Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, January 10, 2013

JINSI YA KUMJUA MWANAMKE UMTAKAYE AU MWANAUME

  •                                   JINSI YA KUMJUA MWANAUME  AU MWANAMKE UMTAKAYE.
    JITAMBUE
    Kwanza wewe kama mwanamke au mwanaume  mwenyewe unatakiwa ujifahamu na kufahamu vigezo vya mpenzi unayemhitaji katika maisha yako.wanawake wengi hawajui wanahitaji wapenzi wa aina gani, hivyo wanajikuta kama watu wanaoingia sokoni bila kujua wanataka kununua nini? Ndiyo maana wengi wameangukia kwa matapeli wa mapenzi, wakachezewa na kuumizwa moyo bure.

    SIFA ZA UMTAKAYE.
    Keti chini na kuorodhesha vigezo vya mwanaume unayemtaka. Baada ya hapo orodhesha tena kasoro za mwanaume unazoweza kuzivumilia na zile ambazo huwezi kuzivumilia kabisa. Hii inatokana na ukweli kwamba mwanadamu hajakamilika,na ana upungufu wake.

    TUMIA MACHO
    Anza kumsaka huyo mwanaume kwa kutumia milango ya fahamu. Cha kufanya hapa ni kuruhusu macho yawaone wanaume na kuwatathmini kwa maumbile yao ya nje na kisha kupata majibu kutoka moyoni juu ya kuvutia kwao ambako hutambulika kwa moyo kuridhika na mwili kusisimka.

    JENGA MAZOEA NAYE
    Kuanzisha safari ya kuchunguza tabia za nje na za ndani kivitendo. Hapa suala la ukaribu baina ya mwanaume na mwanamke linahitajika. Msingi unaotajwa hapa ni kujenga mazoea ya kawaida yasiyokuwa na masuala ya kimapenzi na ngono. Kutambuana, dini, viwango vya elimu, kabila na makundi ya marafiki ni mambo ya kuzingatia.

    Katika uchunguzi huu mwanamke anayetafuta mpenzi hana budi kupitia na kumlinganisha huyo aliyempata na vigezo alivyojiwekea. Zoezi hili liendane na kuweka alama ya pata kila anapobaini kuwa mwanaume anayemchunguza amepata moja ya vigezo vyake. Lakini pia aweke alama ya kosa kwa kila kasoro anayoivumilia na ile asiyoivumilia.

    HAKIKI SIFA ZAKE
    Jipe muda wa kutosha kati ya miezi sita na mwaka kumchunguza huyo mwanaume au mwanamke kisha keti chini na anza kujumlisha alama za vigezo ulivyovijiwekea na jinsi mwanaume huyo alivyopata au kukosa.

    Ikibainika uliyechagua amepata zaidi ya nusu ya alama ya vigezo vilivyowekwa, basi ujue kuwa anafaa. Kuhusu alama chache alizokosa unaweza kumsaidia kuzikamilisha pole pole mkiwa kwenye maisha ya ndoa.

    Lakini angalizo kubwa kabisa ni kwamba mwanaume akionekana kuanguka katika kasoro zisizoweza kuvumilia kwa zaidi ya alama tatu. Yaani kwa mfano ni mlevi, mwizi, muongo, mbishi na katika hizo kashindwa 3, huyu hafai, ni vema akawekwa kando kwani huwezi kubeba kero 3 kwa pamoja katika maisha.

    WEKA MALENGO
    Lazima baada ya kuchunguzana kwa kina wapenzi watengeneze muongozo wa mapenzi yao. Wasiwe kama wanyama, lazima mipango ya wapi wametoka walipo na wanapokwenda waifahamu.
    Hata hivyo, wataalamu wanasema lazima wapenzi wapime umakini wao kwa vitendo. Kama wamekubaliana kuoana, suala la mume kwenda kujitambulisha kwa wakwe na hatua ya kuiendea ndoa ionekane. Usiri usiwepo tena. Kila mmoja amuone mwenzake kama sehemu ya maisha yake na mara zote wasaidiane kwa ukaribu.

    USHIRIKI WA NDUGU/MARAFIKI
    Ni vema ndugu wakashirikishwa ili kuwapa nafasi na wao ya kuamua kama mapenzi hayo ni budi yakaendelea au yakasitishwa. Ni ukweli ulio wazi kwamba licha ya wengi kupuuza maamuzi ya ndugu kwa madai ya kuwa hawana nafasi kwa wapenda nao, lakini uchunguzi unaonesha kuwa wapenzi wengi huachana kutokana na sumu za ndugu hasa pale wanapokuwa wameonesha kutounga mkono uhusiano wa wanaotaka kuoana.

    TENDO LA NDOA
    Hatua hii ni ya kuweza kuzungumzia ufanyaji mapenzi, hapa nina maana kama wapenzi wamejizuia kwa muda mrefu na wanahisi kuchoka wanaweza kujadiliana kuhusu tendo la ndoa na kuamua kuwa pamoja huku wakizingatia suala la afya na uzazi salama.

    NDOA
    Kutimizwa kwa ahadi ya kuoana ni hatua ya tisa ambayo nayo si vema ikachukua muda mwingi kutekelezeka, kwani ucheleweshaji mwingi wa ndoa nao huvunja moyo na mara nyingine umewafanya wengi kutoaminiana.

    UVUMILIVU
    Kuamua kuwa mwili mmoja kwa kuvumilia na kuwa tayari kukabiliana na changamoto zote za maisha ukiwemo mkwamo na dhiki ambazo huchangia sana ndoa nyingi kuvunjika. Hapa pia ni wajibu wa wanandoa kuchukuliana udhaifu na kusaidiana.

    Kuwa tayari kujifunza na kujali zaidi upendo kuliko hisia za mwili ambazo wakati mwingine hudanganya hivyo kumfanya mwanandoa asivutiwe na mwenzake

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu