Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, May 2, 2017

MEN SWEATERS# Aina ya masweta ambayo mwanaume unayopaswa kuvaa ofisini


Nitadokeza aina ya masweta ambayo ukivaa kazini yatakufanya uonekane nadhifu:



Vesti sweta,Haya ni masweta ambayo ukikosea tu kuchagua unaweza kuonekana mzee au sweta likaonekana la mtoko,chagua Rangi nzuri kwa ofisi ni silki au nyeusi.Unaweza vaa na tai ndefu,au bow tai.

Solid-Color Sweta,Masweta ya mtindo unaweza kuvaa na  shati lenye kola yapo ya rangi tofauti lakini angalia rangi ambayo haing'ai sana rangi zilizopoa ni nzuri zaidi.Kwa mtu mfanyabiashara hupendelea rangi hizi zaidi ambazo ni nyeusi,kijani iliyoiva,maruni na grey

Argyle Sweta,Wanaume wengine hupenda masweta yenye michoro basi ukipata sweta lenye mistari kama hili  ni zuri zaidi.

Sweta za mistari,Hizi sweta ni nzuri sana lakini hakikisha kama una umbo kubwa chukua sweta zenye mistari midogo kwani huasahidia hata kufisha muonekano wa unene wako au kitambi,mtu mwembamba tumia sweta zenye mistari mikubwa zingatia pia ku match na surualia au shati lako pamoja na kiatu.
vilevile haya masweta unaweza vaa kazini ikiwa baridi ni kali sana kwani haya huwa ni mazito mno na hufaa kwa mtoko au mtaani.

haya masweta yanafahamika zaidi,unaweza vaa kama unavyoona hapo katika picha lakini siyo lazima ukunje.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu