Jinsi ya kusafisha Unyayo
Si kitu cha ajabu katika saluni zetu kuwakuta wanawake wakisafishwa kucha na kupakwa rangi ili kuvutia miguu yao.Usafishaji na utunzaji wa miili yetu ni jukumu letu kufanya hivyo ili kuendelea kuvutia zaidi.
Leo katika safu hii ya urembo napenda nizungumzie suala hili la usafishaji wa unyayo.Wapo wanawake au wanaume ambao miguu yao huchanika, kuwa na fangasi au kuwa na funza kutokana na mazingira tunayoishi na jinsi tunavyotunza nyayo zetu, wengi wetu tunajisahau katika jukumu hili la kusafisha nyayo zetu.
Zifuatazo ni njia za utunzaji wa Unyayo
Jitahidi kila siku kuosha unyayo wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni, kabla hujaanza kusafisha unyayo wako weka miguu katika maji ya moto kiasi, kwa muda wa dakika 5 kisha anza kusafisha kwa sabuni.
Changanya maji yako na asali, ambayo husaidia kulainisha ngozi ya Unyayo wako pamoja na kuondoa michubuko iliyopo katika Unyayo.
Ukimaliza kuosha Unyayo wako, hakikisha unajikausha na kitambaa kikavu kuanzia katika vidole vyako. Usipo kausha vema hupelekea kupata fangasi na kupelekea miguu kunuka unapokuwa umevaa viatu vya kudumbukiza.Watu walio chanika miguu wanashauriwa kutumia viatu vya wazi kwa muda mrefu huku ukizingatia taaratibu za usafishaji wa nyayo, pia unaweza kutumia cream za kulainisha Unyayo wako ambazo hupatikana katika maduka ya vipodozi.
Pendelea kutumia mafuta ya watoto kujipaka katika Unyayo wako(baby Oil) au paka Grisalini(glyceline) kwenye unyayo kisha vaa soksi wakati wa kulala, Soksi husadia kulainisha Unyayo wako kutokana na hali ya joto inayokuwepo ndani ya soksi.
Ongeza kiwango cha kunywa maji, kila siku jitahidi kunywa angalau lita moja ya maji ambayo husadia ngozi yako kuendelea kuwa nyororo.
No comments:
Post a Comment