Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, June 13, 2013

Dalili za Matatizo ya Hedhi.

Kabla ya kuingia kwenye siku zako za hedhi wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira,husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa,matiti hujaa maziwa,hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri,hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (HOMONE IMBALANCE)na hali huweza kukomaa ndani ya saa 24..baada ya Hedhi.

Wengi mnapata maumivu makali,siku mbili au Tatu kabla..au mara tu muanzapo siku zenu,hali hii pia inasababishwa na kutowepo kwa uwiano wa homoni mwilini,ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani,wengi hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa ktk siku za Nifasi kuliko kawaida,huzuni na kadhalika.

ZIFUATAZO NI DAWA AMBAZO ZINASAIDIA KUTIBU
  • Mboga za Majani.kwanza upatikanaji wake ni rahisi kwahyo jitahdi sana kuzitumia asa juisi yake na supu ya mboga za majani
  • Papai,linasaidia kwa kiasi kikubwa,hususani Papai bichi hulainisha Misukosuko ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa Hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu.linasaidia sana hasa wale wasiopata siku zao kutokana na STRESS.!so kula mara kwa mara tunda hilo..na sio Bichi kabisa liwe limekomaa.!!
  • Ufuta,saga ufuta na Pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto,kunywa mara mbili kwa siku.!kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa Hedhi kwa wasichana wadogo.!pia husaidia kutibu kupata Hedhi kidogo.
  • Tangawizi,nayo ni dawa nzuri sana katika kutibu matatizo yatokanayo na Hedhi,hasa ktk tatizo la maumivu makali na kutopata Hedhi.Chukua kipande cha tangawizi mbichi kiponde na weka kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo,tumia mara mbili kwa siku baada ya mlo.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu