Enter your keyword

Culture for Life.

Wednesday, August 21, 2013

Mavazi ni Sababu ya Wewe kutovutia:


Mavazi ya Rangi Nyeusi.

Black Gown

 

Nguo Nyeusi siku zote huwapendeza watu wengi na haichagui rangi ya ngozi ya mtu pia unaweza kuvaa nguo yenye rangi nyeusi  sehemu yoyote.Wanawake wanaweza kuvaa nguo ya rangi hii na kuing’arisha na vikorombwezo vingine mfano Hereni,Mkufu,Bangiri,Pochi na Viatu au Skafu. Lakini unapokosea kuvaa nguo ya rangi hii lazima utapoteza muonekano wako ni kiwa na maana kuwa huwezi kupendeza endapo hutapangilia vazi hili.Pia wanaume ni vema kujipangilia  endapo utavaa Shati jeusi basi tambua utavaa na suruali gani kulingana na Shati lilivyobuniwa kama linaendana na Jinsi vaa Jinsi na kama linafaa kuvalia suruali ya kitambaa vaa hivyo pia zingatia mazingira unayokwenda.

Usivae Nguo ambayo inakuficha sana Mwili wako.




Pic credit.www.aliexpress.com


Sina maana kuwa watu wavae nguo za kuacha miili yao,ni kwamba vaa nguo ya heshima na iliyo katika mpangilio kama fupi isidhidi magoti,pia kama ndefu iwe ndefu isiwe ya kuishia katikati ya miguu,Kitu ninacho maanisha ni kwamba tusiwe na tabia ya kuvaa nguo nyingi kwa wakati mmoja kiasi kwamba hueleweki umevaa nini? Na kuufanya mwili wako kuelemewa na nguo.Usipende kuvaa vitu vizito au kiatu chenye sori ambayo ni nzito na I kakupelekea kushindwa kutembea.

Kuvaa Brazia ambayo sio kipimo cha maziwa yako.

Bra
Ukikosea kipimo cha maziwa yako katika kuchagua Brazia ya kuvaa,Maziwa yako yatashuka chini na kukufanya uonekane un Maziwa makubwa,  Mama anaye nyonyesha akijua kipimo cha maziwa yake anaweza kuonekana mrembo zaidi kuliko wewe ambaye Brazia yako imebeba maziwa.Kama hujui kipimo cha maziwa yako,jaribu kwenda maduka ya hivyo vitu na utatambua kipimo chako.


Uvaaji wa Nguo za kushika mwili(Jersey Fabric)

Kuna vitambaa vingine havifai kuvaliwa na watu wenye mwili mnene hasa wenye matumbo makubwa,naweza sema ni vema ukijitambua,ukivaa nguo ya aina hiyo inaugawa mwili wako ,hivyo basi hata kama umependeza utaonekana kituko.Wataalamu wanasema nguo za kubana pia zinachangia kuwa na maumbile mabaya,kuwa na tumbo kubwa ndiyom sababu watu wengi matumbo yao yamegawanyika kutokana na kuvaa nguo zinazobana matumbo,Hivyo basi mafuta yanakuwa haya shuki na kutengeneza tumbo lingine.

 

Mitindo ya Nywele

Kwa upande wa wanaume na wanawake huwa inatofautiana kulingana na  umri,hivyo basi ni vema kuzingatia hili kama mwanamke,mafano bibi asuke nywele zenye rangirangi lazima utachekesha cha msingi omba hata ushauri Saloni.Kitu kingine usukaji wako wa Nywele huweza kumtambulisha mtu kuwa wewe ni mtu wa aina gain?..Endelea kufuatilia mada zangu pia maoni ni muhimu sana ukipendezwa na hili  unaweza kumshikilsha(share) mwenzio katika mitandao yetu ya kijamii hapo chini.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu