Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, December 30, 2016

Mitindo 40 ya Vitenge Itakayo endelea kushika chati Mwaka 2017

By On December 30, 2016

African Print Jacket,Unaweza kuvaa wakati wa baridi,Jacket kama hili unaweza kulivaa na kuachia vifungo wazi bila kufunga na ukawa na muonekano tofauti yani two in one. # Africanfashion # Fashionblogger

 

African Print Solo Jacket

African Print coat and Dress.Special for church or official wear.

Nimempenda huyu dada balaa,Ukijijulia mwili wako yaani lazima hupendeze tu,Kazi  kwao wanaosema mwili wangu siwezi kuvaa hivi au vile,pambana na hali yako.








 Kitenge Jumpsuit two in one,Unaweza kutoa hilo koti la juu na ukavaa location ya kawaida bila koti.













 Sara Issa ndani ya Makenzi,ni kitenge ambacho kinavaliwa kila mwaka hakipitwi na wakati hivyo hata mwaka 2017 bado kitakuwa katika chati wewe tu kuchagua mtindo bomba unaokufaa # fashionista.







Thursday, December 29, 2016

Mishono mikali ya skirt za Vitenge iliyobamba Mwaka 2016 #50

By On December 29, 2016
Maxi skirt katika muonekano wa kitenge ni mshono ambayo Mwaka 2016 hauja mtupa mwanamke ,kutoka na uwezo wa kumpendeza kila mtu bila kujali umbo lake.


Wanawake wanene,wembamba,warefu kwa wafupi mshono huu unawapendeza.Mbali na kumpendeza kila mtu mshono huu pia unamfanya mwanamke aonekane mwenye heshima zaidi.

Mtindo huu mwanamke huweza kwenda nao mahali popote { location} yoyote ikiwa hajaweka mpasua  mkubwa mbele ya skirt ama pembeni.Mshono huu kwa mtu mwenye tumbo unaweza kushona belt pana na mtu mwembamba anaweza kushona belt zote mbili aidha pana au nyembamba.

Nimejaribu kuonyesha baadhi ya picha za mtindo wa skirt hizi.Ni wazi kuwa mshono huu hautapitwa na wakati hata Mwaka 2017 utaendelea kushonwa na kuwapendeza wengi.





Modeling ni Kazi kama kazi Zingine ." Tidy Clever"

By On December 29, 2016

Sinyati blog ilifanikiwa kufanya interview na  Tidy Clever mwanamitindo anayejishughulisha na tasnia  hii ya modeling pia ni msanii wa kuigiza, ameigiza filamu mbili ya Chozi la binti kibena na Songa Mbele.Tidy aliweza kuzungumzia mambo mengi yaliyopo katika tasnia hii ya Modeling.Hivi ndivyo mahojiano yalivyokuwa:

 


JINA KAMILI: Abubakar Athuman

JINA LA KISANII:Tidy Clever

UMRI:23

KABILA:Msukuma

MAKAZI:Arusha.

 Tidy Clever anasema"

"Modeling ni kazi ambayo inanipa heshima,imenifanya kujulikana na watu  na wanatambua nichokifanya.hata kukutana na watu ambao sikutegemea kama ningeweza kukutana nao na kufanya nao kazi.Nimefanya kazi na designer Martn Kadinda,Ally Rehmtullah na kwa sasa nafanya kazi na kampuni ya modeling inaitwa Black fox.

Ni vizuri kama unafanya modeling pia uwe unajishughulisha na kazi zingine kwasababu kazi za modeling ni za msimu.Mimi binafsi nina kampuni yangu ya Filamu ipo maeneo ya Moshono-Arusha."


 CHANGAMOTO ZILIZOPO KATIKA TASNIA HII YA  MODELING NCHINI.

Changamoto zipo nyingi ila kubwa ni hizi:

  1. Malipo hafifu yasioendana na mkataba.Wakati mwingine unasaini mkataba wa kufanya kazi na mtu labda n'je ya mkoa,unapofika mfano alikuhaidi utafikia hotelini anakupeleka Guest na wakati mwingine hakupi malipo yako.

  2. Katika jamii ni kwamba modeling inaonekana  kama tasnia ya uhuni.kwamba mtu anayefanya modeling ni shoga,binafsi napenda kuiambia jamii kwamba sikweli ingawa hivyo vitu vipo. kitu cha msingi ni mtu kutambua anachofanya.

Vijana nawashauri kufanya kile kitu anachoweza kufanya na kutosubiri nyumbani ili kuweza kufanya.Vijana wajishughulishe.





 .

 

Designer anayetaka kufanya kazi na mimi kitu cha kwanza lazima aongee na Agency ninayofanya nayo kazi{Black Fox,ipo DSM}.Ila kama ni mimi nimemtafuta tunaongea na kuandikishana mkataba.

Tidy clever katika social Network utampata, facebook kwa jina  la Tidy Clever,Instagram& Twitter, tidyclevertz.Email,tidyclever@hotmail.com

 






30 Ideas of How to Reuse and Recycle Old Tires into fashionable way.

By On December 29, 2016
Ubunifu husaidia pia katika kuinua kitega uchumi na kumfanya mtu kutokuwa tegemezi.Mtindo wa kutumia vitu chakavu na kuwa kitu kipya na chenye msaada ni jambo la heri.Ni vema wakati mwingine katika mazingira tunayoishi kuangalia ni jambo gani ambalo mtu unaweza kufanya na ukaweza kusaidia jamii yako.Leo nitakuonyesha ambayo unaweza kubadilisha tairi la gari lililoharibika  kuwa katika mtindo wa kisasa na  kukufanya uweze kujipatia kipato.


Coffee table.

 Sebule yako unaweza ipamba kwa matairi kama hivyo yaliyonakshiwa tayari.



 Tairi pia unaweza kutengenezea kama makopo ya maua kwa kubuni mitindo tofauti ya kuvutia bustani yako.
 Hii meza ni maalumu kwa sehemu za makutano kama baa,hotelini na Pub.


Unaweza tumia ndoo kama hii ya tairi baa au pub kuhifadhia vitu vya baridi au kwa matumizi yako mengine.
 Hili ni zuri la tairi ambalo unaweza litumia mlangoni mwa Bafu lako.

 
 Hizo hapo juu ni hatua zinazoweza kukusaidia kutengeneza tairi lako na kulipa muonekano wa kipekee.


 

 VIFAA VYA KUTENGENEZEA MITINDO YA MATAIRI UTAKAYO.

  1. Old Tire
  2. 1/2″ Plywood (a 2’x4′ piece worked perfectly) (I actually used MDF, but plywood is better for outdoor use where it may get wet)
  3. Jig saw
  4. Drill
  5. Screws
  6. Furniture Feet 
  7. Sisal Rope (use about 250 ft)


Usisite kutoa maoni yako hapo chini.


    3 Bora Zangu

    Inayotazamwa Sana

    Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

    Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

    Watazamaji Wangu