Vazi la siku ya wapendanao
Siku ya wapendanao ni siku ya kila mtu kuonyesha shukrani zetu kwa watu tunaowapenda na walio karibu na maisha yetu kwa njia moja au nyingine.Watu hao wanaweza kuwa mama,baba,dada,kaka,mpenzi,mchumba,mke,mume,ndugu,marafiki,wafanyakazi wenzako pamoja na majirani .Kwa nini? watu wengi huifanya siku hii maalumu kila mwaka na kuangaika kutafuta nguo ya kuvaa siku hiyo na kuchagua rangi nyekundu pamoja na zawadi.Mpenzi msomaji wa safu hii napenda ujue kuwa mwezi huu ni mwezi wa kuonyesha upendo na kuwa karibu zaidi na watu tunao wapenda pamoja na kuwakumbuka hata ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki.Nimeona vema tukikumbushana baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia hasa katika suala zima la uvaaji.Zifuatazo ni njia ambazo zitakusaidia kufanikisha siku hii ya wapendanao.
Chagua rangi sahihi ya nguo
Njia ya kwanza iliyo rahisi na itakayo kufanya upendeze siku hii ya wapendanao ni kuepuka kuvaa vitu vingi vyenye rangi nyekundu.Sio lazima kila mtu avae nguo yenye rangi nyekundu kama tulivyozoea.Rangi hii nyekundu ni vema ukiitumia kama kikorombwezo(Accesories) katika mavazi yako,hakikisha huchanganyi rangi vibaya kwasababu mtu mwingine anaweza akavaa kijani na nyekundu na kumfanya aonekane kama mti wa krismasi.Hakuna kitu kibaya kama kupendeza kupita kiasi mpaka unaharibu muonekano wako.Vaa kawaida na utavutia sana, ikiwa una mtoko hahikisha unavaa kawaida mfano unakwenda pikiniki, sinema au kupata chakula cha mchana,jioni na marafiki zako.Wanawake wanaweza kuvaa jinsi au suruali ya kawaida,gauni na blauzi(top)yenye rangi ya krimu,nyekundu au pinki,Upande wa wanaume wanaweza kuvaa jinsi au suruali ya kitambaa kulingana na mazingira anayo kwenda na shati au tisheti rangi ya pinki,nyekundu au krimu.
Ifanye siku hii ya upendo
Endapo wewe na na mpenzi wako mnataka kuifanya siku hii kuwa ya furaha(romantic date) kwenu na mmepanga kwenda sehemu tulivu mnayoipenda au katika kumbi za starehe(club) ni vema ukivaa vizuri huku ukihakikisha vazi utakalo vaa linakupa uhuru katika mtoko wako.Jaribu kuvaa gauni jeusi na mkanda mwekundu,oanisha na heleni zenye rangi nyekundu na kiatu cheusi au pia waweza kuvaa gauni nyeupe na skafu nyenye rangi ya pinki bila kusahau kuonanisha na heleni,bangili,mkufu,pochi,viatu kwa kuzichanganya rangi hizi tatu ambazo ni pinki,nyekundu,na krimu.Jitahidi kutumia rangi mbili vizuri ili isiwe kachumbari sana.Pia unaweza kuvaa pinki na rangi nyekundu rangi hizi pia huenda pamoja.Wanaume wanopenda kuvutia na kuwavutia wenzi wao siku hii ya wapendanao ni vema wakichanganya vema rangi hizo tatu katika mavazi yao mfano unaweza kuweka kitambaa chekundu katika mfuko wa shati au koti la suti ulilovaa au kwa wale wanao vaa saspenda wana weza kutumia mikanda yenye rangi nyekundu ilikuongeza nakshi, vilevile sio mbaya kama ukivaa soksi nyekundu ni wazi kuwa haziwezi kuonekana,au tai nyekundu kwa wale wanao vaa tai.Wanaume ni vema mkizingatia mazingira ya mtoko wenu bila kusahau kuangalia mwezi wako kavaaje? ilimsipishane sana.Mbali na hayo unaweza kuvaa vazi ambalo mwenzi wako siku zote hupenda wewe uvae ila usihau kuchanganya japo moja ya rangi hizi tatu pinki,nyekundu na krimu.
No comments:
Post a Comment