Vitu vya msingi
kwa mwanamke katika Mkoba(Hand
bag )wako.
Na Tupokigwe Abnery
Naomba leo tukumbushane mambo matano ambayo yanaweza
kuwa msaada kwetu.Wanawake tunamambo mengi na wakati mwingine tunaweza kushau
mambo ya msingi kutokana na kutokuwa na mpangilio mzuri,
Hivyo basi ilikuondokana na tabia hii ni vema leo
katika safu yetu ya Urembo na mitindo tukumbushane mambo hayo matano:
Pochi
Ni muhimu kuwa na pochi ndani ya mkoba wako ambayo
itakuwa na pesa,kadi ya benki,vitambulisho na vitu vingine ambavyo unaweza uka
weka katika pochi yako.Hii itakusaidia kujua vitu kama
hivyo vipo sehemu gani katika pochi yako
kuliko kufungua mkoba mzima na kuanza kutafuta.
Simu
Nafahamu kuwa ni vigumu kutembea bila simu hivyo
basi chagua sehemu maalumu ambayo utakuwa unaiweka simu yako hasa katika mifuko ya ndani ya Mkoba ,
ilikuhakikisha kuwa usahau sehemu ulio
weka na kuondoa usumbufu wa kukagua begi zima simu itakapoita au wakati
ukihitaji kuitumia.
Funguo
Tusisahau funguo maana utakapoteza itakufanya
uzunguke siku nzima kutafuta hasa sehemu ulizo pita katika mizunguko yako na huu msururu wa magari barabarani utakufanya uchanganyikiwe zaidi.
Kipochi
kidogo
Ni vema ukiwa
na kipochi kidogo kwa ajili ya kuwekea
vitu kama rangi za midomo(lipstics),wanja,poda,mafuta,vitana,ilikuzuia
mpangilio mbaya wa vitu ndani ya mkoba wako pia kuzuia kuchafua mkoba endapo
vikimwagika .
Daftari(Notebook)
na kalaamu
Litakusaidia kujua vitu unavyohitaji kununua na pia
utaweza kuorodhesha vitu ulivyo nunua,kwa wale wenye tabia ya kusahau vitu alivyopangilia kuvifanya mahali anapo
kwenda na hukumbuka wakati amekwisha
rudi nyumbani nadhani daftari ni la msingi sana kwao.
No comments:
Post a Comment