Heri Ya Mwaka Mpya Wasomaji Wangu.Nawapenda sana.
Kwa kusema hayo nimeona vema kuwadokeza leo dondoo kidogo za kufanikisha mwaka 2017,Najua wapo ambao mwaka 2016 haukuwa mzuri kwao ingawa pia wapo walifanikiwa Mwaka huu wa 2017.Binafsi ni furaha yangu kuona kila mtu anafanikiwa basi leo hii nitasema njia chache zitakazo weza kutuvukisha Mwaka 2017 tukiwa na furaha na matarajio mengine makubwa zaidi.NJIA ZA KUKUFANIKISHA MWAKA 2017.
Kuwa na malengo:
Ili kuweza kupambana na hizi changamoto za maisha ni muhimu kila mtu kuwa na wazo na malengo,hata mtoto mdogo ana malengo ndiyo sababu wakati mwingine unapomuuliza unapenda kuwa nani ukiwa mkubwa ,atasema nataka kuwa daktari kwasababu hayo ndiyo malengo yake.Wewe mtu mzima lazima pia ujihoji hivi nina malengo gani mwaka 2017.Mtu asiye na malengo mwaka 2017 huyo hana akili au fikra zake zimekufa.Pia kataaa roho ya kushindwa,unaona kuwa mwaka 2016 huku fanikiwa basi hata mwaka 2017 hutafanikiwa ,hapana usifikirie hivyo maisha ni kupambana bila kuchoka,utafika hatupaswi kuchoka wala kukata tamaa katika haya maisha.Wakati wote tembea na wazo lako kichwani lipambanue utaanzia wapi,angalia changamoto za hicho kitu unachotaka kufanya,usikatishwe tamaa na mtu yeyote,jiamini sema naweza na nitafanya.
NAFSI YAKO ITAMANI KITU:
Mwanadamu ni roho yenye nafsi iliyokaa kwenye mwili.Nafsi ndiyo imebeba kila kitu cha mwanadamu,ndani ya nafsi ndipo kuna maamuzi mema na mabaya,kuna furaha,amani,upendo,chuki,hasira,utapeli na uongo.Endapo nafsi yako ikijaa mafanikio,ni lazima utafanikiwa.Nafsi yako ikitaka kitu ni lazima utakifanya,Nafsi yako isipotaka kufanya chochote uwezi kufanya chochote.Tuzilazimishe nafsi zetu zifanye kitu tutavuka Mwaka 2017 tukiwa washindi.KUWA NA JAMBO LA KUFANYA BILA KUSITA:
Ni vema kuepuka mawazo mgando au mawazo yasiyo na uamuzi sahihi ,utakuta mtu anania ya kufanya jambo lakini wakati huohuo anaogopa kufanya jambo hilo.Kwa mtindo huu si rahisi kufanikia .kama umeamua kujitosa wewe fanya jambo tusiwaze negative tujitahidi kupamabana na kutegemea matokeo hasi na chanya,kama hatuta jaribu tutawezaje.KUWA NA NIDHAMU.
Kitu chochote bila nidhamu hakitafanikiwa ndiyo sababu unaona ili kitu chochote kiende katika taasisi yoyote au ofisi lazima kuna sheria ambazo mtu akienda kinyume nazo basi kuna utaratibu ambao utafanyika juu yake.Ukitaka kufanikiwa ni lazima ujue kuiendesha serikali yako ya kichwa.mfano epuka mambo ambayo kwako hayana faida na ukiaangalia siku zote yanapunguza kipato chako na siyo kukiongoza,Acha starehe,matumizi ya pesa ya kitu kisichokuwa na ulazima.kubali kuteseka kwa mda ili hali ukijua unachokifanya kina faida mbele yako.
Watu wengi hatuwezi kuitesa milii yetu huenda wakati mwingine nafsi inahitaji kufanya jambo lakini Mwili unakuwa dhaifu na kukonyesha hali ya kushindwa.Wakati mwingine ni vema kufanya kwa uweza wa Mungu usitumie akili zako sana .
KUWA NA MBINU:
Lazima uwe na mbinu za kukufanikisha katika jambo unalotaka kulifanya,usikubali kushindwa,inaposhindikana mbinu moja,tafuta mbinu nyingine usichoke.Pia jitahidi kuwa karibu na watu waliofanikiwa katika jambo unalotaka kufanya au wanauwezo hata wa kukushauri hata kama hawafanyi jambo hilo.Hapa ni vema ukitafuta watu wenye hekima kwani siyo kila mtu anapenda mtu mwingine afanikiweKUWA NA BIDII:
Ni vema ukafanya kazi kwa bidii kadri ya uwezo wako bila kujali kama kuna kesho,Watu wengi tunaona walifanikiwa ni kwasababu ya bidii walizonazo katika kazi zao.Mithali 10:4.KUWA NA RATIBA YA KAZI ZAKO:
Ni vema pia katika diary yako ukapanga ratiba ya kazi zako kwa kila siku kila mwezi,Ili uweze kujua mpaka mwaka unapoisha utakuwa umefanya nini,na wapi ulishindwa kutimiza majukumu yako.Sisi watanzania suala la ratiba kwa kweli wengi wetu si utamaduni .Ratiba wengine tumezoea kuziona katika ofisi zetu.Calenda ya mwaka mzima kazini ipo lakini wewe mtu binafsi huna, mimi naona ni vema kujifunza mambo yenye faida kwetu,kama ulikuwa bado jifunze sasa.FANYA MAOMBI.
Tambua kuwa maombi ni silaha yetu kuu wote kwa imani yako.Jitahidi kuzikabidhi mbele za Mungu kazi zako za kila mwezi,kila kazi unayotarajia kuifanya hakikisha unaiombea kabla ya kuanza,tegua kila roho za vikwamizi ili kazi yako iwe na upenyo.Fanya hivyo mwaka mzima na utaona matunda ya kumtegemea Mungu katika kazi zako.Mwisho mpenzi msomaji ningependa kuwaomba kutoa maoni yako unaposoma makala zangu,napenda kufahamu kama nilichokizungumza kimekusaidia au wapi nimekosea, usisite kucomment.Endelea kufuatilia makala zangu kadri ya uwezavyo ukibarikiwa share pia.Pia na karibisha mtu mwenye kazi za kiasili anazofanya kwa mikono yake,naweza kuweka makala yake kwa faida yako na watazamaji pia,nitumie kwa email yangu, abnerytupokigwe@gmail.com au ni text whatsapp kupitia namba 0756377940,mwisho saa 12 jioni.Karibu.
No comments:
Post a Comment