Ni wazi kuwa suala la ndoa kwa sasa ni kilio kwa wengi,Kila mtu ana namna ambavyo analichukulia suala hili,Ukisoma katika magazeti,kusikiliza redio,katika blog na kusikiliza mahubiri yana mtaka mwanamke kusimamia ndoa yake ili isiharibike,Ingawa sijafikia hatua hiyo lakini bado naona katika jamii yangu jinsi ambavyo wanawake wameachiwa majukumu mengi.
Leo naomba wanaume mtambue mchango wenu katika ndoa kwa kufanya haya:
Endelea kumpenda kwa kasi ile ile
Kumbuka wakati wa uchumba jinsi mlivyokuwa mkiishi,unamtumia ujumbe mzuri katika simu yake,pamoja na kumwambia maneno mazuri wakati wote unapokuwa karibu naye au mbali naye,mitoko mikali una mpa zawadi, Ulikuwa una mfanya akuamini hata unapokuwa mbali naye.Hayo mambo uliyokuwa ukiyafanya hata sasa yana nafasi yake na hata kama ndoa ilianza kuingia dosari utakapo fanya tena kwa kasi nyingine hakika ndoa yako itakuwa na furaha.
Kuwa msikivu na muulizaji wa mambo unayotaka majibu yake.
Ni kweli kwamba wanawake wanapenda kusikilizwa kwa umakini,ikiwa mkeo anazungumza na wewe na wewe unakuwa na michakato yako, lazima ataona kuwa unamdharau,Hapo lazima atajisikia vibaya na kuona kuwa kitu anachozungumza hakina faida.Hivyo basi kama mwaka 2016 hukuweza kufanya hivyo sasa ni wakati wako,Anapoaaza kuongea na wewe basi zima simu au weka mbali na wewe ,Tv zima au Punguza sauti.Hata asipotaka kukuambia mwambie mke wangu nahitaji kujua umefikia wapi katika biashara zako,kama anasoma muulize,uliza vitu unavyoamini anavifanya ,basi huenda hata hujui hata kimoja muulize swali la ujumla ili afunguke.
Kuwa mbunifu katika tendo la ndoa.
Hapa watu husahau kuwa tendo la ndoa ni muhimu kwa wanandoa,Muulize mkeo anapendelea nini katika tendo la ndoa mitindo gani anapenda,hata wakati mwingine badilisheni mazingira ya kufanyia sex,sehemu moja kila siku inachosha na kupunguza hamasa ya kufanya tendo lenyewe siku moja mfanyie suprise mama watoto toka hata n'je ya nyumba nendeni hata hotelini au mazingira ya nyumbani hapohapo kwa kutegemea mnaishije kama na familia lazima muwe makini lakini kama mpo wawili basi sehemu ni nyingi.Pia mwanaume jua sehemu zinazo mfanya mke wako afurahie tendo la ndoa ,hujui basi google kwasababu wanawake wengine si rahisi kuongea.
Tumia busara katika kutatua ugomvi.
Kuwa na mda wa kuzungumza na mke wako.
Ndiyo nyakati hizi za sayansi na teknolojia inasababisha pia wanandoa kugombana kwani mda mwingi hutumika katika simu au kompyuta na kukosa mda wa kuzungumza na mkeo.Ni vema kutenga mda wa kuzungumza na mwenzi wako kuliko kuwa busy mda wote na mitandao.Hata kama unatafuta pesa mwanamke anapenda mwanaume anayetenga mda wa kuwa naye japo hata lisa.
Mheshimu na kumjali Mke Wako.
Hakika ukifanya haya mwanamke atakupenda,atakujali na kukuheshimu pamoja na kumuona mkeo akiwa na furaha siku zote. kama utamfanyia haya basi naye ataongeza upendo zaidi kwako hata kufanya yale ambayo ajawahi kukufanyia ili mradi nawe ufurahi.
No comments:
Post a Comment