Enter your keyword

Culture for Life.

Showing posts with label Kitchen Party. Show all posts
Showing posts with label Kitchen Party. Show all posts

Wednesday, April 10, 2019

Umuhimu wa wazo katika Ubunifu . .#Afriposhdesign #Tanzania culture

By On April 10, 2019

Wasifu Binafsi
Jina -Glory James
Primary-Nkoanrua P.School
Secondary-Nkoanrua S.School
Univerisity-SUA
Wazo lako ndiyo utajiri wa maisha yako,Mtu mwingine hawezi kujua mawazo yako zaidi ya wewe mwenyewe utakapo lifanyia kazi wazo lako.Marafiki, wazazi,ndugu na watu wanao kuzunguka hawezi kuona faida ya wazo ikiwa wewe mwenyewe huwezi kulifanyia kazi ili waweze kuliona.

Safari ya Binti  Glory katika tasinia ya ubunifu
Amesomea mambo ya kilimo lakini aliona vema kutumia kipaji chake badala ya kuajiliwa.Afriposhi ilifanikiwa alipoamua kufanya na kuhakikishia umma kuwa inawezekana kufanya kazi za mikono bila kusita na kusubiri ajira .Anasema"Wazazi wangu hawakupenda nijiajiri lakini nilipowashilikisha na kuonesha juhudi, mama yangu alianza kunisaidia,na biashara yangu nafanya kupitia mindao ya kijamii hasa Instagram,Kupitia Instagram napata wateja wengi kutoka n'je na kidogo ndani ya nchi" Mpaka sasa ana followers 30.9k





Watanzania wengi hawajui namna ya kuvaa mapambo ya kiutamaduni(accesories) na mavazi yao jambo ambalo linapelekea kukosa wateja wa ndani.Wengi huamini kuwa vitu vya utamaduni vinafaa kuvaliwa na nguo za kitamaduni kitu ambacho sio sahihi kabisa.Vazi lolote linaweza kuvaliwa na culture yoyote ilimradi uzingatie muktadha(Location)

Changamoto anazokumbana nazo kubwa ni soko la ndani kutofahamu umuhimu wa vitu vya ndani na kujua namna ya kuvitumia hivyo ina mrudisha nyuma kibiashara na kujikita na soko la n'je.Wakati mwingine huwa inambidi kufundisha watu namna ya kuvaa na nguo.

Ushauri wangu kwa mabinti ni kuweza kuyafanyia kazi mawazo yao na kuacha kubweteka kwani linapoanza wazo moja huzaliwa wazo lengine.


Amekwisha valisha wasanii kama:Jokate Mwegelo na Janethn Jackson n.k
kwa maelezo zaid mfollow instagram: #Afriposhdesigns.  #Afriposhdesign or Glory
Anapatikana Arusha viwanja vya nanenane.
Phone no.0757074590,0756377940

Sunday, January 13, 2019

Colar Living Rangi ya mwaka 2019#Coral Living

By On January 13, 2019




              Optimism colar living color of the year 2019





Coral Living  ni rangi iliyochaguliwa na kampuni ya Pantone  rangi imeonesha kuvutia na viumbe wanaoishi kwenye maji,na hii rangi huwa inapatikana kwenye coral reefs,mwaka huu inabeba ujumbe kuwa ni rangi yenye kuonesha matumaini,ujasiri na mafanikio katika mwaka 2019.


Kama uliweza kufuatilia rangi hii ilitumika sana katika nyumba,ambapo watu wengi walikuwa wakipatka rangi hii kwenye kuta za n'je.turajie kuiona rangi hii katika sherehe nyingi.Ingawa wakati mwingine huwa si lazima kuitumia rangi ya mwaka inategemea na upendeleo wa Mtu wa rangi.
Nanukuu:






"Pantone Color of the Year 2019 Mug

SKU: 2019-001


Pair your favorite hot beverage with the cool new Color of the Year 2019: PANTONE 16-1546 Living Coral

The Pantone Color of the Year 2019, PANTONE 16-1546 Living Coral is an animating and life-affirming shade of orange with a golden undertone. We get energy from nature. Just as coral reefs are a source of sustenance and shelter to sea life, vibrant yet mellow PANTONE 16-1546 Living Coral embraces us with warmth and nourishment to provide comfort and buoyancy in our continually shifting environment"

Monday, August 13, 2018

Furaha ya Wazazi ni kumuaga binti yao #Sendoff Party#Mishono ya Sendoff

By On August 13, 2018
Ushawahi kujiuliza  haya maswali,kuwa ni rangi gani utavaa wakati kuagwa nyumbani kwenu,Ushawahi jiuliza unataka kuwa na muonekano gani siku ya sendoff yako,Je?Mume wangu mtarajiwa atavaa nini? ni kweli ni lazima tufanane kimavazi hata rangi tu ya nguo ina ulazima gani?,Wageni waalikwa watavaaje katika siku yangu.

Binti unayeagwa ni vema basi kuwa angala na mavazi ya kanisani, wakati wa kupiga picha,nyumbani, na vazi la kuvaa ukumbini kama una uwezo wa kufanya hivyo lakini kama huna mavazi mawili tu yanakutosha.

Vazi la kanisani ndilo utakalokwenda nalo kupiga picha kisha ukimaliza utaenda kuagwa nyumbani na familia yako.Kisha ukumbini unatafuta vazi zuri litakalo kufaa.

Kumbuka kuwa ugumu wa maisha au ukubwa na udogo wa mambo uko juu yako kulingana na kipato chako.
 
Baadhi ya picha zilizo nivutia katika muonekano wa vazi la Sendoff:



Kwa maelezo zaidi tafuta ukurasa wa  mwanamitindo

Friday, May 11, 2018

Ubunifu wa kipekee,kwa mtu wa kipekee

By On May 11, 2018



Ninapozungumzia ubunifu,hii ni hali ya kuwa na wazo La tofauti katika jambo unalofanya,Mimi nazungumzia ubunifu wa mavazi ambao humfanya mtu kuwa wa kipekee.

Hivyo upekee wa mavazi ndiyo hutambulisha mtu,mfano mtu huambiwa umevaa kama changudoa kutokana na muonekano wa vazi hulilovaa kuwa ni la kichangudoa,au unaweza ambiwa umevaa kama bibi,babu,kijana,mshamba ,miss nikutokana na muonekano wako.

Ushauri wangu ningwomba uwe na mtindo wa vazi lenye staha linalokutambulisha vema.

Thursday, March 29, 2018

Kitenge ndani ya Manyoa.#kichenparty#vitenge

By On March 29, 2018
Tunapozungumzia ubunifu,ni ufundi anaoutumia msanii yeyote katika kuwasilisha/kufanya kazi yake iwe tofauti na na kazi za watu wengin

Vazi La kitenge ni vazi unaloweza kuchanganya na kitambaa au mapambo yoyote katika ubunifu na ukapata vazi LA kipekee ,kama hilo vazi ni la kitenge ila limetiwa nakshi za manyoa kazi kwako.

Saturday, January 27, 2018

Pata muonekano wa Wema Sepetu katika nguva.

By On January 27, 2018

 mnaopenda kudesa muonekano huu hata kwa harusi uko poa lakini upate mbunifu mzuri hasa wa nguo. Mwanadada Wema mara nyingi kuitazama mishono yake ya party huwa  na muuonekano wa nguva lkn hili ni balaa mabibi harusi hawaoni ndani. Big up kwa Designer wake.
.



Wednesday, September 6, 2017

Ubunifu wa kitenge 2017

By On September 06, 2017

Msanii Elizabeth Michael katika muonekano wa kitenge 2017

Muonekano huu wa kuongezea nakshi katika kitenge umekuwa kivutio hasa unapoweza kuchanganya urembo wa hiyo nashi katika kitenge chako,unaweza kuweka chini ya magoti,shingoni,katika kifua,hata mikononi.



Vazi la kitenge ni vazi ambalo ubora wake kila siku unaongezeka,kinachotakiwa ni kuongeza ubunifu vazi hili ili kulipa uthamani wake,Huu ni mtindo mpya wa kitenge ambao umeonekana kuwavutia watu wengi hasa nakshi hii inapowekwa.

Monday, May 1, 2017

Joggers for Men: How to Wear Joggers

By On May 01, 2017
Zamani sngland(jogger) zilikuwa zikivaliwa na wanaume kwa ajili ya michezo.Joga ni huwa na kitambaa kinachotanuka,pia huwa nyepesi vilevile huwa hazingizi joto.Hivyo wanaume wengi hupenda kuvalia ndani ya nguo zao kabla ya kuvaa shati au kuweka jacketi juu.Kwa ajili ya kazi ni vema kuwa na joga nyeupe ambayo hata ukivalia suti au wakati wa joto unapovaa si rahisi kupitisha joto.

Friday, April 14, 2017

Masai wedding dress the best Tanzanian style ever.

By On April 14, 2017

Bibi harusi kulia akiwa na msimamizi wake katika mazingira ya umasain,Hili ndilo kabila linalodumisha utamaduni wake Tanzania ,kabila hili lina utajiri wa vitu vya asili ambavyo binafsi huwa vinanivutia sana kwani vinapobuniwa vema basi huwa na thamani kuwa hata katika kununua.

PIC CREDIT: ME PRODUCTION-ARUSHA

PIC CREDIT: ME PRODUCTION-ARUSHA

 Bibi harusi wa kabila la kimasai vazi lake lazima lijae nakshi za shanga kwa wingi pamoja na cheni ya kimasai hiyo ndefu pamoja na hizo zinazo onekana shingoni kwake ni muhimu sana kwa binti wa kimasai,ambazo huita enkarewa.

 Vazi la bibi harusi wa kimasai si chini ya T.SH 500,000/=Napenda watanzania wote tungekuwa na mwamko wa kuvaa mavazi yetu ya asili hata kama huna basi waweza vazi la kitamaduni lilipo katika kabila lako.

 

PIC CREDIT: ME PRODUCTION-ARUSHA

ME PRODUCTION-ARUSHA 

Wapo  Jijini Arusha karibu na jengo la Namvua Plaza Ghorofa ya Kwanza karibu na Stand kubwa ya mabasi ya mikoani.

Wanapiga picha katika location tofauti pia katika sherehe mbalimbali kama harusi,birthday,sendoff,cocktail part...na matukio yoyote pamoja na video shooting wana bei poa fanya nao kazi ufurahie kumbukumbu ya tukio lako.

Watafute kwa mawasiliano haya:

meproduction22gmail.com

Mobile no.+255 752026643

                  +255 763782044

 


Friday, December 9, 2016

MAGAUNI MAREFU YA VITENGE YANAYOWAVUTIA WANAWAKE WA KIAFRICA.

By On December 09, 2016

 MSANII JACQUELINE WOLPER NDANI YA MAX DRESS.





ELIZABETH MICHAEL a.k.aLULU  ndani ya Vazi la kitenge.




MITINDO MIKALI YA VITENGE MWAKA 2016.....

By On December 09, 2016

Koti refu la kitenge humpendeza mtu mwenye umbo lolote lilie,koti hili unaweza vaa hivyo na gauni fupi la rangi moja,suruali rangi moja na top rangi moja au iliyipo katika kitengeau unaweza kuvaa suruali ya kitenge cha koti na shati la rangi moja. kisha ukajipamba na mapambo yanayoendana na kitenge chako,kama vile hereni,mkufu,bangili,na hata kiatu.Vazi hili unaweza vaa:

  1.  kanisani ikiwa koti lako linafunga hata kwa kifungo kimoja,

  2. Unaweza kuvaa kwenye pati kwa kuachia kifungo bila kufunga.

Unaweza vaa hivi kwa mtoko,familia yako inaweza kupendeza hivi kwa piece mbili  na nusu za vitenge,nunua kitenge cha doti 3,


Add caption

Mpenzi msomaji wa makala zangu za mitindo ya vitenge jitahidi kushona mshono unaoendana na umbo lako,Wengi hupenda mishono mizuri wakiamini watapendeza pia kabla ya kushona shauriana na fundi wako vilevile  ni vema kufahamu rangi zinazokupendeza.

Friday, June 12, 2015

MITINDO YA VITENGE 2015.

By On June 12, 2015

REMBA NDIYO HABARI YA MJINI KWASASA USIPITWE,UNAWEZA KUTUMIA VITAMBAA VYA SATINI,VElVET,LACE,KITENGE n.k

Wednesday, June 10, 2015

FAIDA YA TENDO LA NDOA.

By On June 10, 2015


Image result for tendo la ndoa
Nitumaini langu wewe unayesoma makala hii ni mwanandoa au upo katika harakati za kuingia katika ndoa.Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa hufanywa na wana ndoa tu na siyo wachumba,marafiki na halifanyiki hovyohovyo tu bila makubaliano ya watu wawili nikiwa na maana ya wanandoa.
Image result for tendo la ndoa
1.Tendo hili ni muhimu kwani hufanya ndoa iendelee kuwepo.Ndiyo sababu wanandoa mmoja wapo anapokosa kupata ushirikiano kwa mwenza wake.hupelekea ndoa kuvunjika na kufanya mmoja wapo kutoka n’je ya ndoa.

2.Tendo la ndoa ni burudani kwa wanandoa.Wakati mwingine mtu anayekosa kufanya tendo hili katika ndoa hupelekea migogoro hata kununiana ndani ya nyumba,kuwa na msongo wa mawazo.

3.Hapa wanandoa wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujitoa.

4.lengo hasa la tendo la ndoa ni uzazi.Ili kuikamilisha ndoa lazima mpate watoto ndiyo sababu ya kuunganika na kuwa mwili mmoja.Kwasasa tendo la ndoa limekuwa likifanywa.kinyume,wengi wetu katika jamii wanafanya bila kuzingatiaa maadili ya hili tendo,mzee kwa kijana,mume au mke wa mtu,vijana,watoto walio chini ya miaka 18 pia wamejiingiza katika zinaa(Uzinzi).Mpenzi msomaji kama wewe ni mmoja wapo tulia kuwa na mmoja ambaye ni mume au mke wako ndiyo utafurahia tendo la ndoa.

Saturday, May 9, 2015

MITINDO MIKALI YA VITENGE 2015

By On May 09, 2015

Remba ndiyo habari ya mjini kwa Tz ingawa wa Nigeria walianza kitambo,ila kwa sasa ndiyo imekamata rika zote hasa kwenye shughuli za sherehe..


kitenge kimechanganywa na kitambaa kinachovutika.

Suruali ya Kitenge simple with pemplum top

Solo ya style ya kitenge iliyokatwa kimtego,unaweza vaa popote kulingana na mazingira.Hapa kila shape inapendeza.

Iro$Buba ya kitenge ushindwe wewe.

Gauni la  kitenge solo staili


3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu