Enter your keyword

Culture for Life.

Wednesday, June 10, 2015

NDOA NDOANO KATIKA JAMII....



Image result for tendo la ndoaImage result for tendo la ndoa
Katika safu hii nitazungumzia vitu vichache vinavyowafanya watu wasifurahie tendo la ndoa .Hapa nazungumza na wanandoa na wanaoelekea kungia katika ndoa.Leo tuangalie mambo baadhi kwa ufupi:
  1. Kuongelea matatizo wakati wa tendo la ndoa.Hapa mwanaume/mwanamke unapoona mwenzi wako anahamu na wewe baadala ya kusoma alama za nyakati wewe unaanza kuongelea shida zako,za ndugu hata majirani wakati mwingine mnaanza kukumbushiana majeraha mlio wahi kukwazana.Hii hali itawaoondoa katika raha mlio taka kuipata.Hapa sasa mmoja wapo anapotoka n’je na kukutana na mtu mwenye kusoma alama za nyakati utaipenda kwasababu utampoteza mwenza wako na hatokuwa na shauku na wewe.
  2. Kusumbuliwa na jinni mahaba,hili ni tatizo linalowakabiri wanandoa wengi hukosa hamu ya kufanya mapenzi na wenza wao hata kama alikuwa na shauku akiwa safarini kwamba nikifika mke/mme wangu basi leo nitafurahi lakini anapo mkaribia hamu ina isha.Watu wenye tabia hiyo jua anasumbuliwa na jini mahaba na baadhi ya dalili zao nikuota ndoto wanafanya mapenzi kwenye ndoto,kupoteza pete,kufunga harusi wakiwa katika ndoto n.k.Ukiona hivi wewe ingia katika maombi na ujitenge na hizo roho.
  3. Kutokuwa na Lugha ya mahaba .Wanaume/wanawake wengi huogopa kujiachilia na kumwambia mwenzi wako jinsi unavyojisikia,kuwa wazi kwa mwenzi wako usione aibu unapokuwa naye katika tendo la ndoa.Toa hata kiasauti kidogo hii itamfanya mwenzi wako kuona kuwa unamjali na mko pamoja hata unapo wahikufikia mshindo/kileleni usikae kama bubu endelea kumtia moyo mmeo/mkeo ikiwezekana mwambie aongeze kasi au apunguze mwambie unavyojisikia utamfanya aone kuwa bado una mpenda na akikukumbuka basi atakumbuka sauti zako na kuwa na hamu na wewe.
  4. Uchafu wa kitanda na chumba chetu.Hapa mwanamke ni jukumu lako kufanya chumba chenu kiwe kisafi mda wote.Wanawake wa siku hizi huu utandawazi utatumaliza na kuharibu ndoa zetu hasa tunapo waachia wadada wa kazi kufanya usafi wa chumba chenu.Mwanamke hakikisha huwaruhusu hata watoto kuingia chumbani kwako.kuwa na tabia ya kubadili shuka kila siku mumeo atavutiwa na kubadilisha muonekano wa chumba chako sio kila siku kitanda kina kaa kwenye dirisha au ukutatani.
  5. Uvivu wakati wa tendo la ndoa.Wanawake/wanaume wengi ni wavivu mwanamke usimwachie mumeo kukushughulikia tu wewe ukiwa umekaa kama gogo,wengine ukoroma kabisa hata kulala,hii huonesha dharau kwa mumeo pia wanaume wengine ni wavivu katika tendo la ndoa mshindo mmoja hoi,utampoteza mkeo ,wengine watakusaidia kazi.Mwisho kabisa napenda kuwaomba wanaume/wanawake kuzingatia usafi wa miili yetu  ikiwa ni pamoja na kunyoa nywele za makwapani,sehemu za siri na kusafisha vinywa vyetu  vizuri vilevile tupotaka kufanya tendo la ndoa  mkiweza nendeni hata bafuni muoge pamoja.Wanawake wenzangu ni vema ukiwa msafi zaidi na kujua kusafisha sehemu zetu vema hata kutumia vitu vya kuondoa harufu katika makwapa au vinywa vyetu ili waume zetu wasitukimbie.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu