Enter your keyword

Culture for Life.

Tuesday, March 7, 2017

ITAMBUE NAFASI YA MWANAMKE KIBIBLIA.

Mpenzi msomaji wa makala zangu natumaini wote mnatambua kuwa siku ya tarehe 8march ni siku ambayo tunadhimisha siku ya wanawake duniani,Katika pitapita zangu  nimekutana na hii makala ambayo inamuonyesha huyu mwanamke kibiblia ana nafasi gani:


Na; Patrick samson Sanga.
Mwanzo 1:27 ‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. Sikiliza mahali popote pale mwanamke ni mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya mambo kuliko hata mwanaume.Ikiwa ushawishi huu utatumiwa katika mpango wa Mungu basi kusudi la Mungu litatekelezwa.
Mungu hakumwumba mwanamke kwa bahati mbaya au makosa,kila ambacho Mungu alikifanya ,alikifanya kwa kusudi.kwa lugha nyingine kila ambacho Mungu alikifanya maana yake moja kina nafasi mbele zake na mbili kuna wajibu ambao Mungu aliweka ili utekelezwe na hicho kitu.
Lengo la ujumbe huu ni kukueleza nafasi ambayo Mungu amempa mwanamke katika kanisa,jamii,nchi,ndoa na nk na wajibu wa yeye kutekeleza katika nafasi hiyo:-

1.Mungu anamtazama mwanamke kama msaidizi wa mumewe . 

 Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema si vyema huyo mtu awe peke yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”. Tangu kuumbwa kwa Adam,mpaka Mungu kumletea Eva inasemekana miaka mingi ilipita hapa katikati.

Sasa tunajua katika ile sura ya kwanza na ya pili ya kitabu cha mwanzo,Mungu alikuwa amempa Adam wajibu wa kutekeleza.Ikafika wakati Mungu akaona ule wajibu ni mkubwa sana kwa Adam kuutekelekeza ndipo akampa Eva.Kitu Mungu anataka tujue hapa ni hiki,wajibu aliopewa Adam peke yake asingeweza kuutekeleza bila Eva,maana yake nafasi ya Eva kwa Adam ilikuwa ni ya muhimu zaidi.Pasipo Eva,Adam angeshindwa kutekeleza wajibu.Sasa hata leo katika ndoa,kanisa Mungu ameweka wanawake ili wawe wasaidizi katika majukumu ambayo Mungu amewapa na waume zao au wachungaji wao makanisani.

2. Mwanamke kama mlinzi wa agano na kusudi la Mungu. 

Mithali 14:1 “ Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake ; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe” , Mwanzo 3;13 “ Bwana Mungu akamwambia mwanamke ,nini hili ulilolifanya ? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya ,nikala”..
Ndoa ni agano la Mungu kwa wanadamu. Mlinzi wa agano kimsingi ni mwanamke. Mara nyingi shetani akitaka kuvuruga ndoa atatafuta mpenyo au nafasi hiyo kwa mwanamke ili asambaratishe ndoa hiyo.Sasa mwanamke yupo ili kulinda kusudi hilo.Asipokaa kwenye nafasi yake ya ulinzi basi ajue kwamba kusudi la Mungu la kuwaunganisha halitatimia.Nisikilize ndoa yoyote inapovuruguka ujue mwanamke hakusimama vema kwenye nafasi yake ya ulinzi.

 Ngoja nikuonyeshe kitu hiki. Adam na Eva walipokula tunda ambalo Mungu aliwaambia wasile , kila mmoja wao aliulwiza swali lake. Adamu aliulizwa uko wapi? Mwanzo 3:9, na Eva alimwambia Mwanamke ni nini hili ulilolifanya , Mwanzo 3:13.Ipo tofauti kubwa sana katika haya maswali mawili.Swali la Adam lilimaanisha kwa nini haupo kwenye nafasi yako? Na swali la Eva lilivuka hapo na kumaanisha kwa nini hujafanya ulilotakiwa kufanya yaani kulinda agano.Mahali popote mwanamke ulipo ikiwa ni katika ndoa ,kanisa ,jamii,nchi, jifunze kulinda kusudi la Mungu ambalo unajua Mungu amekuagiza . jifunze kupitia mama yake Musa , yeye alilinda agano la wana wa wa Israeli kwa kumficha Musa na kuhakikisha hafi maana alijua Musa hakuzaliwa kwa bahati mbaya. Kutoka 2:1-10.

3.mwanamke kama muombolezaji.

Luka 23;27-28 “Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumuombolezea , Yesu akawageukia akasema ,Enyi binti za Yerusalemu ,msinillie mimi bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu”.Sikliliza , Mungu amewapa kinamama uwezo mkubwa wa kuomboleza kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ndani ya jamii ,ndoa, kanisa, nchi nk. Hivyo Mungu anamuhesabu mwanamke kama muombolezaji.

Hii ina maana kuwa  kuna vitu havi jakaa sawasawa kwenye ndoa,kanisa,nchi nk, Mungu anajua mwanamke atasimama kwenye nafasi yake na kuomba ili Mungu apate kuliponya taifa kupitia maombi .Ukiona maasi mengi yamezidi katika taifa mfano, vijana wa kike kutoa mimba, uasherati,uchafu na uzinzi basi ujue kina mama katika mji au taifa hawajasimama vizuri kwenye nafasi zao. Si kana kwamba nawalaaumu mama zangu na dada zangu kwa kusema hivyo,bali ninachotaka niwaonyeshe ni kwamba usalama na maendeleo mazuri ya vijana wa kike na kiume katika familia,kanisa na taifa kwa ujumla upo katika mikono yenu na ndio maana Yesu aliwaambia mjililie ninyi na hao vijana wenu.

Nikuulize swali , jiulize una watoto wangapi?, Tabia na mwenendo wao ukoje?,, Je ni mzuri? Unambariki Mungu? sivyo jiulize chanzo cha tabia hizo kwa mwananao ni nini? au ni nani aliyehusika na tabia hiyo? Najua unaweza kwa haraka kusema ni shetani au kumtupia lawama mmeo.

Sikiliza Shetani huwa hafanyi chochote isipokuwa pale anapokuwa  amepewa nafasi na mtu au watu fulani , kwa kifupi mtu anaposhindwa kusimama kwenye nafasi yake. Sasa ukisoma vizuri Biblia utagundua nafasi ambayo Mungu amempa  mwanamke kwa habari ya watoto wake, ndoa yake, kanisa lake kwa ujumla.

Jifunze kusimama kwenye nafasi yako, funga na kuomba kwa ajili ya taifa hili ili Bwana Mungu apate kuliponya . maombi yako yatasababisha kutengenezwa kwa mahali palipobomoka na kurejeshwa kwa njia za kukalia.

4.Mwanamke kama mlinzi wa nafsi ya mtoto wake wa kiume .

Katika hii sura ya 31 ya kitabu cha Mithali tunaona habari za mama mmoja ambaye alikuwa na mtoto wa kiume na huyu mtoto alikuwa ni mfalme. Ule mstari wa pili unasema “ Ni nini mwanangu ?, tena ,nini mwana wa tumbo langu? Tena nini mwana wa nadhiri zangu ? Usiwape wanawake nguvu zako; wala moyo wako usiwape wale waharibuo wafalme”. kinamama wakijua namna ya kuzikamata nafsi za watoto wao wa kiume ,nakuambia kuna uwezekano mkubwa kabisa hawa watoto wasifanye tendo la ndoa mpaka watakapo kuja kuoa.

Hili litawezekana pale tu kinamama watapofanikiwa kuzikamata na kukaa kwenye nafasi za watoto wao wa kiume.Huyu mama alimuuliza maswali mengi mwanawe kwa sababu aliona nafasi yake mama kwenye nafsi ya mwanawe inanyang’anywa na wanawake wengine.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu