Enter your keyword

Culture for Life.

Thursday, June 13, 2013

Mafuta ya Ubuyu/Unga wa Ubuyu na Faida zake Mwilini.

Yana Virutubisho Vifuatavyo:
  • -Vitamin:  (Thiamin) vitamin B1, Riboflavin) B2, (Niacin) B3, kiasi kikubwa cha (Ascorbic Acid) Vitamin C, Vitamin A, Vitamin D, Antioxidant na Vitamin E (Tocopherol)
  • -Madini kama vile: – kiasi kikubwa cha Calcium, Manganese, Iron, Potassium, Zinc, Phosphorus, na Amino acids 

FAIDA ZAKE:-
  • Yanakuongezea hamu ya kula na kukumbuka vizuri kwa ufasaha kutokana na kiwango kikubwa cha vitamin B complex zilizomo. kwa hiyo ni mazuri kwa wakubwa na watoto
  • Yanasaidia kunyonywa kwa vitamin B12 kwenye tumbo kutokana na kiwango kikubwa cha ascorbic acid, ambayo ni muhimu kwenye kutengeneza chembe hai nyekundu na kukuepusha na Anemia.
  • Yanasaidia kusafisha mfumo wa chakula na kufunga tumbo la kuhara zaidi kwenye unga wa ubuyu kutokana na uwepo wa “Rufage” nyingi.
  • Yanasaidia mtu  kuona vizuri kutokana na uwepo wa Vitamin A ndani yake.
  • Mazuri kwa Walemavu wa Ngozi kama (Albino) Kutokana na uwepo wa vitamin A, Vitamin D na Vitamin E (Tocopherol).
  • Ni mazuri pia kwa watoto wadogo na  wajawazito kwa ajili  ya kuimalisha mifupa hasa  kuanzia miezi sita hadi tisa ya ujauzito (third tremester), hiki ni kipindi ambacho mtoto anatengeneza na kuimalisha mifupa yake akiwa tumboni kwa mama yake, hii ni kwasababu ya kiwango kikubwa cha Calcium na vitamin D, na vitamin A.
  • Mafuta haya ni mazuri kwa kupunguza vitambi kutokana na uwepo wa Omega 3.
  • Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini.
  • Hurekebisha shinikizo la damu (pressure).
  • Yanasaidia kuongeza kinga ya mwili yaani CD+4, zaidi kwa wagonjwa wa ukimwi, kansa, au watu waliougua kwa muda mrefu na wanawake wanapokuwa katika hedhi wanaweza kutumia.
MATUMIZI:-Tumia vijiko viwili vya mafuta kwenye kijiko ha chai, kisha changanya kwenye Glasi ya Maji, Juisi, Maziwa yanaweza kuwa mtindi au freshi, Soda, Asali n.k, au unaweza kunywa bila kuchanganya na kitu kingine. tumia hivyo  mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa mafanikio mema na matokeo mazuri.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu