Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, February 12, 2013

Ndoa za Arusha: Harusi, Virusi, Kiharusi


 Na Mpanda Vifodi


 Sasa ni katika moja ya hizo safari za kwenda Uswahilini ambapo lilizuka gumzo linalohusu ‘Ndoa za Arusha,’ ‘Wanandoa,’ na ‘Maovu yanayofanywa na wanandoa wenyewe hapa mjini …. Hapana sijazungumzia lolote kuhusu ‘Katerero!’ kwanza sijui maana yake ni nini.
 “Usitishwe na Ving’ora au Tarumbeta za Arusi, ndoa nyingi za Arusha huvunjika ndani ya mwaka mmoja tu tokea zifungwe.” Alisema msafiri mmoja ambaye sikupata fursa ya kumhoji kama yeye binafsi ameoa na ikiwa ni hivyo ndoa yake imedumu kwa muda gani.

 “Tena usitishwe kabisa na misururu mirefu ya magari siku za arusi, wala sare za wapambe, au pilau, ndafu, ‘Shampeini,’ na vile vinywaji ambavyo huwa vinasubiri hadi mchungaji na mwinjilisti waondoke ndipo vianze kusambazwa mezani.
 Na usijali kuwa wakati ndoa hiyo inafungwa Bibi Arusi tayari ni mjamzito na hakuna kithibitisho kuwa huyo ‘boya,’ anayemuoa ndiye mwenye hiyo mimba. Na usipate shida kujiuliza ikiwa Bwana Arusi naye anakumbuka hata jina la mkewe huyo mtarajiwa.

Na isikupe shida kabisa ikiwa utaona kama vile ‘Bwana Arusi,’ yuko bize akimfinyia jicho yule binti aliyeketi kiti cha Mbele kanisani na mbaye anatabasamu na kumtumia ujumbe wa simu unaosema; “Sweetie, nitakumiss leo jamani, lakini najua kesho tutakuwa wote, halafu Ahsante kwa ile M-Pesa ya jana, ila bado nahitaji Laki moja kwa ajili ya kodi ya Nyumba!”
 Hadi hapo sijaongea lolote kuhusu ‘Katerero,’ na hii ni kwa sababu sijui asilani hili neno huwa lina maana gani nyingine zaidi ya lile Gulio au Soko la akina Kiiza, tulilokuwa tunalisoma kwenye kile kitabu cha ‘Tujifunze Lugha Yetu (4).’
 Hivi tulikuwa tunazungumzia nini? Ooh! Ni kuhusu vifodi vya ‘Kidemi,’ Uswahilini,’ na mazungumzo ya wasafiri wake kuhusu jinsi ndoa za maharusi wa Arusha zinavyozungumza kabla hata ya ‘Kifo kuwatenganisha!’ hao waungwana.

Na tafadhali sana naomba usiendelee kulitaja hilo neno la ‘Katerero,’ maana kwanza halina uhusiano wowote na kile tunachokizungumzia hapa; isitoshe sijui hata vile vitabu vya zamani vya ‘Kiswahili,’ kwa shule za msingi vilipotelea wapi.Ila kwa wale wasiofahamu ni kwamba ‘Gulio,’ kama lile la kule ‘Katerero,’ ni soko la msimu au kwa lugha nyepesi, ‘Mnada!’ kama ule wa Ngaramtoni, Kisongo na Tengeru ambako watu hukusanyika ili kuuza na kununua na pia kuiba na kuibiwa bidhaa zao.

Na tunapozungumzia ‘Kuiba,’ na ‘Kuibiwa,’ watu hapa Arusha pia huiba wake au waume zao na wao pia kuibiwa wake au waume zao; ‘Ngoma droo!’ kama ambavyo wale ‘Machalii,’ wanaovaa ‘Njuti,’ kule Unga-Limited wanavyosema.Na maisha ya Arusha ni kama mnada; inadaiwa kunapokucha tu, watu wakielekea sehemu zao za kazi, biashara au uzururaji, mnada wa binadamu hufanyika. Naam zile dhambi zilizoshindikana huwa zinafanyika maofisini, viwandani, masokoni na hata mashuleni, na hasa kwenye vile vyuo vya ‘Maimuna,’ vinavyofundisha ‘English Course!’

Jioni kila mtu hurejea nyumbani, kwa mkewe au mumewe wakiwa wameshachoka na ‘Kazi,’ za mchana huku wakiwapigia kelele watumishi wa ndani au ‘Hausigeli,’ waharakishe kuleta chakula ili walale zao mapema.Siku hizi hakuna mtu anayelalamika kwenda kazini, maana sehemu za kazi zimegeuka kuwa

‘Magulio,’ naam kama yake ya Katerero, isipokuwa haya ya makazini hufanyika kila siku hayasubiri ule mnada wa Jumamosi Tengeru, Jumapili Ngaramtoni au Jumatatu Mbauda.Sasa hata kama minada hii ya siku za kazi hapa Arusha huwa haifanyiki kule ‘Katerero,’ kama ule wa ‘Kiiza,’ inadaiwa kuwa kuna kitu kinachoitwa ‘Katerero,’ katika hii minada na hii inachangia kuvunjika kwa ndoa nyingi hapa mjini.

 Na wakati mwingine hizi gulio za katerero za mjini hapa husababisha wababa wengine kurejea kutoka‘Safari za mbali,’ wakiwa ‘Wamevimba yote mapaja na kutetemeka mwili! Ugonjwa gani tena, Arusi, Kiharusi au Kirusi?Na kwa wamama na wadada kabla ya kutumbukia humo nao huwa wanapewa mistari kama ule wa lile shairi la ‘Kama mnataka mali ………!”
 chanzo cha story soma Gazeti la KUTOKA ARUSHA TOLEO LA 33,au tembelea website yetu www.kutokaarusha.com.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu