Mito ni Pambo katika kitanda chako pia ni kitu ambacho wengine hupenda kuikumbatia hasa wakati wa baridi huleta joto.{si kwa watu wote} |
Fahamu kuwa hamna sehemu iliyo na maana sana katika maisha yetu kama chumbani au sehemu ya kulala.
Sehemu hii inapaswa kuwa tulivu, safi na yenye vitu vichache, Unapoweka vitu vichache ndani ya chumba chako utakifanya kiwe na hewa nzuri nzuri zaidi.
Chumbani ni mahali ambapo unaweza kupumzisha ubongo wako na kufikiria mikakati ya
kimaendeleo na ukaweza kupata wazo jipya lakini yote hayo utayapata
endapo chumba chako kitakuwa kisafi, tulivu pamoja hewa nzuri.
Zifuatazo ni dondoo za upambaji wa chumba:
Mwanga
Chumba kinapopata mwanga wakutosha huvutia zaidi na kuwa na hewa ya kutosha.
Ninapo
zungumzia mwanga nina maanisha mwanga kutoka dirishani, mwanga wa taa
za chumbani ambazo uwekaji wake upo tafauti kulingana na uwezo ulio nao,
kuna taa ambazo huwekwa chini, ukutani au zile ambazo huwa pembezoni
mwa kitanda. Mwanga wa taa ya chumbani hupaswa kuwa hafifu.
Rangi.
Katika
uchaguzi wa rangi ni pamoja na rangi ya ukuta wa chumba chako, mapazia,
shuka, pamoja na rangi za mito. Hapa inategemea unapendelea rangi gani
lakini unashauriwa rangi za chumbani ziwe rangi ambazo ni tulivu.
Sehemu
ya joto utatakiwa kuweka mapazia ambayo sio mazito, katika hali ya
baridi tumia mapazia mazito pia ni muhimu kuzingatia rangi, usipendelee
rangi zitakazofanya chumba chako kuwa giza.
Pendelea mashuka yenye rangi moja au yenye maua machache. unapaswa kutumia rangi ambazo huonyesha usafi mfano rangi nyeupe.
Unaweza
kuchanganya na rangi zingine katika mito yako ya kitandani.Ubunifu
katika utandikaji wa kitanda chako ni muhimu ili kiweze kukuvutia muda
wote.
Sakafu
Kuna watu wanaopenda kutumia Mazulia (carpets) chumbani. Jaribu kuchagua
rangi nzuri aidha inayoendana na ukuta wako wa chumbani, ilikuleta
muonekano mzuri pia unashauriwa kapeti lisiingie chini ya kitanda ili
kukupa urahisi wakati wa kufanya usafi.
Ni
muhimu kusafisha zulia lako ili kuondoa vumbi na kuepuka kupata mafua.
Pia ni vema kuwa na tabia ya kulitoa maramoja moja ili kuweza kusafisha
sakafu yako na kuondoa harufu ya unyevunyevu uliopo chini ya zulia.
Mwisho zingatia kuweka vitu vichache chumbani na kuwa na mpangilio mzuri wa vitu ndani ya chumba chako.
No comments:
Post a Comment