Neema Daniel ni mjasiriamali anayejishughulisha na ubunifu wa vitu vya asili kwa kutumia vitenge.Anabuni viatu na mikoba ya vitenge.
Kitengeflat shoes |
Mahojiano ya Neema na Sinyatiblog yaliyofanyika kwa njia ya Whatsapp na Facebook messenger.
Sinyatiblog:Neema unajishughulisha na nini ili kupambana na maisha.
Sinyatiblog:Nauza vitenge,nashona nguo za vitenge ,natengeneza
viatu na handbag za vitenge.
Neema:Wateja wangu wengi ni wafanyakazi wa maofisini na
kwenye mitandao.
Sinyatiblog:Nini kinafanya kazi zako zionekane ni za tofauti
na kazi za wengine?
Neema:Utofauti wangu ni kwamba watu wamezoea kubeba handbag
za ngozi,mimi nimeibadilisha kidogo kwa kuivalisha kitenge na kiatu pia, sasa
imekuwa tofauti na inavutia wengi.
Sinyatiblog:Unatumia material gani hasa katika kutengeneza
hizo handbag na viatu.
Neema: Huwa nanunua handbag au viatu alafu naivalisha kitenge.
Makenzi flat shoes na Mkoba.Unaweza kuvaa na nguo ya rangi moja pamoja na kujipamba kwa nakshi kama bangili mkufu na hereni. |
Sinyatiblog:unaishauri nini jamii kuhusiana na kupenda vitu
vya asili hasa vya ndani ya nchi.
Neema:Nashauri jamii wapende vitu vya asili maana ndiyo asili yetu kwa afrika
Sinyatiblog:Neno moja
kwa jamii unaloweza kuwashauri.
Neema:Okay tupende kuwa wabunifu wa vitu mbalimbali ili
isaidie kuongeza kipato.
Sinyatiblog:kama ungepata fursa ya kushauri serikali kuhusu vazi la taifa ungesemaje?
Neema:Ningependeza sana kila sherehe za kitaifa kuwe na sare
za vitenge kama vazi letu la kitaifa.
Hii ni raba ya kawaida lakini imevalishiwa kitenge na kibao kwaajili ya mtoto. |
Mawasiliano ya Neema Daniel.
Napatikana insta:Ulimwengu_wa_vitenge.
No.0713655363
DSM-Kigamboni
No comments:
Post a Comment