Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, October 21, 2017

Ijue Asili Na Namna Ya Kuvaa Pajama(pjs)#pajamas

Mpenzi msomaji  Wa  makala  zangu  Za mavazi,leo  napenda  ujue  asili  ya  vazi  hili  la  pajama ambalo  kwa  sasa  kutokana na   mwanadada  Zari  kulivaa , limeshika  mashiko  sana  Tanzania kwa  wapenda  fasheni .japo  kuna  watu  walimnanga alipovaa  kwa  kutojua  ni  vazi  lilioanza  kuvaliwa  tangu  mwaka 2006 kama  vazi  la  mtoko hata  ofisini na mtani{casual wear}  katika  nchi  za  wenzetu.


 Zari katika vazi la Pajama(pjs)

Pajama  ni neno  lililotoholewa  kutoka  lugha  ya  uajemi(persia) na  kutumika  katika lugha  ya  kingereza huko  India. vazi  hili  asili  yake  ni  India  na  lilikuwa  linavaliwa  na  jinsia  zote  pamoja  na  rika  zote,vazi hili  huvaliwa  wakati  Wa  kwenda kulala  tu usiku.Ili mwili uwe mwepesi kutokana na wepesi wa vazi lenyewe

                                            Joketi  ndani  ya  Pajama(pjs)

Vazi  hili  lilianza  kuvaliwa  mwaka  1870 kama  vazi  la  kulalia huko India.Mwaka 1886 ulaya  wakaanza kulivaaa nao kama  vazi  la  kulalia. kutokana  na  baridi  iliwabidi  kutafuta  vitambaa  vinavyo kidhi joto.Mwaka 2006 watu  wakaaza  kuvaa  kazini  ikakatazwa  kwani  ilionekana  wanawake  wanavaa  kwa  lengo  la  kuonesha  miili  yao.kwasababu vazi  la  pajama humuweka  mtu  huru  hivyo  hafai kuvalia  chupi  ili  uwe  huru  unapolala.

vazi  hili  kwa  baadhi  ya  nchi  toka  mwaka  2012 linapigwa  marufuku  watu  kulivaa  sehemu  za Makutano,ofisini,na hata  njiani. Vazi  hili  ni  mahususi  kwa  kulalala inagawa  kwa  sasa  ndiyo  habar  ya  mjini.

Aina  za  Pajáma

Polka  dots,plaids,floulards,paisleys.

Vitambaa  vya  Kushonea  Pajamá.

Silk,satini,polyester na lycra

Angalizo :wanawake  tunapo  vaa  hizi  pajama  afadhali  ndani  uvae  tight  ndefu  au fupi  kwa kuangalia kitambaa kama hakiko poa, ili  kukustili, kwa  wale  wapenda  mauzo  tinga  hivyo hivyooo. Asante.ukifurahia mada  ni  WhatsApp +255756377940


No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu