KANDAMA MALUNDE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA WANAHABARI SHINYANGA
By
SINYATIBLOG
On
July 25, 2015
In
Maisha
Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugezi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia) |
Kadama Malunde Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
CHAMA
cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC)
jana Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi
watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo
ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa
chama hicho.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi
wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila
alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea
wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.
Kadama
Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na
Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha
Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).
Nkulila
aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen
Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu
Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella
Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.
Baada
ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo,
kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake
kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na
mabadiliko katika klabu hiyo.
Akizungumza mara
baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru
wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao
kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na
kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila
mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.
Kwa
upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka
viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano
waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku
wakizingatia maadili ya wanahabari.