Mwanamuziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki,
Dhamira zilizopo katika wimbo wa msanii Ney wa mitego wapo
Napenda kutoa pongezi zangu kwa Raisi wetu Dkt..John Pombe
Magufuli kwa kuruhusu huu wimbo kupigwa katika vyombo vya habari vilevile
kumtaka msanii huyu kuongeza maudhui mengine katika wimbo huu ili kuielimisha
jamii,Pili pongezi zangu ziende kwa msanii huyu wa mziki wa kizazi kipya Ney wa mitego kwanza kabisa kwa kutumia lugha
ya Kiswahili katika wimbo wake kwani unasaidia sana kuikuza lugha ya Kiswahili pia kwa kutumia lugha raihisi ambayo inaeleweka kwa jamii.
Msanii ni kioo cha jamii na ni daraja la
jamii,Katika wimbo huu binafsi amenigusa sana kwani wasanii wengi wamejikita
katika maudhui ya mapenzi na kusahau matatizo yanayoikabili jamii vilevile ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine pamoja na kuwa fundisho kwa wasanii wengi kuwa wabunifu zaidi katika uwasilishaji wa maudhui ya wazingatie zaidi kipengele cha fani ili kiende sanjari na maudhui.
Kwa ujumla
msanii Ney wa Mitego ameweka wazi matatizo yaliyopo katika jamii katka nchi nyingi.Nikianza na
maudhui nita zitaja dhamira ndogondogo zilizojitokeza katika wimbo huu
i. Kufanya kazi kwa bidii,” uchopanda leo ndiyo utakachovuna kesho”.
ii. Matumizi ya madawa ya kulevya na ukabaji,mfano wasanii mateja,wanafunzi vyuo vikuu na viongozi wanaotumia madawa ya kulevya.
iii. Uhuru wa kuzungumza mf vyombo vya habari
iv. Suala la uwajibikaji kwa viongozii
v. Suala elimu mf kutumia vyeti bandia
vi. Mmomonyoko wa maadili mf {mademu } wanawake kusagana,Biashara ya ngono,mambo hayo yapo kinyume na utamaduni wetu na si kwa wanawake tu bali hata wanaume wanaojihusisha na ushoga ni vema kuacha na kuzingatia maadili.
vii. Mila na desturi potofu mf wasanii kulogana,wanaume kulelewa
No comments:
Post a Comment