Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, May 2, 2017

Men# Mwanaume ni pambo la mwanamke.

JOHN- DUMELO ni msanii  katika tasnia ya filamu toka ghana namkubali kwani miongoni mwa wanaume watanashati ambao kiukweli muonekano wao unanivutia sana ni mpambanaji na anaipenda jamii kwa ujumla.Tuzo alizowahi kupata..
Nollywood Movie Award for Best Actor in a Supporting Role
2012 · A Private Storm
Africa Movie Academy Award for Best Actor in a Supporting Role
2011 · A Private Storm
Africa Movie Academy Award for Most Promising Actor
2010 · Heart of Men
City People Entertainment Award for Best Actor of the Year (Ghana)
2016, 2014
City People Entertainment Award for Best Supporting Actor of the Year (Ghana)
2016


Leo nitakupa siri moja yaani jinsi ambavyo wanawake  tunavutiwa  na wanaume nadhifu, basi hata sisi wanawake tunavutiwa na wanaume wasafi kuanzia muonekano wake,Jinsi anavyoipenda ngozi yake,usafi wa mwanaume si tu kuoga maana wanaume wengine kuoga kwao mpaka sherehe,Unakuta mwanaume ananuka kikwapa yaani akikusogelea unatamani ukimbie hata kuongea naye ndiyo noma zaidi mdomo unanuka usipime.

Mwanaume mtanashati ni yule aliyevizuri katika fikra zake,mipango yake iko vema,Anajikubali na cha zaidi mwanaume asifiwi usafi tu hata kipato na ujue kutunza familia yako nyumbani pamoja na kuwa na mchango mzuri kwa jamii yako.

Mwanaume ambaye hakumbuki boksa yake alifua lini au aliibadilisha lini mmmh huyo hata mwenzi wako atakosa hamu na wewe maana mnapokutana anajua tu huyu mtu ndani yukoje?

Mwanaume anayenuka miguu wala hakumbuki kucha za miguu au mikononi alikata lini mhh huyo si mtanashati,
 Mwanaume anayejua kupangilia mavazi yake huyo nikivutio cha wengi lakini si mwanaume anayevaa kiuhuni,Hata kuaminika si rahisi sana,haijalishi unafanya kazi gani jiweke nadhifu.
Mwanaume asiyejua kuchana nywele au kutambua mtondo gani wa nywele akinyoa una mpa muonekano mzuri mmhmm.
 Mwanaume ambaye nyumba yake ipo katika mpangilio mbaya yaaani sebuleni ndoo za maji katikatiya meza,kitanda shuka la rangi ya kuficha uchafu au hakitandikwi wala mashuka haya fuliwi mmhm,,, 

Mwanaume ambaye ajui kupaka mafuta ,wala hajui thamani ya ngozi yake mmmh  hapana si mtanashati,na hajali ngozi yake huyo hapana maana akifungua vifungo vya shati lake au kuinua suruali yake miguuni yaani ngozi haifai haina hata mvuto dthh no.

 Nitaongea machache tu leo, siku nyingine nitaongezea. Jua tu mwanaume pia ni pambo la mwanamke hatuvutiwi na wanaume wachafu Na kama ukiona umependwa na wala huyo uliye naye hakuweki smart jua kuna kitu kafuata kama si pesa basi kingine{...................}

Mwanaume yeyote unayesoma makala hii kama unatabia moja wapo au ambazo sijazitaja unaweza jirekebisha,lakini kama unaona kuna tabia ambayo sijaitaja unaweza ongezea hapo na nitaiongeza katika makala hii...(COMMENT NI KWA JINSIA ZOTE UNAWEZA COMMENT)

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu