Natumia Vaseline original,situmii vipodozi vyenye kemikali zaidi ya mafuta mgando usoni na lotion mwilini.Matumizi ya vitu vingi usoni husababisha sura kuwa na mikunjo au kuchoka na kuonekana mzee. |
Chunusi
ni ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa .
Chunusi huweza kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana
hasa wakati wa balehe Karibu asilimia 85 ya vijana kati ya umri wa
miaka 12 hadi 25 hupata chunusi na zaidi ya asilimia 20 ya wanawake
wenye umri wa zaidi ya miaka ishirini hupata chunusi wakati mwingine
hata watoto wadogo pia huweza kupata chunusi hii ni tofauti na watu
wengi wanavyofikiria kuwa chunusi ni dalili ya balehe.
Vipele
vinaweza kuwa vidogo au vikubwa. Chunusi wakati mwingine husababisha
mabaka katika ngozi hali hii hutokea pale ambapo seli za ngozi
zilizoharibika huondolewa na seli mpya kutengenezwa.Ngozi mpya
hutengenezwa kirahisi tu mahali palipokuwa na chunusi hali hii
husababisha mlingano usiosahihi wa ngozi na hutoa kidonda ambacho
baadaye hubaki kama baka. Chunusi hutokea zaidi katika uso,kifua ,mabega
na mgongoni.
Chanzo cha Chunusi
Chanzo halisi cha chunusi hakijulikani.hata hivyo baadhi ya vitu vinavyoongeza uwezekanifu wa kupata chunusi ni;
Umri
Kama
nilivyosema( hormone)vikemikali hutolewa kwa wingi sana mtu anapofikia
umri wa kubalehe.Kemikali hizi huongeza utengenezaji wa nta (sebum)
katika ngozi ambayo huchochea kutokea kwa chunusi
Vipodozi
Baadhi
ya vipodozi vya usoni(Make-up) za kina dada na Marashi(spray) za nywele
zina mafuta ambayo yanaweza kusababisha chunusi kuwa nyingi zaidi.
Chakula
Chunusi hazisababishwi na chakula bali baadhi ya vyakula hufanya chunusi kuwa nyingi zaidi.Hasa vyakula vyenye mafuta.
Dawa
Chunusi
zinaweza kujitokeza kutokana na kutumia dawa kadhaa kama vile
antibiotics,Vidonge vya uzazi wa mpango,Steroid ni dawa zenye homoni
zilizotengenezwa kitaalamu ambazo wakati mwingine wanariadha huzitumia
tofauti na makusudio ili kuongeza unene wa misuli yao.
Magonjwa
Magonjwa yatokanayo na matatizo katika vikemikali (hormonal disorders) huongeza matatizo ya chunusi hasa kwa wasichana
Mazingira
Chunusi
huweza kuwa nyingi zaidi hasa unapoishi mazingira yenye mafuta,grisi
au hewa chafu .Kutoa jasho sana hasa katika mazingira ya joto huongeza
uwezekano wa kupata chunusi.
Jinsia
Wavulana hupata sana chunusi kuliko wasichana.
Familia
Wakati mwingine chunusi hujitokeza sana kwa wanafamilia wa familia kadhaa kuliko nyingine.
Homoni
Mabadiliko
ya homoni za mwili hasa wakati mwanamke akiwa katika siku zake,ujauzito
au mwanamke anapokuwa na umri mkuwa hupelekea kupata chunusi.
Usafi wa mwili
Kutumia
sabuni zenye kemikali,kujisugua sana na kuzitoboatoboa chunusi au
vipele husababisha chunusi kuongezeka zaidi.Kukaa muda mrefu na jasho
mwilini au kutooga huongeza uwezekano wa kupata chunusi
Mawazo(Stress)
Mtu anapokuwa na mawazo mengi vikemikali kadha hutolewa mwilini ambavyo huweza kuchangia au kusababisha chunusi
Dalili za Chunusi
Vipele
au vivimbe vidogo vidogo ambavyo pengine husababisha mwasho au
vinavyouma ni dalili ya chunusi.Wakati mwingine huweza kujitokeza kama
baka dogo.
Ikumbukwe
kuwa kutokana mwonekano wa chunusi ni rahisi sana Daktari
kuzigundua,japokuwa katika familia zetu ni mara chache sana mtu akaenda
kumwona daktari au mtaalamu wa magonjwa ya ngozi kwa sababu ya
chunusi.Pale vinapotokea hivyo basi hali inakuwa ni mbaya zaidi.Hata
hivyo si vibaya kumwona daktari ambaye atakuuliza kuhusu,
chakula,ngozi,dawa unazotumia na vitu vingine vinavyoweza.kuchangia mtu
kupata chunusi
Matibabu
Matibabu
ya chunusi yanajumuisha kupunguza utoaji wa (sebamu ),kuondoa seli za
ngozi zilizokufa na kuua wadudu yaani bacteria.Matibabu huweza
kutofautiana kutokana na wingi au ukubwa wa tatizo. Suala la kuzingatia
ni kuepuka mambo yanayoweza kusababisha chunusi kama
nilivyokwishakueleza katika makala iliyopita.
Dawa za kupaka
Kuna
dawa za kupaka ambazo hupakwa katika eneo la ngozi lililoathirika kwa
chunusi.Dawa hizi hupatikana kama cream,losheni,jel .Dawa hizi hutumika
kutibu chunusi ambazo haziko katika hali mbaya hasa kama kuna vijipele
vidogo vidogo tu.
Dawa nyingine ni zile zinazolainisha nta na kufanya vishimo vya jasho kufunguka na dawa nyingine huongeza kasi ya utengenezwaji wa seli mpya za ngozi
Dawa
hizi za kupaka hushauriwa kupakwa angalau mara mbili au tatu kila siku
hasa baada ya kusafisha kwa maji safi na sabuni ya kawaida na kukausha
kwa taulo eneo lenye chunusi na matibabu yanaweza kuchukua wiki kadhaa.
.
Matibabu mbadala
Haya
hujumuisha lishe bora na usafi wa mwili.Ni vema kuoga mara kwa mara na
kujifuta maji kwa taulo safi na kuiweka ngozi katika hali ya ukavu na
kuepuka upakaji wa mafuta mengi ya mgando hasa wakati wa joto.
Watu
wenye chunusi wanashauriwa kula mlo kamili wenye vyakula vyenye madini
ya zinki,nyuzinyuzi,matunda , mboga za majani,vitamin B. Ni vema
kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe,vyakula vya
maziwa,tumbaku,sukari,vyakula vilivyoandaliwa viwandani na vyakula
vyenye Iodine nyingi kama vile chumvi.
Mambo ya kuzingatia ili usipate Chunusi
Hakuna njia sahihi ya kujizuia ila unaweza kufanya yafuatayo;
· Osha
taratibu sehemu unayodhani ina chunusi kwa maji safi na sabuni angalau
mara mbili kila siku huku ukisugua taratibu ,usikwaruze kwa kucha au
kitu chochote kigumu.
· Tumia Vipodozi au vilainisha ngozi visivyo na mafuta ya mgando
· Osha nywele zako kila mara na epuka nywele kuziba uso (kwa wenye nywele ndefu)
· Kula mlo kamili na epuka vyakula vyenye mafuta mengi.
· Usibinye au kutoboa vipele kwa pini au kitu chenye ncha kali.
· Epuka kukaa sana juani,mwanga wa asubuhi ni mzuri ili kupata vitamin D
· Punguza mawazo
Kumbuka kuwa chunusi haziwezi kutibika kabisa iwapo
matibabu yatakuwa sahihi watu 60 kati ya 100 hupona na unapokuwa
unatumia dawa usitarajie kupona haraka kwani inaweza kuchukua hata miezi
miwili kupata nafuu na zinaweza kujitokeza unapoacha kutumia
dawa.Chunusi pia huweza kupona kwa kuacha mabaka ambayo kwa hapa nchini
hakuna utaalamu sahihi wa kuyaondoa bali huweza kuondoka kadri muda
unavyoenda au kwa kemikali kali ambazo zinaweza kuwa na madhara katika
ngozi.
Ukitaka kuondoa chunusi usoni na kusafisha uso usiwe na madoa kwa nija ya kiasili, njia zifuatazo zaweza sana kukusaidia.Tafuta ukwaju loweka katika maji ukishalainika changanya na asali, paka usoni.Ni dawa nzuri sana na utaona ngozi yako inabadilika kwa kipindi kifupi.
Kama utashindwa kupata vitu hivyo tafuta sabuni pamoja na krimu yenye mchanganyiko wa asali na ukwaju,lakini nadhani asali na ukwaju kama utaenda sokoni ni rahisi kupata.Pia ni vema ukitumia losheni yenye mchanganyiko wa asali au ukwaju.
No comments:
Post a Comment