Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 15, 2012

Jinsi ya kuvaa Stoking

 (Stoking)

 

Stokingi ni vazi ambalo limeshika kasi sana siku hizi, watu wengine uliita vazi hili soksi chupi au soksi ndefu kutokana na muundo wake ulivyo,Vazi hili huvaliwa na rika zote,wengi hupendelea kuvaa kwasababu huwasaidia kustili miili yao huku wengine wakilitumia kujizuia baridi.Katika safu yetu hii ya urembo na mitindo

nitakupatia dondoo chache za vazi hili na namna linavyostahili kuvaliwa:

Chagua rangi sahihi ya stokingi yako:

Watu wengi hawako Makini  katika  rangi za nguo, unatakiwa kujua  mpangilio wa rangi za nguo utakazo vaa (combination of color) ilikukupa muonekano mzuri.

Siku hizi mtindo huo wa kuchanganya rangi wameupa jina la kachumbari,mambo ya kuoanisha(match) kiatu na nguo,mkanda labda na rangi ya nguo au mkoba,

yamepitwa na wakati kwa sasa lakini ni vema kupangilia vizuri mavazi yako ili uweze kuvutia zaidi.Uvaaji wa  stokingi huongeza kitu kipya katika vazi lako kama ni

gauni au sketi ya jinsi au kitambaa.Kitu cha msingi ni kujua rangi ya stokingi utakayovaa pamoja na hilo gauni au sketi yako.Wakati mwingine ukikosea kuvaa vazi hili

 kwa kufanya chaguo ambalo si sahihi utaonekana kituko mbele za watu.

 

Unapokuwa umevaa stokingi kwa ajili ya kuelekea kwenye sherehe,harusi au kwenye mtoko na mpenzi wako au rafiki lazima utahitaji kuonekana bomba zaidi.

Hivyo basi ni vema ukitambua rangi sahihi za kuvalia siku hiyo.Nikiwa na maana kuwa  stokingi nyekundu,bluu,kijani,au njano na rangi zinginezo,rangi hizo ni vigumu

sana katika kutaka kuoanisha (match) na gauni au sketi na ikiwa utavaa  stokingi za rangi hizo unaweza kuonekana kituko katika ulimwengu huu wa mitindo.Gauni

 nyeusi au nyeupe rangi hizo za stokingi lazima zitaendana na gauni lako,rangi nyeusi na nyeupe ni rahisi kuoana(match) na rangi zingine.Hakikisha umejitazama katika

 kioo kabla ya kutoka n'je kwasababu rangi zingine za stokingi hazipendezi kuvalia magauni yenye rangi.Pendelea stokingi nyeusi zaidi ambazo ni rahisi kuvalia na

gauni au sketi rangi tofauti.

 

Stokingi za wavu(fish net stocking)

Hizi ni stokingi za kipekee,stokingi zenye muundo wa wavu ni vema kuzivaa na gauni nyeusi ambayo kwa asilimia kubwa inaonyesha
miguu yako kutokana na kwamba stokingi nyingi ni nyeusi,pia unaweza kuvaa na gauni nyeusi ,nyeupe,hudhurungi au kahawia hata gauni la njano.Wakati mwingine
stokingi za wavu unaweza kuvaa unapokwenda disko kutokana na jinsi muundo wake ulivyo.Hakikisha huvai aina hii ya stokingi na gauni au sketi fupi sana kulingana na utamaduni wetu kwasababu stokingi hizi huonyesha ngozi yako.

stokingi nzito

Hizi ni zile stokingi ambazo sio nyepesi na si rahisi kuonyesha ngozi ya mtu aliyevaa,Wengi hupendelea kuvaa stokingi hizi ili kuficha miguu yao wengine huvaa kipindi
cha baridi ilikupata joto, pia unaweza kuvaa  na viatu virefu au viatu vya kudumbukiza.Kama huelewei ni rangi gani? ya stokingi ina kufaa basi pendelea kuvaa stokingi zenye rangi ya ngozi yako.
Watu wengine uvaaji wa stokingi ni sehemu ya maisha yao, haiwezi kupita wiki bila kutupia stokingi kwa ndani hivyo basi kama wewe ni mpenzi wa vazi hili
jaribu kuchagua rangi sahihi itakayo endana na vazi lako ili kukupa mwonekano mzuri zaidi katika vazi utakalo kuwa umevalia.Ukivaa stokingi na viatu vya wazi  lazima utaonekana kituko.

abnerytupokigwe@gmail.com





No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu