Enter your keyword

Culture for Life.

Friday, June 12, 2015

MFANANO WA WANANDOA.






Hongera Wilfred Pastory na Queen Boaz (Mr&Mrs.Mushi)


Mambo matano ambayo wanandoa hufanana wanapokuwa pamoja kwa mda mrefu;
  1. Wewe na mpenzi wako kuwa na lugha binafsi(private language).Kadri wenza watumiavyo lugha binafsi hii huonesha kiasi gani huwa na furaha pamoja.Huweza kuitana majina ya utani ikiambatana na kutaniana.Hii hali hufanya mapenzi yao kuwa na furaha na yatofauti.
  2. Kuacha kujialaumu/kujikosoa(self-censoring).Ni wazi kuwa tunapokuwa tunaongea na rafiki,ndugu na jamaa huwa tuazungumza kwa kuangalia mazingira uliyopo lakini upozungumza na mpenzi wako uliyemzoea huwa unakuwa huru kuzungumza kama kawaida(Naturaly)bila kujali mazingira/unajiachilia.
  3. Mazungumzo hufanana(You start to sound alike)Watu waliokaa pamoja kwa mda mrefu ,wakati mwingine watu husema hufanana hadi sura,Ukweli ni kwamba watu hawa hufanana kimsamiati hata mpangilio wa sentensi zao huwa sawa.
  4. Hufanana.Wanandoa na wapokaa kwa pamoja kwa mda mrefu na kufanya vitu vingi pamoja hupelekea wao kufana.
  5. Kuwa na utani uliopitiliza.Wenza huweza kuelewana kwa ishara hata vitendo kabla ya mazungumzo kwasababu wanaelewana vema hata kwa kutazamana huweza kuzungumza yote inatokana na kukaa kwao kwa kipindi kirefu na kujuana vema,wakati mwingine huweza kutaniana na watu wanao wazunguka wakaona kuwa si utani lakini wao huona kawaida kwasababu wanaelewana vema.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu