Ushawahi kujiuliza haya maswali,kuwa ni rangi gani utavaa wakati kuagwa nyumbani kwenu,Ushawahi jiuliza unataka kuwa na muonekano gani siku ya sendoff yako,Je?Mume wangu mtarajiwa atavaa nini? ni kweli ni lazima tufanane kimavazi hata rangi tu ya nguo ina ulazima gani?,Wageni waalikwa watavaaje katika siku yangu.
Binti unayeagwa ni vema basi kuwa angala na mavazi ya kanisani, wakati wa kupiga picha,nyumbani, na vazi la kuvaa ukumbini kama una uwezo wa kufanya hivyo lakini kama huna mavazi mawili tu yanakutosha.
Vazi la kanisani ndilo utakalokwenda nalo kupiga picha kisha ukimaliza utaenda kuagwa nyumbani na familia yako.Kisha ukumbini unatafuta vazi zuri litakalo kufaa.
Kumbuka kuwa ugumu wa maisha au ukubwa na udogo wa mambo uko juu yako kulingana na kipato chako.
Baadhi ya picha zilizo nivutia katika muonekano wa vazi la Sendoff:
Kwa maelezo zaidi tafuta ukurasa wa mwanamitindo
https://www.instagram.com/p/Bj7AW6FB4pa/?hl=en&taken-by=ceolumineeofficial
HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MADHUBUTI WA MIRADI
YA MAENDELEO
-
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imepongeza uongozi
wa Halmashauri ya Jiji la Arusha ukiongozwa na Mkurugenzi wa Jiji, Ndugu
Joh...
19 hours ago





No comments:
Post a Comment