Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, January 19, 2013

Historia ya lugha ya kiswahili

 HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI.
Kiswahili ni lugha ambayo inawekwa katika kundi la lugha za Kibantu. Neno “Swahili” linatokana  na neno la Kiarabu “sahel” linalomaanisha “sawahil” na katika Kiswahili ni “mpaka” au “pwani”(linalotumika kama kivumishi kumaanisha “wakazi wa pwani”. Kuongeza kwa herufi mbili za “ki” [‘lugha’] kupata “Kiswahili” kumaanisha “lugha ya pwani”. Wakati mwingine, neno “sahel” linatumika kumaanisha “mpaka wa jangwa la Sahara”. Unganishaji wa herufi ‘i’ mwisho wa neno “Kiswahili” ni kutokana na umbo la  kivumishi katika lugha ya Arabu (‘sawahil’). Jambo la hakika ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo imeazima maneno kutoka Kiarabu, Kiuajemi, Kireno na hivi karibuni Kiingereza. Hali hiyo, imekifanya Kiswahili kufika kiwango cha lugha ya kisasaZamani, Waswahili walitumia utawala wa mfumo wa mamlaka moja. Karibu na karne ya 10, pwani nzima ya Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa mfalme mmoja ambaye aliishi katika mji mkuu wa Safala.

Karibia karne ya 14, jamii ya Waswahili ilibadilishwa kuwa nchi yenye miji ya kisasa. Miji mingi hiyo ilikuwa midogo yenye majengo ya jiwe, misikiti, familia ya Waislamu walio na tabaka la juu na wengine wengi ambao hawakuwa Waislamu. Majiji makubwa kama Mogadishu, Pate, Mombasa, Malindi, Zanzibar na Kilwa yalijengwa na marijani na matumbawe ambayo yalionesha dalili za utajiri kwani yalikuwa  na vifaa vya ujenzi  vya gharama sana. Idadi kubwa ya majiji hayo yalikuwa chini ya utawala wa Sultani ambaye alikuwa Mwislamu. Ilifika kipindi ambacho majiji makubwa hayo yalitawala mengine ambayo hayakuwa na uwezo wa kuchukua mamlaka. Kwa mfano, Sultani wa Kilwa alitawala sehemu kubwa ya pwani ikiwemo Sofala na Zanzibar. karne ya 14 (kipindi cha mwaka 1390) idadi kubwa ya miji iliyotawaliwa na Masultani wa Omani kama Sofala ilianza kupata uhuru. Kuanzia karne ya 8 mpaka 19, Kiswahili kilizumgumzwa na makabila kadhaa kwa umbali wa maili 1000 kwenye pwani ya Afrika Mashariki kati ya Mozambique na kusini kwa Somalia.

Kwa mamia ya miaka,sehemuambazo palikuwa na Waswahili palikuwa vituo vya biashara muhimu kati ya wenyeji na nchi kama Arabia, India na Asia Mashariki na raslimali za Afrika Mashariki. Ushirikiano huu wa kibiashara uliathiri jamii ya wenyeji (Waswahili), utamaduni, dini na lugha  katika Afrika Mashariki. Katika enzi za karne ya 19, Kisiwa cha Zanzibar kilikuwa kituo kikuu na cha umuhimu kwa ajili ya biashara iliyokuwapo kwenye pwani ya Afrika Mashariki; sehemu ambapo safari ya watu na usafirishaji wa bidhaa kwenda katikati ya eneo hilo (Afrika Mashariki). Wakati huo, Kiswahili kilitumika kama lugha ya biashara na ya mawasiliano. Kutokana na hali hii, watu wengi ambao ni Waswahili walihamia kuishi kwingine hasa katikati ya Afrika Mashariki kwa lengo la kufanya biashara.

Naye Profesa Whiteley (1969), amefafanua hali hii akisema,“Wakati upanuzi wa biashara ulipobadili mbinu ya biashara kwa kutumia msafara kutoka pwani, haja ya kuhitaji lugha muafaka wa biashara ulikuwa muhimu sana na hapo ndipo Kiswahili kilipojizindua jukwaani”.(“When the expansion of trade shifted the initiative to caravan from the coast, the need for an effective lingua franca became acute and Swahili came into its own”).Baadaye, yaani katika karne ya 20, wakati wa ukoloni wa Uingereza, lahaja ya Unguja (aina ya Kiswahili iliyotumiwa na Wazanzibari ilienea sana Tanzania na aina nyingine ya Kiswahili ilienea mpaka Kenya, Uganda, Burundi, Congo, Mozambique na ilifika mbali sana hata mpaka Afrika Kusini. Aina hii ya Unguja ilikuwa imeathirika sana na Kiarabu.

Aina nyingine zilizojitenga kutoka Unguja zilipitia mabadiliko tofauti wakati wa usambazaji wa Kiswahili. Kwa sasa, tuna aina nyingi za Kiswahili zinazotofautiana angalau kidogo sana katika lugha hii ya Kiswahili. Ni muhimu kukumbuka kwamba kulikuwa na sababu moja ambayo ilisababisha usambaaji wa Kiswahili. Hii ilikuwa hali ya kuoana miongoni mwa wafanyabiashara (ambao walikuwa Waswahili) na wenyeji ambao wengi walikuwa watumwa. Inakubalika bila shaka kwamba watoto waliozaliwa na familia ya mchanganyiko huo walipata nafasi ya kujua na kuongea Kiswahili.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu