Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, February 2, 2013

Harufu mbaya ukeni

Tatizo la uchafu ukeni
Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano, ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin's glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix).

Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku. Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.

Sababu za kutokwa na uchafu huo
Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri. Maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis Bacteria n.k husababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.
Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hususani mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya bacteria wanaosababisha harufu mbaya.

Dalili za ugonjwa wa kutoa harufu
Wanawake wenye tatizo la Vaginosis huwa na dalili kubwa ya kutokwa na
ute na majimaji yasiyo ya kawaida (Uchafu) kutoka sehemu za siri. Uchafu huu huwa unatoa harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.
  •  Wakati mwingine uchafu wenye rangi kama ya kijani hutoka
  • - -Kuwashwa na kuchomachoma sehemu za siri, mgonjwa asipopatiwa tiba haraka husababisha vidonda sehemu za siri.
  • - Mwanamke anapoona anatokwa na ute uliochanganyikana na damu hata kama hayupo kwenye siku zake, hii ni dalili nyingine ya Vaginosis.
  • - Maumivu makali wakati wa tendo pia ni dalili za ugonjwa huu.

Matibabu
Tatizo hili hutibika hospitalini baada ya vipimo vya kitaalamu kuchukuliwa na daktari au nesi mwenye uzoefu wa kutosha juu ya magonjwa ya wanawake. Dawa za kupaka (Ointment/ Cream) na dawa za kumeza (Pills) huweza kumaliza tatizo hili. Kumbuka: Ni makosa kutumia dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa daktari au nesi.
Jihadhari
wanawake wengi hupenda kutumia baadhi ya dawa ukeni kwa lengo la kuongeza vionjo kwenye mapenzi pia kuufanya uke kunukia vizuri vitu hivyo ni kama sabuni za kukaza uke,shabo inayowekwa kwenye maji machafu ili kusafisha wenyewe huweka ukeni ili kukaza uke,dawa za kusafishia ukeni hasa zenye kemikali,hudi asali na vingine vingi naomba niseme kuwa njia hizi hufurahisha kwa mda mfupi lakini madhara yake ni makubwa kama hivyo kuanza kutoa harufu mbaya.

2 comments:

  1. aisee! makala nzuri sana hii...!
    natamani kila mwanamke angepata nafasi ya kuisoma

    ReplyDelete
  2. DADA UMENENA,ELIMU HII IWAFIKIE HADI WANAWAKE WA VIJIJI

    ReplyDelete

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu