Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, June 13, 2013

Pelvic Exercises(Mazoezi ya misuli ya Uzazi)

Mazoezi ya Mama mjamzito,mwanamke unayependa pia kufanya zoezi la PC,
Image:www.mutusystem.com

Image:www.positivehealth.com


Kila mwanamke anapaswa kufanya mazoezi ya PC kwasababu husaidia kwa namna mbili;-
1. Humsaidia mume na mke kufurahia mapenzi zaidi
2. Hufanya uzazi wa mtoto kuwa salama zaidi kwa upande wa mama na mtoto vile vile

Msuli unaotawala uke wa mwanamke na kibofu chake cha mkojo huitwa “msuli wa PC”. Msuli huu ni muhimu sana. Kama mwanamke ana msuli imara wa PC, uke wake utaweza kuubana sawasawa uume wa mumewe. Jambo hili litamsaidia mke kujisikia raha wakati wa kufanya mapenzi.

Lakini kama msuli wake wa PC ni dhaifu, uke wake utakuwa mkubwa mno, na hivyo kushindwa kupata msisimko wakati wa kufanya mapenzi. Wanawake wengi wana misuli ya PC iliyodhaifu, kwa nini? Kwasababu hawajui namna ya kufanya mazoezi. Hata kama mwanamke ataambiwa “msuli unaozunguka uke unahitaji kufanyiwa mazoezi”; anaweza asijue namna ya kufanya mazoezi hayo.

Kwa mfano, wakati Martha alipojaribu kufanya mazoezi ya msuli wa PC, alifanya makosa ya kubana msuli ambao haukuwa wenyewe. Badala yake alibana msuli wa paja. Kwa bahati nzuri kuna njia ya mwanamke kutambua tofauti kati ya msuli wa PC na misuli ya paja. Msuli wa PC hukaza uke na vile vile huzuia mkojo kutoka. Hivyo mwanamke anaweza kujifunza kwa urahisi namna ya kubana msuli wake wa PC kwa kufanya mazoezi ya kubana anapokuwa anakojoa kama ifuatavyo:-
  • Akiwa anakojoa, hupanua magoti yake na kisha atazuia mkojo kwa muda wa sekunde chache. Baada ya hapo ataendelea hivyo kufanya hivyo kufunga na kufungua hadi kibofu chake kiishe mkojo.Kila anapofunga mkojo usitoke anabana msuli wake wa PC, kwasababu wakati magoti yake yamepanuliwa msuli ambao unaweza kufunga mkojo ni msuli wa PC peke yake. Lakini kama magoti yake yatakuwa pamoja anaweza kuzuia mkojo kwa kutumia misuli ya paja.

Kadri mwanamke anavyofanya mazoezi ya kuzuia mkojo kutoka, atajifunza kutambua tofauti iliyopo kati ya msuli wa PC na misuli ya paja. Wakati atakapokuwa na uhakika amejua namna ya kubana msuli wake wa PC, anaweza kuwa anaubana msuli huo saa yoyote apendayo, siyo wakati wa kukojoa tu. Na hapo ndipo atakapoanza kufanya mazoezi ya PC.

Kila mwanamke anapaswa kufanya mazoezi ya aina hii si chini ya mara 40 kwa siku. Hii ina maana mara 40 kila mchana, kubana kwa sekunde tatu na kulegeza kwa sekunde tatu. Siyo vigumu kufanya mazoezi mara 40 kwa siku.

Kwa mfano mwanamke kila asubuhi anaweza kufanya mazoezi mara 5 kabla ya kuamka kitandani (kwa kuwa kila zoezi huchukua sekune sita tu, anaweza kufanya mazoezi 5 katika nusu saa). Baada ya hapo anaweza kufanya mazoezi mengine zaidi wakati akingojea basi katika kituo cha basi (hakuna atakayeona kuwa unabana msuli wako wa PC). Kwa kufanya mazoezi kidogo kidogo kila wakati, atajikuta amaefanya mazoezi 40 kwa siku, kwa urahisi.

Dorothy, alikuwa na ugumu kukumbuka kufanya mazoezi haya ya PC, hivyo aliandika vijikaratasi na kuvibandika sehemu mbalimbali nyumbani. Kila kijikaratasi kilisema “mazoezi”. Alibandika kijikaratasi kimoja karibu na karo lakuoshea vyombo jikoni, kingine karibu na meza ya kunyooshea nguo n.k. Siku moja dada yake aliviona vijikaratasi hivyo na alitaka kujua ni vya nini. Ilimbidi Dorothy amweleze dada yake yote kuhusu mazoezi ya PC. Baada ya miezi miwili kupita, dada yake alirudi tena na kusema “mume wangu anafurahi sana kwa jinsi ninavyoanza kustareheshwa na mapenzi ya kimwili siku hizi. Anataka kujua dawa ya aina gani uliyonipa!”

Kwanini mazoezi ya PC huongeza starehe ya kufanya mapenzi?
Kwasababu mwanamke mwenye msuli wa PC imara anaweza kuubana uume wa mumewe wakati wa kufanya mapenzi, na hii hufanya mapenzi yawe matamu zaidi kwa wote wawili.

Siku hizi watu wengi hununua madawa ghali ambayo yanapaswa kuongeza utamu wa kufanya mapenzi. Ni wazi hakuna dawa kama hiyo ambayo hufanya kazi vizuri sana (kubana msuli wa PC). Lakini mazoezi ya PC humsaidia kila mwanamke anayefanya mazoezi, nah ii ndiyo dawa tena ya bure!

Kumbuka pamoja kufanya mazoezi vile vile pamoja kuongeza utamu wa wa kufanya mapenzi, mazoezi ya PC husaidia uzazi wa mtoto kuwa salama zaidi.

TUNAPENDEKEZA MAZOEZI YA PC KWA KILA MWANAMKE!!!!!

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu