Vazi la kitenge litumike katika Sherehe zote za kitaifa."Maoni Ya Neema Daniel"
By
SINYATIBLOG
On
December 15, 2016
In
Ubunifu
Neema Daniel ni mjasiriamali anayejishughulisha na ubunifu wa vitu vya asili kwa kutumia vitenge.Anabuni viatu na mikoba ya vitenge.
![]() |
Kitengeflat shoes |
Mahojiano ya Neema na Sinyatiblog yaliyofanyika kwa njia ya Whatsapp na Facebook messenger.
Sinyatiblog:Neema unajishughulisha na nini ili kupambana na maisha.
Sinyatiblog:Nauza vitenge,nashona nguo za vitenge ,natengeneza
viatu na handbag za vitenge.
Neema:Wateja wangu wengi ni wafanyakazi wa maofisini na
kwenye mitandao.
Sinyatiblog:Nini kinafanya kazi zako zionekane ni za tofauti
na kazi za wengine?
Neema:Utofauti wangu ni kwamba watu wamezoea kubeba handbag
za ngozi,mimi nimeibadilisha kidogo kwa kuivalisha kitenge na kiatu pia, sasa
imekuwa tofauti na inavutia wengi.
Sinyatiblog:Unatumia material gani hasa katika kutengeneza
hizo handbag na viatu.
Neema: Huwa nanunua handbag au viatu alafu naivalisha kitenge.
![]() |
| Makenzi flat shoes na Mkoba.Unaweza kuvaa na nguo ya rangi moja pamoja na kujipamba kwa nakshi kama bangili mkufu na hereni. |
Sinyatiblog:unaishauri nini jamii kuhusiana na kupenda vitu
vya asili hasa vya ndani ya nchi.
Neema:Nashauri jamii wapende vitu vya asili maana ndiyo asili yetu kwa afrika
Sinyatiblog:Neno moja
kwa jamii unaloweza kuwashauri.
Neema:Okay tupende kuwa wabunifu wa vitu mbalimbali ili
isaidie kuongeza kipato.
Sinyatiblog:kama ungepata fursa ya kushauri serikali kuhusu vazi la taifa ungesemaje?
Neema:Ningependeza sana kila sherehe za kitaifa kuwe na sare
za vitenge kama vazi letu la kitaifa.
![]() |
Hii ni raba ya kawaida lakini imevalishiwa kitenge na kibao kwaajili ya mtoto. |
Mawasiliano ya Neema Daniel.
Napatikana insta:Ulimwengu_wa_vitenge.
No.0713655363
DSM-Kigamboni





















