Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 15, 2012

Umuhimu wa tikiti maji kwa wanaume


Umuhimu wa Tikitimaji(Watermelon) kwa wanaume

Nitumaini langu kuwa tunda hili sio geni masikioni kwa wengi,Hivyo basi
naomba leo niweze kuwa elezea umuhimu wa tunda hili kwa ambao hawafahamu na inawezekana wengine wanalitumia bila kujua faida ya tunda hili kiafya. Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, 'Potassium', 'Magnesium' na virutubisho vinginekibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha
hisia za kimwili na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (ErectileDysfunction).

Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta
mhemuko wa mwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za
kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya
damu na kuufanya mzunguko wa damu mwilini kuwa rahisi bila athari
yoyote mbaya.

Upungufu wa nguvu za kiume au Ugumba.
Tikitimaji lina kirutubisho aina ya'arginine', ambacho huchochea uzalishaji wa 'nitric oxide' kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa yaViagra.

Utafiti uliofanyika  kwa wanaume 50 waliokuwa na matatizo ya nguvu za kiume,
ulionesha kuwa wanaume hao waliweza kufanya tendo la ndoa baada ya
kupewa vidonge lishe (food supplement) venye kirutubisho aina ya'arginine'.

Misuli
Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya 'Potassium' kama vile
Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo.
Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali,
huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
Husaidia kupunguza uzito wa mwili.
Tikitimaji ni tunda lenye  kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango
kikubwa cha maji, hivyo kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili
linaweza kumsaidia kwa kula kwa wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo
kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana, hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia
na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima na bila kuathirika kiafya.

Huimarisha kinga ya mwili.
Kirutubisho cha 'arginine' kilichomo kwenye Tikitimaji kina kazi nyingi
mwilini, mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea
kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Kama unavyojua, kinga
ya mwili ndiyo msingi wa afya bora, kwani ukiwa na kinga imara huwezi
kusumbuliwa na maradhi hata siku moja.

Huondoa sumu mwilini
'Arginine' vilevile hufanya kazi muhimu ya uponyaji madonda na kuondoa
'ammonia' na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu
kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.

Faida zingine
Faida za Tikitimaji kiafya ni nyingi, tunda hili hufaa kuliwa na
wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza
nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo
yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa
ya tumbo.

Kumbuka
Matunda kama haya hupaswa kuliwa mara kwa mara na wakati ungali mzima
ili kuupa kinga mwili wako ilikujikinga na maradhi wenyewe, usisubiri
mpaka upatwe na maradhi hayo na kwa kuambiwa na daktari ndiyo uanze
kula, kumbuka siku zote kinga ni bora kuliko tiba!

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu