Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, June 26, 2015

JINSI YA KUTUMIA LIPSTICK(RANGI YA MDOMO)

By On June 26, 2015

KAMA UNA MIDOMO(LIPS)NDOGO HAKIKISHA USIKOREZE SANA LIPSTICK YAKO ITAFANYA MIDOMO YAKO IONEKANE VIBAYA.PAKA KISHA TUMIA WANJA KUUFANYA MUONEAKANO MZURI WA MDOMO WAKO.

KERRY WASHINGTON,LUPITA NYONGO NA RIHANNA,WOTE WAMEPAKA RANGI KULINGANA NA NGOZI ZAO.

BAADHI YA HIZO PICHA ZITAKUONGOZA NAMNA YA KUPAKA LIPSTICK  KULINGANA NA NGOZI YAKO.

MEN SUIT.

By On June 26, 2015

VAZI LA SUTI NI VAZI AMBALO UNAWEZA KUVAA OFISI,KWENYE MIKUTANO,HARUSINI,KANISANI N.K.


WANAUME WENGI HUPENDELEA RANGI NYEUSI,LAKINI TAMBUA KUWA KUNA RANGI AMBAZO HAZIJAZOELEKA ZIKIVALIWA VEMA ZINAVUTIA ZAIDI.

 

HAKIKISHA SUTI YAKO INAKUKAA VIZURI SIYO BEGA MOJA KUBWA LINGINE DOGO,MIKONO MIREFU KUZIDI MKONO WAKO N.K


PIA CHAGUA KITAMBAA KIZURI SI KILA KITAMBAA KINAFAA KWASUTI.


Friday, June 12, 2015

MISHONO MIPYA 10 YA VITENGE 2015

By On June 12, 2015

AFRICAN HEADWRAP(KILEMBA)

By On June 12, 2015
Zamani mimi wakati nakuwa miaka ya 90 huko ilikuwa ukijifunga kiremba kama hivi unaonekana mshamba ila hivi sasa ndiyo habari ya mjini,watu wanasema remba unaweza vaa kwenye pati,kanisani,msimbani,kazini na kwenye mtoko wako,isipokuwa ufungaji wa remba hili hutegemea pia mazingira unayo kwenda usije funga remba na mtoko msibani au remba la harusi msibani au kwenye mtoko au mishe zako.Leo katika safu hii ya ubunifu na mitindo nitatupia picha chache  jinsi ya kufunga Afrcan Headwrap

AFRICAN HEADWRAP


MAKENZ GOWN

AFRICAN HEADWRAP WITH SIMPLE MAKEUP


INGIZO JIPYA LA INDIAN LACE NA FRENCH LACE 2015

By On June 12, 2015

Purple Yoke lace gauni imechanganywa na satini.Bila kusahau kutupia remba(African Gele)


MITINDO YA VITENGE 2015.

By On June 12, 2015

REMBA NDIYO HABARI YA MJINI KWASASA USIPITWE,UNAWEZA KUTUMIA VITAMBAA VYA SATINI,VElVET,LACE,KITENGE n.k

MFANANO WA WANANDOA.

By On June 12, 2015





Hongera Wilfred Pastory na Queen Boaz (Mr&Mrs.Mushi)


Mambo matano ambayo wanandoa hufanana wanapokuwa pamoja kwa mda mrefu;
  1. Wewe na mpenzi wako kuwa na lugha binafsi(private language).Kadri wenza watumiavyo lugha binafsi hii huonesha kiasi gani huwa na furaha pamoja.Huweza kuitana majina ya utani ikiambatana na kutaniana.Hii hali hufanya mapenzi yao kuwa na furaha na yatofauti.
  2. Kuacha kujialaumu/kujikosoa(self-censoring).Ni wazi kuwa tunapokuwa tunaongea na rafiki,ndugu na jamaa huwa tuazungumza kwa kuangalia mazingira uliyopo lakini upozungumza na mpenzi wako uliyemzoea huwa unakuwa huru kuzungumza kama kawaida(Naturaly)bila kujali mazingira/unajiachilia.
  3. Mazungumzo hufanana(You start to sound alike)Watu waliokaa pamoja kwa mda mrefu ,wakati mwingine watu husema hufanana hadi sura,Ukweli ni kwamba watu hawa hufanana kimsamiati hata mpangilio wa sentensi zao huwa sawa.
  4. Hufanana.Wanandoa na wapokaa kwa pamoja kwa mda mrefu na kufanya vitu vingi pamoja hupelekea wao kufana.
  5. Kuwa na utani uliopitiliza.Wenza huweza kuelewana kwa ishara hata vitendo kabla ya mazungumzo kwasababu wanaelewana vema hata kwa kutazamana huweza kuzungumza yote inatokana na kukaa kwao kwa kipindi kirefu na kujuana vema,wakati mwingine huweza kutaniana na watu wanao wazunguka wakaona kuwa si utani lakini wao huona kawaida kwasababu wanaelewana vema.

Wednesday, June 10, 2015

NDOA NDOANO KATIKA JAMII....

By On June 10, 2015


Image result for tendo la ndoaImage result for tendo la ndoa
Katika safu hii nitazungumzia vitu vichache vinavyowafanya watu wasifurahie tendo la ndoa .Hapa nazungumza na wanandoa na wanaoelekea kungia katika ndoa.Leo tuangalie mambo baadhi kwa ufupi:
  1. Kuongelea matatizo wakati wa tendo la ndoa.Hapa mwanaume/mwanamke unapoona mwenzi wako anahamu na wewe baadala ya kusoma alama za nyakati wewe unaanza kuongelea shida zako,za ndugu hata majirani wakati mwingine mnaanza kukumbushiana majeraha mlio wahi kukwazana.Hii hali itawaoondoa katika raha mlio taka kuipata.Hapa sasa mmoja wapo anapotoka n’je na kukutana na mtu mwenye kusoma alama za nyakati utaipenda kwasababu utampoteza mwenza wako na hatokuwa na shauku na wewe.
  2. Kusumbuliwa na jinni mahaba,hili ni tatizo linalowakabiri wanandoa wengi hukosa hamu ya kufanya mapenzi na wenza wao hata kama alikuwa na shauku akiwa safarini kwamba nikifika mke/mme wangu basi leo nitafurahi lakini anapo mkaribia hamu ina isha.Watu wenye tabia hiyo jua anasumbuliwa na jini mahaba na baadhi ya dalili zao nikuota ndoto wanafanya mapenzi kwenye ndoto,kupoteza pete,kufunga harusi wakiwa katika ndoto n.k.Ukiona hivi wewe ingia katika maombi na ujitenge na hizo roho.
  3. Kutokuwa na Lugha ya mahaba .Wanaume/wanawake wengi huogopa kujiachilia na kumwambia mwenzi wako jinsi unavyojisikia,kuwa wazi kwa mwenzi wako usione aibu unapokuwa naye katika tendo la ndoa.Toa hata kiasauti kidogo hii itamfanya mwenzi wako kuona kuwa unamjali na mko pamoja hata unapo wahikufikia mshindo/kileleni usikae kama bubu endelea kumtia moyo mmeo/mkeo ikiwezekana mwambie aongeze kasi au apunguze mwambie unavyojisikia utamfanya aone kuwa bado una mpenda na akikukumbuka basi atakumbuka sauti zako na kuwa na hamu na wewe.
  4. Uchafu wa kitanda na chumba chetu.Hapa mwanamke ni jukumu lako kufanya chumba chenu kiwe kisafi mda wote.Wanawake wa siku hizi huu utandawazi utatumaliza na kuharibu ndoa zetu hasa tunapo waachia wadada wa kazi kufanya usafi wa chumba chenu.Mwanamke hakikisha huwaruhusu hata watoto kuingia chumbani kwako.kuwa na tabia ya kubadili shuka kila siku mumeo atavutiwa na kubadilisha muonekano wa chumba chako sio kila siku kitanda kina kaa kwenye dirisha au ukutatani.
  5. Uvivu wakati wa tendo la ndoa.Wanawake/wanaume wengi ni wavivu mwanamke usimwachie mumeo kukushughulikia tu wewe ukiwa umekaa kama gogo,wengine ukoroma kabisa hata kulala,hii huonesha dharau kwa mumeo pia wanaume wengine ni wavivu katika tendo la ndoa mshindo mmoja hoi,utampoteza mkeo ,wengine watakusaidia kazi.Mwisho kabisa napenda kuwaomba wanaume/wanawake kuzingatia usafi wa miili yetu  ikiwa ni pamoja na kunyoa nywele za makwapani,sehemu za siri na kusafisha vinywa vyetu  vizuri vilevile tupotaka kufanya tendo la ndoa  mkiweza nendeni hata bafuni muoge pamoja.Wanawake wenzangu ni vema ukiwa msafi zaidi na kujua kusafisha sehemu zetu vema hata kutumia vitu vya kuondoa harufu katika makwapa au vinywa vyetu ili waume zetu wasitukimbie.

FAIDA YA TENDO LA NDOA.

By On June 10, 2015


Image result for tendo la ndoa
Nitumaini langu wewe unayesoma makala hii ni mwanandoa au upo katika harakati za kuingia katika ndoa.Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa hufanywa na wana ndoa tu na siyo wachumba,marafiki na halifanyiki hovyohovyo tu bila makubaliano ya watu wawili nikiwa na maana ya wanandoa.
Image result for tendo la ndoa
1.Tendo hili ni muhimu kwani hufanya ndoa iendelee kuwepo.Ndiyo sababu wanandoa mmoja wapo anapokosa kupata ushirikiano kwa mwenza wake.hupelekea ndoa kuvunjika na kufanya mmoja wapo kutoka n’je ya ndoa.

2.Tendo la ndoa ni burudani kwa wanandoa.Wakati mwingine mtu anayekosa kufanya tendo hili katika ndoa hupelekea migogoro hata kununiana ndani ya nyumba,kuwa na msongo wa mawazo.

3.Hapa wanandoa wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujitoa.

4.lengo hasa la tendo la ndoa ni uzazi.Ili kuikamilisha ndoa lazima mpate watoto ndiyo sababu ya kuunganika na kuwa mwili mmoja.Kwasasa tendo la ndoa limekuwa likifanywa.kinyume,wengi wetu katika jamii wanafanya bila kuzingatiaa maadili ya hili tendo,mzee kwa kijana,mume au mke wa mtu,vijana,watoto walio chini ya miaka 18 pia wamejiingiza katika zinaa(Uzinzi).Mpenzi msomaji kama wewe ni mmoja wapo tulia kuwa na mmoja ambaye ni mume au mke wako ndiyo utafurahia tendo la ndoa.

JINSI WAZAZI WANAVYO WAHARIBU WATOTO .

By On June 10, 2015



Uelimshaji wa mtoto ni jukumu la kila mtu.Kumbuka kuwa moja ya vitu vinavyowachanganya watoto ni makuzi ya watoto katika mazingira wanayo lelewa.Leo katika safu napenda kuzungumzia baadhi vipengele ambavyo vitamuweka mtoto wako katika mazingira mazuri ikiwa wazazi watazingatia haya katika kuwa sahihisha watoto na wakuwarekebisha.

  1. Image result for watoto

    Usahihishaji wa dhana au maneno katika kuyaelewa na kuyatamka.mfano

     

Mtoto- Mtoto anaona mtoto wa Punda kisha anamwambia mama Mbwa.Hapa wazazi wengine huitikia ndiyo Mbwa bila kujua kuwa anampotosha mtoto.Mama ilitakiwa aseme hapana  ni mtoto wa Punda.Hapo mtoto wakati mwingine hatosema Mbwa anatasema mama Punda.

  1. Urekebishaji wa tabia,kukemea na kupongeza.Mtoto mwenye tabia ya kutukana anapaswa kukemea na anapokuwa na tabia nzuri anapaswa kupongezwa.
  2. Mpangilio sahihi wa maneno.(Sintaksia ya watoto)Mara nyingi wazazi hawazingatii urekebishaji wa makosa ya kisarufi kwa watoto zaidi huzingatia maana .Kimsingi mtoto anapaswa kufundishwa namna ya kupangilia maneno katika sentensi na katika matumizi ya nyakati.Mfano.
              Mtoto- Juma ataenda shule jana.
               Mtu mzima- Juma alienda shule jana.kumbuka kuwa mtoto mdogo anauwezo mkubwa wa kujifunza lugha kuliko mtu mzima.Hivyo basi mtoto anaporekebishwa akiwa mdogo hatoweza kukosea tena.






JINSI MTU MZIMA ANAVYOWEZA KUUTEKA USIKIVU WA MTOTO.

By On June 10, 2015

.
Image result for watoto

Mpenzi msomaji wa makala zangu, leo napenda kuwakumbusha watu wazima katika uzungumzaji wao hasa wanapo zungumza na watoto.Ifahamike kuwa siku zote mzungumzaji humtegemea msikilizaji anapozungumza.Ikiwa mtu mzima anaongea katika kundi la watoto ni vema akitumia nguvu kubwa ya ziada na kufanya yafuaatayo:



  1. Matumizi ya majina na alama za mshangao(Attention getters).Hii itasaidia kumuelekeza mtoto mazungumzo gain yanaelekezwa kwao na yapi yanayopaswa kusikilizwa.Matumizi ya majina na vichekeo hupatikana katika makundi mawili makubwa.mfano mtu mzima anapoongea na mtoto hutumia jina la mtoto la mwanzoni mfano.Irene njoo hapa,wakati mwingine hutumia alama za mshangao baadala ya kutumia majina,mfano aah! Mbona husikii. Alama hizi huwa kabla ya sentensi anyotaka kusema.
  2. Matumizi ya Vichekeo(Attention holders stimulus)vinavyovuta hisia.Hivi hutumika pale mzungumzaji anapotaka kuzungumza jambo zaidi ya moja.Mfano anaposimulia  hadithi.
  3. Ubadilishaji wa sauti(Attention holder)katika kipengele hiki kuna vitu vifuatavyo:Uzungumzaji wa sauti ya juu kwa watoto,mtu mzima huongea kwa sauti ya juu sana hasa anapoongea na mtoto wa miaka miwili,miaka mitano sauti ya juu kiasi..
  4. Unong’onezaji.Mtu mzima hutumia sauti ndogo ya kunong’oneza na watoto wao hasa wanapowalisha au anapombembeleza ili alale.Watu wazima hunong’oneza hasa wanapoongea na watoto wa miaka 2-5 lakini wanpozungumza na watu wazima hawa nong’oni.


3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu