Vazi la Ubunifu kwa kutumia Ungo#Makeke
By
SINYATIBLOG
On
April 18, 2018
In
Mitindo
Baada ya uzoefu mkubwa katika matumizi ya mapishi jikoni, ungo umejizolea umaarufu mkubwa baada ya kuingizwa rasmi katika tasnia ya sanaa hususani katika ubunifu wa mavazi na kupewa jina la *LUPAHERO* na Jo;cktan Makeke.
*MAANA YA LUPAHERO*
Ubunifu huu wa mavazi umepewa jina la *LUPAHERO* ambalo ni mchanganyiko wa majina mawili ambayo ni *LUPAPIKE*, neno la *kinyakyusa* lenye maana ya ungo na neno la pili ni *LUHELO*, ambalo ni neno la kihehe lenye maana ya ungo.
Muunganiko wa maneno haya mawili umelenga kuleta dhana ya ushujaa kutokana na ladha ya mavazi hayo kuwa na dhima hiyo, huku neno Luhelo likitamkwa herufi za mwisho kama Hero, herufi *L* ikibadilishwa kuwa *R* ili kupata neno *hero* la kingereza lenye maana ya shujaa na kukamilisha maana halisi ya ubunifu huo kuwa shujaa wa ungo.