienyeji wala kukaa sehemu zenye
vilabu vya pombe za kienyeji
No comments:
Post a Comment