Beyoncé na Jay Z ni wazazi wa binti Blue Ivy mwenye umri wa miaka mitano sasa tangu wafunge ndoa mwaka 2008.Ambapo kwa sasa familia hii inatarajia kupata watoto mapacha habari zilizosambaa baada ya Beyonce kupost picha za utupu akionesha ujauzito wake na kuonesha kuwa na furaha kubwa juu ya hilo amesema katika ukurasa wake wa instagram"
"We would like to share our love and happiness. We have been blessed two
times over. We are incredibly grateful that our family will be growing
by two, and we thank you for your well wishes. - The Carters"
Angalizo tu wabongo kwa kuiga hamkawii kupiga hivyo na kutupia mitandaoni ni vema mkazingatia utamaduni wetu pamoja na mila na desturi zetu uzingu tuwaachie wazungu.
Siku ya wapendanao ni siku ya kila mtu kuonyesha shukrani zetu kwa watu
tunaowapenda na walio karibu na maisha yetu kwa njia moja au
nyingine.Watu hao wanaweza kuwa
mama,baba,dada,kaka,mpenzi,mchumba,mke,mume,ndugu,marafiki,wafanyakazi
wenzako pamoja na majirani .Kwa nini? watu wengi huifanya siku hii
maalumu kila mwaka na kuangaika kutafuta nguo ya kuvaa siku hiyo na
kuchagua rangi nyekundu pamoja na zawadi.
Mpenzi msomaji wa safu hii napenda ujue kuwa mwezi huu ni mwezi wa
kuonyesha upendo na kuwa karibu zaidi na watu tunao wapenda pamoja na
kuwakumbuka hata ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki.Nimeona vema
tukikumbushana baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia hasa katika suala
zima la uvaaji.Zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia kufanikisha siku
hii ya wapendanao.
Chagua rangi sahihi ya nguo
Njia ya kwanza iliyo rahisi na itakayo kufanya upendeze siku hii ya
wapendanao ni kuepuka kuvaa vitu vingi vyenye rangi nyekundu.Sio lazima
kila mtu avae nguo yenye rangi nyekundu kama tulivyozoea.Rangi hii
nyekundu ni vema ukiitumia kama kikorombwezo(Accesories) katika mavazi
yako,hakikisha huchanganyi rangi vibaya kwasababu mtu mwingine anaweza
akavaa kijani na nyekundu na kumfanya aonekane kama mti wa krismasi.
Hakuna kitu kibaya kama kupendeza kupita kiasi mpaka unaharibu muonekano
wako.Vaa kawaida na utavutia sana, ikiwa una mtoko hahikisha unavaa
kawaida mfano unakwenda pikiniki, sinema au kupata chakula cha
mchana,jioni na marafiki zako.Wanawake wanaweza kuvaa jinsi au suruali
ya kawaida,gauni na blauzi(top)yenye rangi ya krimu,nyekundu au
pinki,Upande wa wanaume wanaweza kuvaa jinsi au suruali ya kitambaa
kulingana na mazingira anayo kwenda na shati au tisheti rangi ya
pinki,nyekundu au krimu.
Ifanye siku hii ya upendo
Endapo wewe na na mpenzi wako mnataka kuifanya siku hii kuwa ya
furaha(romantic date) kwenu na mmepanga kwenda sehemu tulivu mnayoipenda
au katika kumbi za starehe(club) ni vema ukivaa vizuri huku
ukihakikisha vazi utakalo vaa linakupa uhuru katika mtoko wako.Jaribu
kuvaa gauni jeusi na mkanda mwekundu,oanisha na heleni zenye rangi
nyekundu na kiatu cheusi au pia waweza kuvaa gauni nyeupe na skafu
nyenye rangi ya pinki bila kusahau kuonanisha na
heleni,bangili,mkufu,pochi,viatu kwa kuzichanganya rangi hizi tatu
ambazo ni pinki,nyekundu,na krimu.Jitahidi kutumia rangi mbili vizuri
ili isiwe kachumbari sana.
Pia unaweza kuvaa pinki na rangi nyekundu rangi hizi pia huenda
pamoja.Wanaume wanopenda kuvutia na kuwavutia wenzi wao siku hii ya
wapendanao ni vema wakichanganya vema rangi hizo tatu katika mavazi yao
mfano unaweza kuweka kitambaa chekundu katika mfuko wa shati au koti la
suti ulilovaa au kwa wale wanao vaa saspenda wana weza kutumia mikanda
yenye rangi nyekundu ilikuongeza nakshi, vilevile sio mbaya kama ukivaa
soksi nyekundu ni wazi kuwa haziwezi kuonekana,au tai nyekundu kwa wale
wanao vaa tai.Wanaume ni vema mkizingatia mazingira ya mtoko wenu bila
kusahau kuangalia mwezi wako kavaaje? ilimsipishane sana.Mbali na hayo
unaweza kuvaa vazi ambalo mwenzi wako siku zote hupenda wewe uvae ila
usihau kuchanganya japo moja ya rangi hizi tatu pinki,nyekundu na krimu.
Panga chumba chako
Samahani hapa naomba tukumbushane kidogo kuwa siku hii ni siku ya
tofauti.Jaribu kukibadilisha chumba chako na kukipa muonekano wa tofauti
kwa mwenzi wako jitahidi kuwa mbunifu kwa kuweka nakshi mbalimbali ili
kukifanya chumba chako kuwa katika hali ya upendo zaidi (romantic
place)siwezi kuzungumzia sana ila unajua nini cha kufanya kwa mwezi
wako.Tukumbuke kuwa sivema vazi la kulalia liwe pajama au gauni jepesi
refu/fupi kama tulivyozoea jaribu kuvaa kitu cha tofauti kwaajili ya
siku hii ni kiwa na maana kuwa unaweza kuvaa kitu cha tofauti ambacho
kila mmoja wenu ajazoeleka na mwenzi wake kuvaa.
Zawadi
Katika siku ya wapendanao ni vema pia ukawa na zawadi mfano sadaka ya shukrani kwa ajili ya upendo wa Mungu katika maisha yako,zawadi ya familia na marafiki,zawadi ya wazazi hata ya mwenza wako au mkeo.
Arusha Yasimama Kwenye Maombi: Miaka 63 ya Uhuru
-
Viongozi wa dini ,mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda na wananchi
wakiendelea na maombi katika matembezi ya kuombea mkoa wa Arusha na
maathimisho ya mi...
Cara Terbaik Untuk Menang Judi Sicbo Online
-
Bergabung dalam permainan judi sicbo online yang dapat dimainkan melalui
smartphone, maka tentu saja para pemain bisa melakukan sejumlah taruhan
dengan nya...
BANC ABC YAANZISHA HUDUMA MPYA KWA WATEJA WAKE
-
* Meneja wa Banc ABC Magabe Nyambuche akizungumza na waandishi wa habari
jijini Arusha*
Na Pamela Mollel,Arusha
Banc ABC katika kuwajali wateja wake wa ...