Naamini Mpenzi Msomaji unaye jaribu kufuatilia makala zangu za afya
unanielewa vema,Pia naomba mpenzi msomaji kama unatatizo ni vema zaidi ukimuona
dakitari ikiwa kile nilichokisema hapa kinakugusa kwa namna moja au nyingine, huenda
ndugu,Rafiki au Jirani yako anatatizo hili ni vema umshauri kwenda kituo cha afya mapema.Naomba kuelezea ugonjwa
huu wa Saratani ya Shingo ya Kizazi kama ifuatavyo.
Saratani ya Shingo ya Kizazi huwapata wanawake zaidi ya Laki tano
kwa Mwaka ambao huwa na maambukizi ya ugonjwa huu.Zaidi ya asilimia 80 ya
Wanawake hao wanaishi katika nchi masikini,zaidi ya vifo 274,000vya wanawake
husababishwa na Ugonjwa huu kila Mwaka,kila baada ya dakika 2,mwanamke mmoja
anafariki kutokana na Saratani ya Shingo ya kizazi duniani kote
.
.
Kati ya wanawake wawili
wanaofariki kwa Saratani ya matiti,mmoja hufariki kwa Saratani ya Shingo ya
Kizazi duniani kote,Saratani hii inashika nafasi ya pili katika Saratani za
wanawake duniani.Na ndiyo sababu kubwa ya vifo vya wanawake kwenye nchi
zinazoendelea.Tutambue kuwa Takwimu zilizo tajwa hapo juu sio namba
tu,zinawakilisha wake zetu,mama zetu,mabinti zetu na rafiki zetu.
Dalili ya Saratani ya Shingo ya Kizazi
Saratani hutokea wakati chembe
hai za sehemu yoyote ya mwili zinapokuwa bila mpangilio maalum katika shingo ya
kizazi.Shingo ya Kizazi ni sehemu ya mfuko wa uzazi inayounganisha sehemu ya
ndani na sehemu ya n’je (uke)
Human Papilloma Virus(HPV)
Hivi ni virusi ambavyo
husababisha Saratani ya shingo ya Kizazi,Saratani ya Shingo ya Kizazi huchukua
miaka 10-20 tangu kuambukizwa au mara nyingine inaweza kuchukua miaka miwili tu
kutokea kwa Saratani.
Saratani ya Shingo ya Kizazi husababishwa na vitu vifuaatavyo:
Wanawake wengi ambao hukutwa na
Saratani ya Shingo ya kizazi ni kuanzia miaka
35-55,wengi wao huwa
wameambukizwa na HPV wakiwa na umri kati ya miaka 13-20.
- Kufanya tendo la ndoa katika umri mdogo
- Upungufu wa kinga mwilini
- Kurithishana kati ya vizazi
- Ugonjwa wa mkanda wa Jeshi.
- Kuzaa watoto wengi
- Upungufu wa Madini ya Folic acid
- Magonjwa ya ngono yanayojirudia
- Kufanya mapenzi na mtu zaidi ya mmoja
Dalili za Saratani ya Shingo ya Kizazi
- Kutoka kwa damu ukeni kwa hali isiyo ya kawaida kwa uzito
- Maumivu makali wakati wa Kujamiana
- Kuvimba kwenye kinena
- Kutokwa na mkojo au kinyesi kusikozuilika,Pia ijulikane kuwa dalili hizi pia zinaweza kutokea katika magonjwa mengine ya Saratani ya Shingo ya kizazi,ni vizuri kupata ushauri ili ujue tatizo linalosababisha hizo dalili.
Mpenzi msomaji
Mada hii nimeirejea katika kipeperushi cha
“Tupambane
Kutokomeza Saratani ya Shingo ya Kizazi”kilichotolewa na
GlaxoSmithKline(GSK)kwa lengo la kuboresha afya.Asanteni
No comments:
Post a Comment