Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, July 25, 2015

KANDAMA MALUNDE ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI MPYA WA WANAHABARI SHINYANGA

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo.
Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugezi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia)

Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club).                                                                                                                                                                                       
Kadama Malunde Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC) jana Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.

Kadama Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN).

Nkulila aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.

Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo, kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika klabu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.

Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku wakizingatia maadili ya wanahabari.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu