Nitumaini langu wewe unayesoma makala hii ni mwanandoa au
upo katika harakati za kuingia katika ndoa.Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa
hufanywa na wana ndoa tu na siyo wachumba,marafiki na halifanyiki hovyohovyo tu
bila makubaliano ya watu wawili nikiwa na maana ya wanandoa.
1.Tendo hili ni muhimu kwani hufanya ndoa iendelee
kuwepo.Ndiyo sababu wanandoa mmoja wapo anapokosa kupata ushirikiano kwa mwenza
wake.hupelekea ndoa kuvunjika na kufanya mmoja wapo kutoka n’je ya ndoa.
2.Tendo la ndoa ni burudani kwa wanandoa.Wakati mwingine mtu
anayekosa kufanya tendo hili katika ndoa hupelekea migogoro hata kununiana
ndani ya nyumba,kuwa na msongo wa mawazo.
3.Hapa wanandoa wanatakiwa kuwa wavumilivu na kujitoa.
4.lengo hasa la tendo la ndoa ni uzazi.Ili kuikamilisha ndoa
lazima mpate watoto ndiyo sababu ya kuunganika na kuwa mwili mmoja.Kwasasa tendo
la ndoa limekuwa likifanywa.kinyume,wengi wetu katika jamii wanafanya bila
kuzingatiaa maadili ya hili tendo,mzee kwa kijana,mume au mke wa mtu,vijana,watoto
walio chini ya miaka 18 pia wamejiingiza katika zinaa(Uzinzi).Mpenzi msomaji
kama wewe ni mmoja wapo tulia kuwa na mmoja ambaye ni mume au mke wako ndiyo
utafurahia tendo la ndoa.
No comments:
Post a Comment