Uelimshaji wa mtoto ni jukumu la kila mtu.Kumbuka kuwa moja
ya vitu vinavyowachanganya watoto ni makuzi ya watoto katika mazingira wanayo
lelewa.Leo katika safu napenda kuzungumzia baadhi vipengele ambavyo vitamuweka
mtoto wako katika mazingira mazuri ikiwa wazazi watazingatia haya katika kuwa
sahihisha watoto na wakuwarekebisha.
-
Usahihishaji wa dhana au maneno katika kuyaelewa na kuyatamka.mfano
Mtoto- Mtoto anaona mtoto wa Punda kisha anamwambia mama Mbwa.Hapa
wazazi wengine huitikia ndiyo Mbwa bila kujua kuwa anampotosha mtoto.Mama
ilitakiwa aseme hapana ni mtoto wa
Punda.Hapo mtoto wakati mwingine hatosema Mbwa anatasema mama Punda.
- Urekebishaji wa tabia,kukemea na kupongeza.Mtoto mwenye tabia ya kutukana anapaswa kukemea na anapokuwa na tabia nzuri anapaswa kupongezwa.
- Mpangilio sahihi wa maneno.(Sintaksia ya watoto)Mara nyingi wazazi hawazingatii urekebishaji wa makosa ya kisarufi kwa watoto zaidi huzingatia maana .Kimsingi mtoto anapaswa kufundishwa namna ya kupangilia maneno katika sentensi na katika matumizi ya nyakati.Mfano.
Mtoto- Juma ataenda shule jana.
Mtu mzima- Juma alienda shule
jana.kumbuka kuwa mtoto mdogo anauwezo mkubwa wa kujifunza lugha kuliko mtu
mzima.Hivyo basi mtoto anaporekebishwa akiwa mdogo hatoweza kukosea tena.
No comments:
Post a Comment