Uchaguzi mbaya wa vyombo vya ndani.
Mojawapo la kosa kubwa ambalo watu hufanya ni uchaguzi mbaya wa vitu kama sofa,viti au kabati sina maana kwamba urefu ufanane,kinachotakiwa hapa ni kuangalia uwiano ulipo baina ya viti na sofa kuwe kuna mfanano kiasi sio kwamba kiti kifanane urefu na sofa ,zingatia mtindo,rangi,pia kabla ujanunua sofa zako angalia kwanza ukubwa wa sebule yako,kwasababu unaweza kununua sofa kubwa na ukaziweka nyumbani kwako na kufanya sebule yako kuwa ndogo na kupelekea usumbufu wakati wa kupita, jua kuwa sheria ya sebule inatakiwa kupangilia vitu vyako ili usimsumbue mtu wakati wa kupita.Hivyo basi sebule inatakiwa iwe na uwazi mkubwa.Uwekaji wa vitu vyote unavyovipenda sebuleni.
Kuna vitu ambavyo huwa tunakosea katika upangaji wa vitu tulivyonavyo katika nyumba zetu,leo katika safu hii mpenzi msomaji nataka utambue kitu na uweze kujirekebisha pale ambapo nitakuwa nimekugusa.Njia zifuatazo zitakuongoza na kukupa mwanga namna ambavyo unapaswa kupanga chumba chako, kutokana na makosa nitakayo yataja hapa chini..Jaribu kuweka vitu vichache ambavyo ni vya muhimu kuwepo sebuleni,ili uweze kuepuka mpangilio mbaya wa vitu ambavyo huna matumizi navyo katika eneo hilo,Ni wazi kuwa huwezi kuweka flemu( photo flame)zote za picha unazo zipenda ukutani,maua au vitambaa katika sebule yako,ikiwa una nyumba kubwa jitahidi kupangilia nyumba yako na kila eneo ifanye kazi yake.
No comments:
Post a Comment