Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, January 7, 2017

Vazi La Kanisani Ndani ya African Print 2017

Siku ya jumapili ni siku ya Ibada kwa kila Mkristo.Ni vema ukavaa vazi la heshima lisilohalibu uwepo wa Mungu kwa waumini,Wakati mwingine unaweza vaa vazi ambalo ukipita tu watu wanasahau kusikiliza neno,Leo nitatupia picha baadhi ambazo unaweza ukavaa kanisani katika vazi la kitenge katika muonekano maridadi na waheshima zaidi.

Church Outfit.


Designer Jocktan Makeke 

 Kwa upande wa wanaume hakika kama ukipata mbunifu mzuri akakushone shati zuri la kitenge,bazee au batiki  kisha ukavaa na suruali yako au kadet yako.Hakika utapendeza sana na kuonekana Nadhifu na mstarabu.Tatizo siku hizi bado kuna vijana wanao amini shati la kitenge linavaliwa na wazee hapana endapo utapata mbunifu mzuri hutochukia vazi la Kiafrika.
 Iro and Buba ni vazi ambalo wenzetu nigeria na ghana wanavaa sana ,ni vazi ambalo hata ukiwa nyumbani unaweza kujifunga na ukapendeza katika muonekano uanotaka na ukavalia top yoyote unayotaka.Unachotakiwa kufanya ni kuchukua kitenge chako na kukutanisha pande mbili za kitenge katikati kisha kipande cha kulia peleka kushoto na kushoto kulia.




Mtindo wa shift skirt ni mtindo ambao hamtupi mtu,lazima upendeze


Mtoto wa Kiafrica huonekana mwenye Heshima zaidi anapokuwa katika vazi refu kama hili au skirt,Gauni hili pia inaweza kuwa outfit ya kawaida tu still ukapendeza ndani ya African Print.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu