Enter your keyword

Culture for Life.

Saturday, December 15, 2012

Upambaji wa chumba

Upambaji wa Chumba
Chumba ni sehemu muhimu kuliko mahali popote katika nyumba.Tulio wengi huona sehemu hii kama mahali pa kupumzika pale tunapokuwa tumechoka na wakati wa kulala ndipo huwa tunakumbuka eneo hili.
Fahamu kuwa hamna sehemu iliyo na maana sana katika maisha yetu kama chumbani au sehemu ya kulala.
Sehemu hii inapaswa kuwa tulivu, safi na yenye vitu  vichache, Unapoweka vitu vichache ndani ya chumba chako utakifanya kiwe na  hewa nzuri nzuri zaidi.
Chumbani  ni mahali ambapo unaweza kupumzisha ubongo wako na kufikiria mikakati   ya kimaendeleo na ukaweza kupata wazo jipya lakini yote hayo utayapata endapo chumba chako kitakuwa kisafi, tulivu pamoja hewa nzuri.
Zifuatazo ni dondoo za upambaji wa chumba:
Mwanga
Chumba kinapopata  mwanga wakutosha huvutia zaidi  na kuwa na hewa ya kutosha.
Ninapo zungumzia mwanga nina maanisha mwanga kutoka dirishani, mwanga wa taa za chumbani ambazo uwekaji wake upo tafauti kulingana na uwezo ulio nao, kuna taa ambazo huwekwa chini, ukutani au zile ambazo huwa pembezoni mwa kitanda. Mwanga wa taa ya chumbani hupaswa kuwa hafifu.
Rangi.
Katika uchaguzi wa rangi ni pamoja na rangi ya ukuta wa chumba chako, mapazia, shuka, pamoja na rangi za mito. Hapa inategemea unapendelea rangi gani lakini unashauriwa rangi za chumbani ziwe rangi ambazo ni tulivu.
Sehemu ya joto utatakiwa kuweka mapazia ambayo sio mazito, katika hali ya baridi tumia mapazia mazito pia ni muhimu kuzingatia rangi, usipendelee rangi zitakazofanya chumba chako kuwa giza.
Pendelea mashuka yenye rangi moja au yenye maua machache. unapaswa kutumia rangi ambazo huonyesha usafi mfano rangi nyeupe.
Unaweza kuchanganya na rangi zingine katika mito yako ya kitandani.Ubunifu katika utandikaji wa kitanda chako ni muhimu ili kiweze kukuvutia muda wote.
Sakafu
Kuna watu wanaopenda kutumia Mazulia (carpets) chumbani. Jaribu  kuchagua rangi nzuri aidha inayoendana na ukuta wako wa chumbani, ilikuleta muonekano mzuri pia unashauriwa kapeti lisiingie chini ya kitanda ili kukupa  urahisi wakati wa kufanya usafi.
Ni muhimu kusafisha zulia lako ili kuondoa vumbi na kuepuka kupata mafua. Pia ni vema kuwa na tabia ya kulitoa maramoja moja ili kuweza kusafisha sakafu yako na kuondoa harufu ya unyevunyevu  uliopo chini ya zulia.
Mwisho zingatia kuweka vitu vichache chumbani na kuwa na mpangilio mzuri wa vitu ndani ya chumba chako.

No comments:

Post a Comment

3 Bora Zangu

Inayotazamwa Sana

Jinsi Ya Kuufanikisha Mwaka 2017

Mpenzi msomaji wa Makala zangu kwanza kabisa nachukua fursa hii kuwashukuru wote mnaofuatilia Blog yangu,Naomba niwatakie heri ya Mwaka Mpya...

Watazamaji Wangu