.
Mpenzi msomaji wa makala zangu, leo napenda kuwakumbusha watu wazima katika uzungumzaji wao hasa wanapo zungumza na watoto.Ifahamike kuwa siku zote mzungumzaji humtegemea msikilizaji anapozungumza.Ikiwa mtu mzima anaongea katika kundi la watoto ni vema akitumia nguvu kubwa ya ziada na kufanya yafuaatayo:
- Matumizi ya majina na alama za mshangao(Attention getters).Hii itasaidia kumuelekeza mtoto mazungumzo gain yanaelekezwa kwao na yapi yanayopaswa kusikilizwa.Matumizi ya majina na vichekeo hupatikana katika makundi mawili makubwa.mfano mtu mzima anapoongea na mtoto hutumia jina la mtoto la mwanzoni mfano.Irene njoo hapa,wakati mwingine hutumia alama za mshangao baadala ya kutumia majina,mfano aah! Mbona husikii. Alama hizi huwa kabla ya sentensi anyotaka kusema.
- Matumizi ya Vichekeo(Attention holders stimulus)vinavyovuta hisia.Hivi hutumika pale mzungumzaji anapotaka kuzungumza jambo zaidi ya moja.Mfano anaposimulia hadithi.
- Ubadilishaji wa sauti(Attention holder)katika kipengele hiki kuna vitu vifuatavyo:Uzungumzaji wa sauti ya juu kwa watoto,mtu mzima huongea kwa sauti ya juu sana hasa anapoongea na mtoto wa miaka miwili,miaka mitano sauti ya juu kiasi..
- Unong’onezaji.Mtu mzima hutumia sauti ndogo ya kunong’oneza na watoto wao hasa wanapowalisha au anapombembeleza ili alale.Watu wazima hunong’oneza hasa wanapoongea na watoto wa miaka 2-5 lakini wanpozungumza na watu wazima hawa nong’oni.
No comments:
Post a Comment